Hivi ni sahihi kwa wakati mmoja kusoma na kufanya kazi?

rbsharia

Member
Sep 14, 2011
41
6
Kwa kawaida hapa nchini kwetu tumezoea kusema mimi nafanya kazi huku napiga shule. Na hapo hapo tunaambiwa kuwa mshika mawili moja humponyoka.
Kwa upande wangu mimi naona sio sahihi sababu ili jambo lifanyike kwa ufanisi linahitaji muda mwingi zaidi. Je, mambo mawili kwa wakati mmoja mtu utaweza kujigawa 50% kwa 50% ?
 
Kwa kawaida hapa nchini kwetu tumezoea kusema mimi nafanya kazi huku napiga shule. Na hapo hapo tunaambiwa kuwa mshika mawili moja humponyoka.
Kwa upande wangu mimi naona sio sahihi sababu ili jambo lifanyike kwa ufanisi linahitaji muda mwingi zaidi. Je, mambo mawili kwa wakati mmoja mtu utaweza kujigawa 50% kwa 50% ?

shughuli za kiuchumi ndo zinatufanya hivyo hakuna jinsi lakini inawezekana.
 
Kwa m2 ambae yuko kazni thn akaenda chuo,maisha kwake ni mazuri sana aisee,kwanza haishiwi na weng wao huwa ni wa2 ambao tayar wanajua maisha ni nin kuliko m2 anaetoka shulen direct.
 
Mimi naona ni sahihi kabisa kufanya hivyo endapo mtu kama huyo ana uelewa mkubwa, seama sisi watanzania tumekuwa wavivu sana kufanya kazi ndio maana Waziri mkuu akitushauri 2chape kazi 2ache malumbano,
Hivyo basi kama mtu ana mda wakutosha kusoma na kufanya maana haina maana yeyeote ile kwa waajiri kuwabania watu kama hao!!!!!!!!!
 
Ni sahihi, hakuna ubaya. Hiyo itategemea na mwajiri wako na namna wewe utaweza pangilia muda wako.
 
yah thats is very cool and m doing that... nasoma huku nafanya kazi na mambo yanakwenda
 
Mkuu ni sahihi kbc,mm nilipata kazi nikiwa mwaka wa pili chuoni na mpk namaliza maendeleo yangu kimasomo yalikuwa mazuri tu,kikubwa ni kuwa makini na kuutumia vzr muda unaoupata baada ya kazi.
 
rbsharia; Kwa kawaida hapa nchini kwetu tumezoea kusema mimi nafanya kazi huku napiga shule. Na hapo hapo tunaambiwa kuwa mshika mawili moja humponyoka.Kwa upande wangu mimi naona sio sahihi sababu ili jambo lifanyike kwa ufanisi linahitaji muda mwingi zaidi. Je, mambo mawili kwa wakati mmoja mtu utaweza kujigawa 50% kwa 50% ?Mkuu, Inawezekana kabisa, mara nyingi kwa graduate level nimeona wengi wanafanya hivyo.Kufanya vizuri kwenye masomo haijalishi kuwa upo full time, unaweza kufanya kazi na bado ukafanya vizuri kwenye shule yako pia. Ni kupangilia mda na kujima usingizi kidogo mambo yanaenda.
 
Dah! Ama kweli penye wengi hakiharibiki kitu, mimi nilikuwa naamini kuwa kufanya kazi huku ukiwa unasoma ni ngumu sana sababu huku unahitajika na huku unahitajika lakini kumbe si hivyo.

Je, na wale wanaoamua kuahirisha masomo na kufanya kazi tu tatizo linakuwa ni nini? Au ndio wameshindwa kumaintain 50% kwa 50% ?
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom