Hivi ni sahihi kuanzisha kanisa unapohisi una upako?

Huwezi kuhisi kuwa una upako isipokuwa unaweza kujua kuwa una upako. Kwa mfano, Mzee wa Upako Mch. Anthony Lusekelo, anajua kuwa ana upako, huwa hahisi kuwa ana upako.
Ukiona unahisi, huyo siyo Roho Mtakatifu (RM). RM huwa hawezi kuongea na muumini halafu akamuacha kwenye mashaka. Ukiona uko kwenye mashaka na unauliza lakini bado unaendelea kuwa kwenye mashaka, hapo unakuwa hujajibiwa. Kwa hiyo, hali hiyo uliyonayo wewe sasa hivi, nakushauri usifanye hilo jambo, bado hujaitwa! Usije ukalazimisha halafu ukawa uanasimama madhabahuni unaanza kurusha mapepo kwa waumini. Haya nayo pia yapo hasa kwa wale ambao hawakuitwa bali walilazimisha, wakiwa wanatafuta ajira Kanisani, tumeshayaona yapo!
We uhakika wa kuamini mzee wa upako ana upako kweli umeujuaje?

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Mungu alishawahi kuwatumia hadi makahaba kama akina Rahabu, na kuna nabii fulani, (nadhani ni yule aliyewahi kuongezewa umri wa kuishi miaka 15) aliambiwa aende akaoe kahaba.
Sikatai kuwa Mungu ni mtakatifu, na anahitaji utakatifu ila kumbuka pia amesema kuwa "njia zangi si njia zenu.........". Mungu anajua kila kitu, Anaweza kila kitu, Yuko kila mahali. Hata hapo ulipo wewe sasa hivi yupo pia
Kila alichokiumba Mungu ni kitakatifu kwake na anaweza kukitumia kama apendavyo yeye.
Nachelea kusema kuwa wewe ni mmojawapo kati ya watu wale ambao wamenyimwa kabisa roho ya kichungaji, huna hekima hiyo. Waache wale ambao wamepewa karama hiyo wamtumikie Mungu usiwabigudhi, usije mwishowe ukamsababisha akakugeukia na kukutandika
Mkuu umemiss kitu kidogo na ni cha muhimu,sijakataa Mungu kumtumia mtu aliyekuwa kahaba au mlevi au mwizi,ulichomiss ni mtu kuendelea na ukahaba au wizi wakati tayari anamtumikia Mungu hapo tu umekosea.Hao unaowasema walikuwa makahaba kabla ya kutumiwa,je baada ya kuanza kumtumikia Mungu waliendelea kuwa makahaba?Sasa linganisha na huyo ndugu in subject,video za kulewa zilikuwa kabla ya huduma au wakati anafanya huduma?Hapo tu ndiyo huwa mnapotezwa.
 
Mimi huwa nalia na mitume na manabii wanaoishi kifahari, nyumba,magari, helicopter,ndege,mabaunsa,nk huku waumini wakiwa masikini dhoofu hali.
Anzisheni hata vyuo vya maarifa mfano ufundi cherehani, udereva,kilimo, seminar za ujasiliamali nk kisha waumini masikini wasome bure kwa gharama za sadaka zao kuliko kuishi kifahari kesho mtaulizwa.
 
Kanisa n biashara nzuri isiyo lipiwa kod hakuna Cha upako wala nn n mbinu ya kukwara sadaka
 
Idadi ya makanisa lazima iendane na idadi ya Bar na Grosari zilizojaa mitaani.

Idadi ya madhehebu lazima izidi idadi ya viwanda vya bia na pombe kali.

Kitoko
Cucer
SmartG
Double Kick
KVant n.k
Hili ndo lakuzingatiwa. Siyo kijiji kina bar mbili makanisa kumi na nne
 
Back
Top Bottom