Hivi ni sahihi kuamini Magufuli alikuwa hajui ni lini wizara ya TAMISEMI inatarajia kukamilika katika mji wa kiserikali pale Dodoma?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
37,593
2,000
Nauliza swali hili kwasababu tumeona waziri mkuu akienda katika eneo husika kukagua ujenzi wa majengo yale zaidi ya mara moja huku akipewa taarifa ya maendeleo ya ujenzi na hilo jengo la TAMISEMI tuliambiwa lenyewe ndio lingekuwa la ghorafa na hivyo ni wazi lingechukua muda zaidi na hizi taarifa naamini waziri mkuu alikuwa anazifikisha kwa Rais.

Sasa cha kujiuliza,TAMISEMI wangeweza kujenga hilo jengo bila ridhaa ya Rais?

Na je,katika vikao ya baraza la mawaziri,walikuwa hawajadiliani maendeleo ya ujenzi wa mji huo wa serikali hapo Dodoma?

Au lengo la agizo la kutaka Waziri na wasaidi wake wahamie katika jengo hilo ambalo halijakamilika ni kutaka tu kuonyesha kuwa mheshimiwa ni mkali(mambo ya kisiasa)?

Na je,hii ndio sababu ya Waziri husika nae kupiga picha kuonyesha ametii agizo hilo(mambo ya kisiasa)?

Halafu ni kweli Waziri kahamia rasimi katika ile ofisi ya mabati tunayoiona mitandaoni?

Najiuliza maswali mengi sana kuhusu hili jambo na sipati majibu.
 
mwanadome

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
4,045
2,000
Jamaa anatumia nguvu nyingi sana kujitukuza wakati mwingine kwa vitu vya hovyo kabisaa.

Ni ujinga kuamini kua yeye hakua na taarifa za kukwama kwa ujenzi
 
Stanley Mitchell II

JF-Expert Member
Jul 2, 2018
708
1,000
Watakaojamba ni wale kajamba nani..

Huyo waziri hawezi kukaa humo ndani atajitafutia viji ziara vya hapa na pale vya kuzunguka nchi nzima mpaka jengo likikamilika anarudi ......
 
Mndali ndanyelakakomu

JF-Expert Member
Dec 14, 2016
12,799
2,000
Kuna wakati kujadili tunao amini ni wanyonyaji ni kupoteza muda

Hapo ni kuwa kila kitu kifanyike kama kilivyo pangwa

Kwenye hilo jengo kuna mtu anasubiriwa sadaka
 
KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,532
2,000
kwani wizara nyingine zilipojenga mapema walipewa ridhaa ya kujenga na rais?

agizo la kila wizara kuhamia dodoma limetolewa lini? unataka kuniambia pesa ndio ilikuwa kikwazo kwa tamisemi kukamilisha ujenzi? ghorofa ndio sababu ya kuchelewa kukamilisha ujenzi? Lazima ifike mahali tukiri kuwa kuna uzembe mkubwa katika utekelezaji wa majukumu . TBA imejenga hostel za magufuli UDSM flat zaidi ya 20 ndani ya mwaka mmoja, washindwa jengo la ofisi tu?

Wizara nyingine zimehamia dodoma mapema ila TAMISEMI walikuwa wanajaribu kuona tukichelewa kuhamia itakuwaje. siasa tuache pembeni kuna mambo mengi rais analaumiwa tu.
 
Mtaji wa CCM ni watu kama nyie unless unatumika kutetea vihoja!
 
K A B U R U

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
636
1,000
TAMISEMI walishahamia kikamilifu Dodoma kabla Kikwete na Magufuli hawajawa maraisi. Sina uhakika na kinachojengwa huko Ihumwa kama ndio Wizara itahamia na kuacha magorofa makubwa kuanzia Mkapa House mpaka TAMISEMI House pale katikati ya mji.
 
ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
4,438
2,000
TAMISEMI walishahamia kikamilifu Dodoma kabla Kikwete na Magufuli hawajawa maraisi. Sina uhakika na kinachojengwa huko Ihumwa kama ndio Wizara itahamia na kuacha magorofa makubwa kuanzia Mkapa House mpaka TAMISEMI House pale katikati ya mji.
Kama Tamisemi wana ofisi na walihamia Dom kitambo zile kiki za kuhamia kwenye jengo ambalo halijakamilika ni za nini? Kama ujenzi umekwama kwa sababu zao kulikuwa hakuna haja ya kili ni juwajibishana tuu
 
Top Bottom