Hivi ni sababu gani imfanyayo mwanamke kuwa Changudoa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni sababu gani imfanyayo mwanamke kuwa Changudoa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Akili Unazo!, Jul 20, 2009.

 1. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,818
  Likes Received: 2,530
  Trophy Points: 280
  Wakuu nimekuwa nikisikia neno hili changudoa na kujiuliza nini hasa chanzo cha hawa ndugu kujiingiza na tabia changu aifanyao?wakati mwingine nimekuwa nikijiuliza kuwa hii biashara ni wadada maskini au ambao hawajasoma au laah.Mpaka hivi ninavyoandika hii hoja sijapata jibu.
  ukienda casino,Jolly Club,maisha club,club ambience kwa ufupi tu japo zipo kumbi nyingi ambazo unaweza kutana na hao wadada achilia mbali kwa mama cheni na kinondoni makaburini,temeke na mahosetli mengi (hostel ya Buguruni,mabibo Hostel kwa ufupi tu.

  Wakuu nini hasa kinachopelekea dada yangu mkubwa kujiuza?ni kweli nikutafuta kipato au ni hulka?nikufuata mkumboa au ni sifa za kijinga?

  kama nikutafuta kipato mbona wenye kazi zao utawakuta wapo kwenye biashara hiyo?
  Na kama ni ukosefu wa elimu mbona walioko vyuoni ndo wanaongoza jahazi?
  reference hall three,mabibo hostel,mzumbe,St gasper Mwanza tumaini university?

  wakuu nisaidieni maake imekuwa kero na tabia hii ya ndugu zangu.
   
 2. GP

  GP JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  uchangudoa huwa uko tofauti kati ya msichana na msichana.
  ila asilimia kubwa ni ugumu wa maisha, hasa kwa wale waliokuja mjini kufanya kazi za ndani wakatimuliwa wakaenda kuwa mabaamedi mwisho wa siku wengine ndo wanajiuza.
  wengine ni hulka zao tu, wapo wengine ni wafanyakazi sehemu nzuri lakini kwa kua wamashazoea 'extreme' sasa nao utawakuta. tena wengine wake za watu kabisa wanajiuza.
   
 3. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Labda kwa sababu wananume wanawafuata kwa sababu uchangudoa hauwezi kuwa kamili kama jinsia ya pili itarefrain kuindulge kwenye hilo.
   
 4. GP

  GP JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  sio kweli kwamba 'soko' lipo juu ndio maana 'bidhaa' zinajitokeza!.
  wao wapo ndio maana wanafuatwa, wapo kujitafutia ridhiki, hawatoi huduma bure, hivyo ugumu wa maisha ndio tatizo (sio kwa wote, wengine ni kama fasheni tu au hobi)
   
 5. S

  Salehe Ndanda Member

  #5
  Jul 20, 2009
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa Tanzania hakuna kazi ya 'UCHANGUDOA' wote wanaofanya kazi hiyo ni WAARIFU, kama waarifu wengine.serikali ikiamua kuwakamata inawashitaki wanafugwa hakuna uharari wa kazi hiyo.
  kwa hiyo machagudoa wapo wa haina nyingi wamavyuoni wapo wanafanya wengine kwa shida hakizoea ikaingia kwenye damu inakuwa HULKA' hata acha hata kama ataolewa ataendelea tu, mwenginewe tamaa au kuiga, na mwinginewe HULKA au UGONJWA wa ngono, ujue kuna ugonjwa wa hiyo kitu kupona kwake uwe unabadirisha dizaini za MIKWAJU.

  Wasio soma SHIDA ,NJAA.

  Mashangudoa wa maofisini wale ni HULKA au kulipiza kisasi tabia ya mwanaume malaya naeanalipizia huko. lakini kuna wanaume malaya ambao wanawafanya wakezao kuwamachangudoa. wengine vigenge potofu au marafiki potofu matokeo wanakuingiza kwenye uchangudoa.

  KWA UFUPI HULKA,SHIDA,TAMAA NA NJAAA AWE NA ELIMU AU HANAELIMU
  NJAA KILA MTU INAMFIKA.KWA WANAWAKE
  KWA WANAUME NI HULKA NA TABIA YA MWANAUME, WANAUME WA NAMNA HII UWA HAWAACHI NG'O WANAMANENO YA KULAGHAI SANA.
  MBONENYAI.
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Tuseme kama ugumu wa maisha ukiisha nchini uchangudoa utakwisha?
   
 7. GP

  GP JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kaka,
  UGUMU WA MAISHA NI KIPIMO CHA AKILI!!
  so ugumu upo tofauti kati ya mtu na mtu, hata ulaya na marekani huko maisha ni magumu vile vile.
  hivyo wao baada ya maisha kuwa magumu akili zao zikawatuma wawe machangudoa!, sasa Mungu akibariki maisha yakawa mazuri, wapo watakaoacha na wapo ambao kwao ni hobi hawataacha.
   
 8. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,633
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  Sababu zinazosababisha Umalaya au uchangudoa ni:-

  -Umasikini au hali mbaya ya maisha.

  -Familia kufarakana

  -frustration au sijui mfadhaiko (ambapo labda mwanaume anamtaka msichana mzuri tu, na bahati nzuri mwanamke anapata mimba. Sasa mwanaume anamtoroka huyo msichana, sasa mwanamke hana kazi na anataka kumlea mwanae, hana msaada wa ndugu zake)

  - Malezi mabovu ya wazazi

  -Msichana kupenda anasa au vitu kuzidi uwezo wake. Unakuta msichana anataka mavazi mazuri kila mara, vyakula vizuri kila mara, vinywaji..

  -Tamaa tu basi

  -Kukosa kazi na hivyo kuwa huru sana

  Sasa baada ya kujua sababu, naomba tujadili jinsi ya kutatua au kupunguza hili tatizo
   
  Last edited: Jul 20, 2009
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Wengi wao ni tabia tu. Kisingizio chao ni kwamba hakuna njia nyingine ya kupata pesa. Ila sababu kubwa ya wanawake kuwa machangudoa ni kuwepo kwa wingi wa wanaume ambao wana taka huduma zao. So this all goes down to an individuals personal behavior.
   
 10. GP

  GP JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sikweli hata kidogo.
   
 11. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Jibu ni hili. Uchangudoa ni old profession ambayo iko toka mwanamke na mume walivyoumbwa. Ni profession kwa sababu wanaume wanaofaidika nao wapo tena kibao kwa sababu mbalimbali. Kwa hiyo ni kazi , Wala sii ugumu wa maisha ndio unaosababisha hayo, japo inaweza ikawa sababu moja wapo.

  Changudoa wengine wanafedha na hali nzuri tu za maisha lakini kwa kuwa wameamua kujichagulia kazi hiyo ambayo ni rahisi, ya starehe, na yenye fedha za hapo kwa hapo zisizosubiri mwisho wa mwezi then that is it.

  Kwa wanafunzi ,ambao kwa sasa ni wengi jibu liko wazi .Hii ni temporary employement hadi watakapomaliza vyuo na pengine waolewe. Hao wake za watu unaowaona hivi sasa wakiuza issue zao walikotokea huko huko maana walinogewa na sasa hawawezi kuacha . (Kinda visious circle) Wanasema mbuzi akishaonja magadi haachi tena .

  In short , it is a quick and convenient, way of making quick money for some women, which has been in practice since time immemorial.
   
  Last edited: Jul 21, 2009
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  MwanaF1,
  Nakuunga mkono kabisa kuwa ni tabia na tabia hii ni kwa wote mtoa na mtumia huduma. Kuna wasichana/wanawake ambao pamoja na kuwa wana kipato kizuri bado hutaka kujivinjari na watu mbalimbali na mwisho wa siku ni kupata ujira wa hali au mali. Ina maana kuwa, kuna madaraja ya uchangudoa. Watumia huduma nao huchangia kuendelea kwa tabia hii.Kuna wanaume huwapa vishawishi wanawake kama chambo cha kuwapata - hutumia fedha, ahadi mbalimbali kama kuwapa vyeo, nafasi na fursa mbalimbali.Mwanamke kama huyu chances are ataendelea kuwa na tabia ya mapenzi ya kubadilishana na vitu na siyo utu.Kwa wale wasichana na wanawake ambao hawakuwa na tabia hii, basi wanaweza kufikiri hii ni njia rahisi ya kufikia malengo.WANAUME WAKIWEZA KUACHA KUTUMIA WANAWAKE KAMA CHOMBO CHA STAREHE NAAMINI UCHANGUDOA UTAPUNGUA.KWAMBA UTAKWISHA KABISA HII HAIWEZEKANI KWA SABABU HALI HAIWEZI KURUHUSU - huu ni mjadala mwingine wa aina yake.
   
 13. Prince Alberto

  Prince Alberto Member

  #13
  Jul 21, 2009
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Binfsi nafikiri suala hili ni pana sana na sababu zake zinaweza kuwa nyingi sana,lakini iliyo kubwa kabisa ni umaskini wa kipato ambao unawakabili watu wengil akini hawa dada zetu wenyewe wanapenda short cut ya maisha ndio maana wanajiingiza katika hilo suala,maana kuna kamsemo kanakosema "uchumi unao lakini unaukalia' kwahiyo utaona hapa kwamba wameigeuza miili yao kuwa kama kitega uchumi, lakini kwa mwanaume aliyekamilika ni ngumu kufanya hivyo labda awe shoga, kitu kingine ni Tamaa kubwa walizokuwa nazo hawa dada zetu mfano humo vyuoni utakuta msichana akimuona mwenzake ana drive basi na yeye lazima atafute mtu au watu ambao atampatia usafiri au akiona mwenzie ana pafyumu nzuri,suruali nzuri au viatu vizuri au simu nzuri basi lazima na yeye atafute mtu au watu watakao mpa vitu kama hivyo, kwahiyo utaona kwamba hawa dada zetu wengi wao sio watu wa kulizika na hali zao za kawaida ndio maana wengi wanajiingiza katika mambon haya ya uchangudoa,vilevilke wengine wanakuwa ni 'SEXMANIA' sasa hawa wenyewe wanakuwa wanapenda zaidi kufanya sana ngono hata kama atakuwa anapewa pesa kidogo,au wengine wanakuwa na hata kazi nzuri lakini wanakuwa na hiyo tabia ambayo wanashindwa kujikontrol na kujikuta wanatumbukia katika hilo janga hatari, labda nitoe angalizo kidogo hapa unajua katika mfumo wa kibepari kawaida kila kitu kinabadilika na kuwa kama bidhaa ambayo inaweza kuuuzwa au kununuliwa,hivyo basi hii imepelekea hata wasichana kutumia miili yao kama bidhaa ili tu waweze kujipatia fedha fulani ambayo labda itawasaidia kupata mahitaji yao, sasa mfumo huu huwa unatawaliwa na vitu vikuu viwili DEMAND & SUPPLY, sasa kama mahitaji ya huduma ni makubwa hii ikiwa na maana ya kuwepo kwa wateja wengi baasi hata bidhaa zinakuwepo kwa wingi vilevile,kwahiyo suala hili pia ni la kimfumo zaidi kuliko kama tunavyofikiria.
   
 14. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Uchangu doa si umasikini wala sababu yeyote hapo juu bali ni mentality. If you can engage in uchangudoa na ukapata fedha certainly one could have sold maaandazi or mchicha and get a living. It is non sense. Uchangudoa uko hata huku merikani na unafanywa na watu ambao family backgrounds zao ni nzuri ajabu. Uchangudoa kimsingi hufanywa na watu irresponsible, wasiotaka kufanya kazi na kutaka vya ubwete. Watu hawa ni wenye tamaa ya mali pasipokujishughulisha. Watch out, evaluate and see outside the box. When the goin get tough ladies do not sell your body.
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Jul 21, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mi nikitia neno tu hapa nitarefusha mjadala labda aje mzee wa Jolly Yo Yo enzi hizo kabla hajamdondokea Mola.
   
 16. M

  Mzee Mwafrika Senior Member

  #16
  Jul 21, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Jamani naomba niulizie kuhusu hawa wamama wauza miili wajulikanao kama "WAHAYA".Hawa inakuwaje jamani?Maana wako very organized na wengi wao ni wa mama na heshima zao na hata wazee na wana camp zao kama huko Buguruni,Manzese nk.Jibu la Hawa litajibu maswali mengi sana!
   
 17. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni tabia ya mtu tu!
   
 18. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #18
  Jul 21, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Labda pia tujiulize, ni kwa nini wanaume wengi nao hupenda kutembea na mwanamke zaidi ya mmoja? Nadhani hii ni tabia zaidi kuliko ufukara, mtu ukishapenda kuonja onja basi ndio taabu yake hii. Bahati mbaya majina haya yote mabaya (malaya, machangudoa n.k) wamepewa dada zetu, sijui wanaume wao wamepewa yepi, kwani wao ndio wanaowabadilisha huyu na yule kila kukicha!
   
 19. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,818
  Likes Received: 2,530
  Trophy Points: 280
  Wanaitwa mafataki!hujawai sikia jina hilo?au kiwembe!!
   
 20. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #20
  Jul 21, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Soko lipo kutokana na ndoa nyingi kuwa za kujionyesha tu bali kuridhisha kimapenzi hakupo,upo hapo?
   
Loading...