Hivi ni nini mantiki ya Zanzibar kushiriki mashidano ya vilabu ya Afrika na si timu ya taifa?

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,140
9,323
Wadau hili suala huwa linanitatanisha sana!

Hivi inakuwaje Zanzibar inashiriki mashindano ya Vilabu ya CAF ilihali sio mwanachama, na ndiyo linapokuja suala la Timu ya Taifa inayotambuliwa ni ya Tanzania (URT)

Au kwenye vilabu Zanzibar hushiriki kama mwalikwa wa kudumu?
 
Na timu ya Taifa ya Zanzibar inatambuliwa pia na CECAFA. Japokuwa bado inatumia wimbo wa taifa wa Tanzania. Huu ni mkanganyiko mwingine.
 
Nasubiri majibu ilinishangaza kusikia Tz imevunja rekodi yakupeleka timu nne mashindano ya Caf nikabaki na swali kichwani timu za Zenji sio Tanzania tukajihesabia tumepeleka timu sita?
 
Wanashiriki CAF vilabu kwa sababu kwa sababu , kisheria Znz haitambuliki FIFA ,hivyo ikapelekea Tanzania tukawa na nafasi 2 tu za vilabu toka Tanzania katika mashindano ya CAF kwa maana ya Champions League na Shirikisho

Turudi nyuma miaka ya 90 Tanzania ikiwa ina nafasi mbili tu za ushiriki ,ilitumia mtindo wa LIGI YA MUUNGANO kupata wawakilishi wawili ,tunakumbuka ligi hii ilishirikisha timu 3 toka Bara na 3 toka Tanzania visiwani ( enzi za TFF na ZFF )

CAF na FIFA wakaleta mabadiliko ambapo bingwa ligi ya nchi mwanachama atacheza CCL na mshindi wa kombe la FA ( chama cha soka cha nchi itashiriki shirikisho )

Hapa ki kanuni znz ikawa nje ,ila CAF kwa busara na kutaka kula wakaipa 'favor' ZFA kushiriki vilabu vya znz michuano ya CAF ya vilabu tu hivyo katika vilabu CAF imeipa znz heshima hy

Tanzania bara tukabaki na TPL ambayo bingwa anacheza CCL na mshindi wa Azam cup FA anacheza shirikisho

Kwa utaratibu huu Tanzania bara na Zanzibar tulikuwa na timu 6 ktk michuano ya CAF mwaka huu 2019/2020

Nimejaribu vile najua ,naruhusu kusahihishwa

MTC | 101|
 
Hapa ki kanuni znz ikawa nje ,ila CAF kwa busara na kutaka kula wakaipa 'favor' ZFA kushiriki vilabu vya znz michuano ya CAF ya vilabu tu hivyo katika vilabu CAF imeipa znz heshima hy
Samahani,...busara na kutaka kula wakaipa favor ....heshima hiyo!? Una maanisha nini Mkuu!
 
Back
Top Bottom