Hivi ni nini hatma ya vijana wasio na ajira wenye umri wa miaka 26 na kuendelea

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,682
Hivi inakuwaje nafasi za kazi za siku hizi wanataka vijana wenye umri wa miaka 24 kushuka chini haswa serikalini.

Sasa katika hapa kuna watu wapo nyumbani karibia miala 4 wakisubili ajira na huo umri wa 25 wameshauvukaa.

Sasa ni nini hatma ya vijana wenye huu umri kuelekea miaka 30
 
wasomi wazembe saana.wanapenda walivyo anzisha wenzao
 
UMEONA MBALI SANA MKUU HALAFU ISITOSHE KUJIAJIRI MITAJI NAYO SHIDA HALAFU MZUNGUKO WA PESA KATIKA KUJIAJIRI UMEKUWA MGUMU SANA.SERIKALI ILITATUE BOMU HILI
 
Hivi inakuwaje nafasi za kazi za siku hizi wanataka vijana wenye umri wa miaka 24 kushuka chini haswa serikalini.

Sasa katika hapa kuna watu wapo nyumbani karibia miala 4 wakisubili ajira na huo umri wa 25 wameshauvukaa.

Sasa ni nini hatma ya vijana wenye huu umri kuelekea miaka 30
Tanzania inaardhi kubwa na nzuri kwaajili ya kilimo!

Nendeni shamba mlime mazao ya chakula mtuletee jijini!
 
Katika maisha mkuu kila binadamu ana ndoto zake ambazo amejiwekea .

Haiwezekani mtu ndoto yako ukiwa mtoto ilikuwa uwe PILOT leo hii ukipelekwa kwenye kilimo ni sawa kujidhalilisha
 
utakufa masikini kijana!
badili gia angani, anza kilimo pia ndoto yako ya kuwa mwalimu haitakufikisha popote kimaisha zaidi ya kuona wenzio wakipga hatua kimaisha

Wachana na ualimu!
 
Daah ndio maana vijana wengine wanakimbilia kufanya siasa tu...Wengine huenda mbali hata kufanya biashara haramu
 
Ukiona anaesema ukalime akat ukuandaliwa kulima basii jua ajui machungu ya kusoma na atakua kma sio aliishia drasa la saba au form four.... Basi hta cm anayotmiaa hata JF app amesaidiwa kudownload.. Huna lolote.
 
Hivi inakuwaje nafasi za kazi za siku hizi wanataka vijana wenye umri wa miaka 24 kushuka chini haswa serikalini.

Sasa katika hapa kuna watu wapo nyumbani karibia miala 4 wakisubili ajira na huo umri wa 25 wameshauvukaa.

Sasa ni nini hatma ya vijana wenye huu umri kuelekea miaka 30
Nani aliyekudanganya kuwa ajira za serikalini umri wa mwisho ni 24yrs?

Umri wa mwisho kuajiriwa serikalini ni miaka 45
 
Hili ni pigo na changamoto, mimi ni gvt employee ila nilitaka kubadili taasisi nilishindwa kuingia mahali fulani kisa umri.
Wengine hushauri wenzao wakajiari bila kujua kuwa hata elimu waliyonayo wameipata kwa mkopo au ufadhili. Kabla hujatoa ushauri kwa mtu yetote katika maisha ni vyema ufikiri mambo haya;
A: Huyu ninayetaka kumshauri ni nani na yuko katika status gani ya maisha?
B: Ukijua status yake basi vaa uhusika wake na chukua utu changanya.
Haya mambo ukiyatafakari lazima utakuwa mwanadamu halisi na utaacha kuropoka kama mwehu.
Wewe umemaliza shule/chuo umefunguliwa kibanda cha tigopesa na dada au shemeji yako unaleta jeuri humu ndani.
Biashara au kilimo hivi vyote pia vina challenges nyingi. Mimi ni mfanyabiashara pia licha ya kwamba ni mwajiriwa.
 
Vijana wengi tuna hofu na maisha ndo maana hata mtu aliye ajiliwa anaona
kama akiacha kazi anayolipwa kiduchu na "mkoloni mweusi" basi ndo atakuwa
kapoteza kila kitu maishani.

Ila hakika kujiajili ndo ukombozi wa kijana wa leo.
 
Back
Top Bottom