Hivi ni nini faida ya milango ya kutembea yenyewe kwenye majengo ya umma?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Nimesikia bwana mkubwa akipiga panga bajeti ya kuweka milango ya kutembea yenyewe (automatic door) kwenye majengo ya watu wengi endapo mtu anaukaribia.

Ameelekeza kuwekwa milango ya manual - kusukumwa kwa mikono.

Swali hiyo teknolojia ya 'automatic door' ina faida gani na zaidi ya ile ya manual?

Kwa haraka haraka kwa kufikiri kwangu ni kuwa automatic door unaepusha, mosi, magonjwa ya kugusana, mfano, ebola.

Pili, unarahisisha watu kupita kwa urahisi zaidi tena kwa kupishana pia. Tatu, hauna rabsha ya kusaidiana kushika mlango wakati ukipita.

Nne, upunguza kuingia kwa wadudu kama nzi au kupoteza ubaridi wa kiyoyozi kwani watu sio wakamilifu, hivyo kusahau kufunga ni obvious

Tano, kuna uimara fulani kwani bawaba za manual door uchoka mapema na mlango unaegama (tilt) na kuleta kelele na pia kukwangua tiles/ sakafu.

Mwisho, ni milango ya karne hii, hivyo ni budi kutumika na kupendezesha jengo.

Points za bwana mkubwa kwenye suala ili zinanifanya nianze 'to beninise' or 'to saananenise' about the University of London.

 
Halafu muda mwingine sijui tunakuwaje watu. Huyu jamaa si ndio aliwahi kunaswa kwenye kipande cha video akisema tukimpa urais tutalimia meno?

Alisikika kwa mbali mlalahoi mmoja akihoji juu ya hoja ile
 
Mlimpa nchi mchunga ng'ombe mnategenea nin

Ushamba mzigo mkubwa sana, anatulazimisha tuone hio milango haina maana, bila kujua kuwa just advancement of technology so modern building must have such kind of door
Umemaliza kila kitu hapo mkuu, ni ushamba tu kudhani kila kitu advanced ni luxurious. Narudia tena USHAMBA NI MZIGO MKUBWA SANAAA.
 
Ushamba mzigo mkubwa sana, anatulazimisha tuone hio milango haina maana, bila kujua kuwa just advancement of technology so modern building must have such kind of door
Madirisha ya aluminum ni anasa nayo....
shubamiiit!!
 
Mwanamayu,
Ili kuepukana na maambukizo ya ebola watu wanapeana VIWIKO kuna maambukizo ya magonjwa ya macho na Dodoma ndiyo kinara hakika ni jambo la hekima Mkuu asiwabeze wasaidizi wake awaache waboreshe miundombinu kwa heshima yake mwenyewe.
 
JPM ANA HAKI YA KUTOA POVU
MBONA MIMI NAUZA KWA LAKI 7 KAMA HII 👇 👇
HALAFU WAO WANAMWAMBIA MKUU ETI BILION 8 ZIPO NGAPI HIZO CCTV

CCTV.png
 
Kwanini yeye hatumii passo au bajaji? Kwanini wabunge na mawaziri wanapewa magari mapya ya kifahari badala ya kutumia magari ya bei rahisi?

Kuwa kiongozi wa nchi sio lazima kujua kila kitu.
 
Hizi Headquarter zote zihamishwe Dodoma kutatokea UFISADI mwingi sana kwenye ujenzi labda majengo yajengwe na jeshi na takukuru wawe macho sana :rolleyes:

Take note:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom