Hivi ni nchi ngapi ktk sayari hii ambazo JK hajawahi kutembelea?

segwanga

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
2,789
729
Katika bajeti ya mwaka huu serikali ina mpango wa kupunguza hela kwa ajili ya ziara. Cha kushangaza kila wiki JK ana talii nchi za nje.Wiki iliyopita alikuwa Africa kusini kuhudhuria mazishi ya mwanahakati wa kupigania uhuru na leo hii yuko uswis kuhudhuria mkutano wa ILO. Hivi JK amebakiza nchi ngapi ktk dunia kuzitembea?
 
Usiombe wakusikie.
Watakuambia kupunguza ziara za rais tayari lipo kwenye mpango wa maendeleo.
 
JK ni raisi wa Kimatatifa nchi zoote katembelea labda uulize ni mikoa gani hajatembelea toka amepata uraisi!?
utapata majibu kibao.
 
Katika bajeti ya mwaka huu serikali ina mpango wa kupunguza hela kwa ajili ya ziara. Cha kushangaza kila wiki JK ana talii nchi za nje.Wiki iliyopita alikuwa Africa kusini kuhudhuria mazishi ya mwanahakati wa kupigania uhuru na leo hii yuko uswis kuhudhuria mkutano wa ILO. Hivi JK amebakiza nchi ngapi ktk dunia kuzitembea?

ninachojua ni kwamba Rais hakwenda kuhudhuria mazishi ya mama sisulu pekee ila alihudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa EAC,SADC na COMESA juu ya uwezekano wa kuunganisha jumuiya hizi na kutengeneza moja kubwa.kwa akili zako nyingi ulitaraji akae nyumbani wakati kuna mkutano wenye umuhimu kama huu?
 
JK ni raisi wa Kimatatifa nchi zoote katembelea labda uulize ni mikoa gani hajatembelea toka amepata uraisi!? utapata majibu kibao.
JK ataingia kwenye Guines book,tangu awe waziri wa mambo ya nje hadi kuwa rais atakuwa amebakiza nchi chache sana kuzitali ambazo atazitembelea ktk kipindi cha miaka iliyobaki (nafikiri hvyo)
 
JK ni raisi wa Kimatatifa nchi zoote katembelea labda uulize ni mikoa gani
hajatembelea toka amepata uraisi!? utapata majibu kibao.

Atembelee mikoa achekwe! Mambo yote ni kwenda kusafisha macho majuu, ili apate cha kusimulia
we unadhani akitembelea Tabora kwa mafano, atamsimulia nani kwani kila mtu anaweza kwenda
huko bila hata kuulizwa visa.
 
hilo eti umeambiwa usilizungumzie.strictly prohibited. lakini mimi silaumu safari za kikwete.nalaumu waliopanga foleni kuweka alama ya v kwa ajili yake.
 
labda kijiji chetu kinachoitwa BAGHAI kipo wilayani LUSHOTO KATA YA MLALO, HUKO NDO NINA HAKIKA HATA KUKIJUA HAKIJUI.
 
ninachojua ni kwamba Rais hakwenda kuhudhuria mazishi ya mama sisulu pekee ila alihudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa EAC,SADC na COMESA juu ya uwezekano wa kuunganisha jumuiya hizi na kutengeneza moja kubwa.kwa akili zako nyingi ulitaraji akae nyumbani wakati kuna mkutano wenye umuhimu kama huu?
Sawa mkuu broken heart,inaonekana una akili sana mkuu nakupongeza kwa hilo! naomba unisaidie mimi na watanzania wengine tunaolalamikia ziara za rais dr JK.Hata serikali wamesikia kilio cha watanzania tusiokuwa na akil kama mimi,naomba mkuu broken heart utuambie ziara ambazo waziri mkulo alisema zitapunguzwa ni zipi au Dr JK ziara zake haziguswi la tamko hilo.Naelewa kabisa JK huwa anasafiri kwa manufaa ya uma,lakn kama safari zinapokuwa na gharama kubwa basi hazina tija kwa taifa
 
JK ni raisi wa Kimatatifa nchi zoote katembelea labda uulize ni mikoa gani hajatembelea toka amepata uraisi!? utapata majibu kibao.
JK ataingia kwenye Guines book,tangu awe waziri wa mambo ya nje hadi kuwa rais atakuwa amebakiza nchi chache sana kuzitali ambazo atazitembelea ktk kipindi cha miaka iliyobaki (nafikiri hvyo)
 
Kwa mjibu wa takwimu zangu nilizozifanya tangu sharobalo/loveboy mzaliwa wa Musoga pale bagiamoyo, tangu aingie magogoni mwaka 2005, hii safari ya uswisi jana ametimiza safari ya nje ya 305. Hii ni record ya kipekee na ndio kumbukumbu muhimu atakayotuachia watz!!
 
asante mkuu kwa data zako,nataka nijaribu kulinganisha na nchi nyingine za africa kama marais wao wanafanya ziara kama za Jembe K
 
central Africa Republic, au nakosea!? Lakini unajua anajiandaa na ujasiriamali ambao ni mgumu hivyo inatakiwa exposure!
 
Back
Top Bottom