mkwawa masawe
JF-Expert Member
- Nov 19, 2018
- 225
- 345
Tunamuomba RAIS Mama Samia na Serikali yetu sikivu wasikie kilio Chetu Sisi wastaafu tuliostaafu wakati mfumo wa mishahara Serikalini Ikiwa kidogo.Maana pension inalipwa kulingana na size ya mshahara WAKO wakati unastaafu.Mfano Mimi nilikuwa Officer wa Serikali Mwenye first degree niliyekuwa nimefanya kazi kwa zaidi ya miaka 15 baada ya ku-graduate.Wakati nastaafu,mshahara wangu ulikuwa sh 25,000 kwa mwezi(kwa wakati HUO mshahara huu ulikuwa unanitosha mahitaji muhimu kwa mwezi(ambayo siyo ya anasa).Pension yangu kwa mwezi kwa Sasa nalipwa sh 100,000.Ni kidogo Sana jamani kwa Khali ya MAISHA ilivyo kwa Sasa.Equivalent officer (kwa cheo nilichostaafu nacho Mimi) aliyestaafu miaka ya karibuni analipwa pension ya shs 1,000,000 kwa mwezi.Tunaomba Serikali ituongezee angalao pension yetu Sisi tuliostaafu zamani pension angalao tulipwe sh 300,000 kwa mwezi badala ya hii sh 100,000 tunayolipwa KILA mwezi kwa Sasa.