Hivi ni nani anawadanganya watanzania kuwa lockdown haifanyi kazi? Hata kama tumeigomea, tuache kupotoshana!

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,989
22,521
Naona kumekuwepo na hali ya upotoshaji nchini kuwa hatua za lockdown hazina manufaa! Hili naona kama ni upotoshaji ambao unasababishwa na ukweli kwamba viongozi wengi wameingiza siasa kwenye vita dhidi ya corona na matokeo yake ndo haya ya upotoshaji pamoja na mambo mengine.

Mifano iko mingi, lakini kuna mfano nilioamuwa kuutumia kujenga hoja yangu. Mfano huu ni wa gavana wa Ohio kule marekani, anayeitwa Mike Dewine! Huyu alichukuwa hatua zote kabla ya Trump! Pamoja na kwamba Trump anaogopeka na viongozi wengi ndani ya chama chake cha republican, mfano maseneta na magavana, huwa wana wasiwasi wa kupingana naye kwasababu ya umaarufu alio nao ndani ya chama cha Tembo ama Republicans!

Sasa huyu alichukuwa hatua za lockdown toka mwanzo kabisa wakati Trump akiwa analeta utani na gonjwa hilo! Matokeo yake, jimbo lake linafanya vizuri sana na yeye amekuwa maarufu siyo tu kule Ohio, bali marekani nzima! Alikuwa na guts za kufanya maamuzi sahihi ya kulinda raia wake kuliko rais wa nchi! Na wananchi wanasema hatua hizo alitakiwa azichukuwe Trump mwenyewe, na pengine mikusanyiko iliyokuwa ikiendelea kwenye majimbo mengine mfano New York, New Orleans na kwingineko ambako michezo iliendelea kama kawaida na mikusanyiko mingine kama makanisani nk, ambapo matokeo yake ndo haya tunayoyaona wanakufa kwa kasi na maambukizi ambayo yalikuwa tayari yametapakaa.

Jimbo lake lina maambukizi machache na vifo vichache sana, na wameshaanza kufungua taratibu taratibu. Pia jimboni kwake alifanya mkakati siyo wa total lockdown, hiyo ni baadhi tu ya sehemu. Wale wanaojitetea kuwa lockdown ni mbaya, wanawaongopea wananchi kwa manufaa yao binafsi, most likely uchaguzi. Ni bora waseme lockdown siyo njia muafaka kwasababu ya mfumo wetu wa uchumi ulivyo na maisha ya wananchi wake, au pia kwamba wamechelewa kwasababu tuliendelea kupokea wageni wote hata kutoka China! Lakini haina maana kuwa partial lockdowns hazifai na wala hazikufaa! Na lockdowns kwenye maeneo korofi ni za muhimu!

Lakini pia tulipuuza tokea mwanzo na kuanza kusema wapinzani wanataka wananchi wafe na njaa! Hii ni propaganda ambayo matokeo yake si mazuri kwenye jamii inayokabiliana na janga hatari linalochukuwa maisha ya watu kila siku na pengine kila saa duniani.

Bila kupoteza muda, naweka hiki kipande hapo chini chenye kusapoti ninachokisema, pia link kama ukitaka kusoma habari yote na kujiridhisha wewe mwenyewe kuwa niyasemayo ni kweli.

Mike Dewine gavana wa Ohio, alipata umaarufu hata kumzidi Trump ambaye naye akaanzisha utaratibu wa kuongea na waandishi wa habari kila siku. Jambo ambalo Dewine alikuwa akilifanya jimboni kwake kila siku saa nane mchana, na wakati huo wana Ohio wanakuwa kwenye luninga zao wakimsikiliza. Ndiyo wakaanzisha usemi wa “it’s 2’oclock somewhere...wine with mr Dewine”, ambapo wakati wa lunch wanapata wine wakimsikiliza Dewine. Wala hawa kuwa na habari na Trump!

A Republican, he took early and bold actions to lock down his state, even as the head of his party, President Trump, dismissed the threat of the pandemic.

Mr. DeWine’s decisiveness — closing schools before any governor in the country, postponing the state’s March 17 primary election to protect voters — sent his popularity soaring. The folksy governor, previously best known for an annual ice cream social at his rural home, became something of a cult figure on social media. Ohioans tuned into his five-day-a-week briefings to celebrate “Wine With DeWine,” a ritual whose motto is “It’s 2 o’clock somewhere.”

Ohio’s G.O.P. Governor Splits From Trump, and Rises in Popularity

Kwahiyo ndugu watanzania wenzangu, kabla ya kufanya upotoshaji, jiridhishe kwa kautafiti kadogo tu ili uweze kuwa huru kifikra! kama ikifikia mahali unamkabidhi mtu mwingine jukumu la kufikiria kwa niaba yako, ujuwe kuna shida kubwa sana kwa upande wako! Kusema lockdown haisaidii, ni sawa pia na kusema “to hell with social distancing”. Kwasababu huwezi kuwaambia watu wafuate masharti kwa ugonjwa ambao siyo hatari kabisa kwa jinsi unavyochukuliwa, kutokana na hatua za viongozi wetu, pamoja na matam

Siyo sahihi kusema lockdown haisaidii kwasababu zenu za kisiasa! Kwanza ingekuwa ni kwetu, huyo Dewine angekiona cha mtemakuni!

Lakini kwasababu ya kiasi cha demokrasia na mfumo wao wa uongozi, Dewine aliweza kuchukuwa maamuzi muhimu kwenye jimbo lake kinyume na rais wa nchi! Na ameonekana kwamba alikuwa sahihi na kiongozi shupavu!

Nyota yake inang’ara! Trump hawezi tena kusema kuwa lockdown haisaidii! Na kwetu Tanzania siyo sahihi kusema hivyo, semeni tu hamkuchagua lockdowns kwasababu mtakufa njaa, ama pia mlichelewa kuchukuwa hatua za kufunga mipaka!

Mag3 Nguruvi3 JokaKuu Kalamu1 imhotep Detective J
 
The poll, by Baldwin Wallace University, also showed overwhelming support for the governor. Eighty-five percent of respondents approved of his handling of the coronavirus, 89 percent said they trusted him as a source of information about the outbreak, and three out of four said he was doing a better job than Mr. Trump.

Mr. DeWine’s data-driven response to the outbreak has won the support of top Democrats in the state. Many have praised his management style — honed over a lifetime of serving in all levels of government — as a departure from that of the president, who quixotically says to social distance one day and to ignore it the next.
 
Magufuli anasema Hofu ndio inauwa sana kuliko corona kwa hiyo Lockdown haitasaidia

Swali langu kwenye cheti cha kifo je sababu inaandikwa "Hofu" ?
Hiyo ni sababu ya uongo. Kwenye vitu haangalii watu. Hii ni fact. Kwahiyo tatizo hili limekuja tu kuukuza udhaifu wake zaidi.

Hata Trump anapiga kelele maana mahoteli yake yanasafaa!
 
Kuna mifano pia ya nchi ambazo hazijafanya ,,lockdown” na ziko vizuri na kufanikiwa zaidi klk zile zilizofanya, mfano Taiwan ingawaje ipo karibu kabisa na China na ni moja kati ya nchi za kwanza kabisa kushambuliwa lkn haikufanya ,,lockdown” na sasa hivi Taiwan ni success story kwenye kupambana na virusi vya corona.

Hata Sweden haikufanya lockdown na bado wametoka vizuri klk nchi zilizofanya lockdown kama Italia au Uingereza, isitoshe swala hapa siyo kwamba lockdown inasaidia au la, bali swala ni kwamba nchi nyingi hata zilizoendelea haziwezi kumudu lockdown.

Na watu wengi zaidi watakufa kutokana na madhara ya lockdown kuliko corona, wengi wamepoteza kazi, wamepoteza Health insurance, hata Afrika kwetu wanaokufa na njaa ni wengi kuliko wa corona, hiyo ndiyo argument, kwamba lockdown inaumiza zaidi kuliko kuponya, ...
 
Kwa hiyo unashauri na Tanzania tuweke LOCKDOWN?
Dar ilitakiwa lockdown, pia kuna partial lockdowns ambapo siyo wote wanazuiliwa, inaweza kuwa ni sehemu ama eneo fulani, ama pia watu Fulani kutokana na maambukizi.

Kinachofanyika sasahivi Tanzania ni kwamba hakuna hatua zozote ambazo zinapigiwa kampeni na serikali, zaidi ya kauli ambazo zinasababisha wananchi kuona ni kawaida tu na kuacha kuchukuwa hatua!

Sasa hadi mipaka tufungiwe ndo unasema lockdown ni mbaya?
 
Dar ilitakiwa lockdown, pia kuna partial lockdowns ambapo siyo wote wanazuiliwa, inaweza kuwa ni sehemu ama eneo fulani, ama pia watu Fulani kutokana na maambukizi.

Kinachofanyika sasahivi Tanzania ni kwamba hakuna hatua zozote ambazo zinapiggies kampeni na serikali, zaidi ya kauli ambazo zinasababisha wananchi kuona ni kawaida tu na kuacha kuchukuwa hatua!

Sasa hadi mipaka tufungiwe ndo unasema lockdown ni mbaya?
Too late now.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom