Jana tukiwa na furaha na bashasha za kusubilia KIFAA chetu brand new AIR BUS 220-300, Mh mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam ndugu Paul makonda alipewa nafasi ya kuwakaribisha na kuwatambulisha wananchi wa mkoa wake maana yeye ndiye alikuwa mwenyeji wa hafla hiyo.
Katika hotuba yake fupi ya ukaribisho alimuahidi Mh Rais kuwa wanampango mkakati wa kujifungia ndani yeye pamoja na watendaji wake ili kufanyia kazi suala la ukusanyaji wa kodi. Na alienda mbali zaidi kwa kumhakikishia Mh Rais kuwa jiji la Dar Es Salaam litakuwa namba moja kwa ukusanyaji wa kodi.
Nilisikiliza na baadae nikaanza kujiuliza na kutopata majibu mimi mwenyewe,
kuwa Mh Makonda, asimamie ukusanyaji wa ushuru na mpka jiji la Dar es Salaam liwe kinara wa ukusanyaji mapato wakati sio miezi mingi ilopita Mh Makonda alikuwa na mgogoro na TRA pamoja na waziri wa fedha juu ya kutolkulipa kodi.
Huyu alietaka asilipe kodi leo anakuwa kinara wa ukusanyaji wa kodi?
Au ni watu gani ambao ni walengwa wa kulipa kodi ili jiji letu liwe kinara wa ukusanyaji wa mapato/kodi?