Hivi ni nani anakagua ofisi ya CAG? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni nani anakagua ofisi ya CAG?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Amavubi, Apr 30, 2012.

 1. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,445
  Likes Received: 4,729
  Trophy Points: 280
  Pamoja na mazuri ninayohisi yamefanywa na CAG, najiuliza ni nani anayemkagua katika utendaji wake?
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  CAG anakaguliwa na wakaguzi wenzake wa nje. Katika taaluma ya kikaguzi kuna kitu inaitwa peer review ama Engagement Quality Review ambapo kunakuwa na wakaguzi wenzi ambao hukagua utendaji wa wakaguzi wengine ili kuangalia kama wanatenda kazi zao kulingana na weledi. Ila kitu nilichogundua ni kwamba hii taaluma imejilinda sana hivyo hata hizo report huwa si za hadhara.
   
 3. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo nalo neno,kwani mwoshwa lazima naye aoshwe,ngoja wadau wachangie tuone
   
 4. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,445
  Likes Received: 4,729
  Trophy Points: 280
  siasa ni game hovyo sana inawezekana tunapigwa trick yA MBINU YA KUWAONDOA WATU KUPITIA KITU
   
 5. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,445
  Likes Received: 4,729
  Trophy Points: 280
  Maana yake ni wao kwa wao....nataka kujua anatumia kiasi gani mpaka anahitimisha kazi yake na kuna usafi kiasi gani katika matumizi hayo
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  niliwah kujiuliza hili swali
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  nakuelewa,AU NDO MANA J.K ALISEMA RIPOTI YA CAG IENF BUNGENI?
   
 8. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280


  Kwani vipi, amekuteda?
   
 9. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,445
  Likes Received: 4,729
  Trophy Points: 280
  CAG i wangu ni wa watz, una maana kin Mkulo etc amewatenda?? jenga hoja mkuu usiharibu utamu, afu soma hapa chini
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu nilijua tu kwamba mwisho wa siku ni matumizi ya utendaji kazi. Kusema kweli jinsi ninavyojua hawa wanaofanya ukaguzi kwa wakaguzi huwa wanaangalia budget na matumizi ya CAG (sijui kama CAG wa TZ) amewahi kufanyiwa ukaguzi huu. Lakini lengo lao kuu huwa ni kuangalia kama CAG anakagua kulingana na standards walizojiwekea. Huenda kwa CAG nako kuna madudu.
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu Report ya CAG kwenda bungeni ni matakwa ya Kikatiba. Imekuwa ikienda bungeni miaka yote. Tatizo ni kwamba miaka ya nyuma ilikuwa report zinachelewa sana. Kwa mfano ungweza kukuta report ya 2007/2008 inasomwa bungeni mwaka 2012 kwa hiyo zikawa zinakosa impact. Ila miaka ya hivi karibuni ukaguzi umekuwa ukifanywa kwa wakati na repott kwenda bado ya motomoto kama hii ya juzi.
   
 12. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Pole kama report yake imekuumbua ndio maisha bwana acha ufisadi.
   
 13. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Naona wote mnajikanyaga na kuna baadhi yetu hawajaelewa hoja ya mleta hoja. Someni[SUP]1 [/SUP]hapa:-  [SUP]1[/SUP]
  http://www.nao.go.tz/files/PUBLIC%20AUDIT%20ACT.pdf
   
 14. c

  collezione JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ngoja tuulize. Nani anamkagua jaji??
  Jaji akishatoa hukumu, nani anatoa hukumu ya kumuhukumu Jaji aliyetoa hukumu ya kwanza.

  Ukishatoa majibu hapa. Utajijibu swali lako la kwanza.
   
 15. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,710
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Ana report kwa Goverment Audit Committee sijui ipo? Au Bunge Audit Commitee na anateuliwa nayo, Sijui ipo kwenye katiba, anateuliwa na GAC au BAU sijui analipwa na nani mshahara-na nani anampangia mshahara-widhara ya fedha-''Wadau wa katiba hii ni changamoto""
   
 16. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii nchi bwana. Juzi kati wakati wa issue ya Jairo, huyu CAG alionekana mbaya sana, lakini leo anaonekana wa maana sana!
   
 17. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CAG inaonekana kakata mirija za baadhi ya watu hapa,zengwe limeanza kuandaliwa kuwa nae ni fisadi,kweli ufisadi ukikuingia huwezi acha.
   
 18. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,124
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Mleta mada,

  Ukiachilia mbali wanaokubeza kwa mada yako inabidi nikupongeze kwani umeleta kitu kikubwa kilichojificha kutokana na wengi wetu nikiwemo mimi tuko wavivu wa kusoma.

  Katiba yetu iko wazi kabisa kuhusu CAG. Ibara ya 143 (i) inasema: {Kutakuwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano.}

  Hapo hakuna matatizo. Jibu la swali lako linaweza kupatikana kwenye ibara ya 143(6) isemayo hivi: {Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2), (3) na (4) ya ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hatalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu mwingine yeyote au idara yoyote ya Serikali, lakini maelezo hayo ya ibara hii ndogo hayataizuia Mahakama nayo kutumia madaraka yake kwa ajili ya kuchunguza kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ametekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii au sivyo.}

  Hapo kwenye blue ni kwamba CAG si mwisho he/she is subject to court. Hivyo, CAG anaweza kushitakiwa mahakamani kama ameboronga.

  Kikubwa kingine ambacho hukukileta lakini nakiona potential kwenye post yako ni kwenye ibara ya 143(4) isemayo hivi: { Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atawasilisha kwa Rais kila taarifa atakayotoa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2) ya ibara hii. Baada ya kupokea taarifa hiyo Rais atawaagiza watu anaohusika wawasilishe taarifa hiyo kwenye kikao cha kwanza cha Bunge kitakachofanyika baada ya Rais kupokea taarifa hiyo na itabidi iwasilishwe katika kikao hicho kabla ya kupita siku saba tangu siku ile kilipoanza kikao hicho. Iwapo Rais hatachukua hatua za kuwasilisha taarifa hiyo kwa Spika wa Bunge (au Naibu wa Spika ikiwa kiti cha Spika ki wazi wakati huo au ikiwa kwa sababu yoyote Spika hawezi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania}

  Hapa ndipo penye sakata ambalo inawezekana hujui lakini umelianzisha. Maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Rais ndiye anayepewa report ya madudu aliyogundua CAG wakati wa ukaguzi wake. Mara tu Rais anapoipata report hiyo anaipeleka kopi Bungeni.

  Hivyo, mtiririko wa safari ya report ni kwamba inaanza kwa CAG, inaenda kwa Rais, kisha inaenda Bungeni. Hakuna mahala panapoonyesha kuwa Makamu wa Rais, au Waziri Mkuu au Waziri yoyote anapitia mlolongo wa kuipokea au kuigusa report ya CAG.

  Kumbe, Waziri Mkuu na mawaziri wenzake, wanashtukia kuyasoma madudu yale report inaposomwa Bungeni. Hivyo, kwa utaratibu huu mtu pekee anayejua madudu ya report kabla haijaenda Bungeni ni Rais na CAG tu.

  Kwa utaratibu huu, huwezi kusema Waziri Mkuu hakumshauri Rais kuhusu madudu yaliyomo kwenye report ya CAG wakati Waziri Mkuu hakupata nafasi ya kuiona kwani utaratibu uko wazi kabisa yeye anaijua report inaposomwa Bungeni.

  Nakubali kwamba Pinda anaweza kuwa aliiona mapema, lakini kikatiba anapoiona Pinda ni kwamba ime-leak kwani hakutakiwa hadi aisikie ikisomwa Bungeni.

  Hivyo, kikatiba huwezi kusema Pinda anapaswa kuwajibika kwa lolote lililotajwa na CAG. Eti hakumshauri Rais. Angemshauri vipi kwa jambo ambalo katiba yenyewe inasema kuwa hakutakiwa kulijua kabla report haijasomwa Bungeni na kuisikia kama tunavyoisikia sisi.

  Hivyo, aliyeshindwa kuwawajibisha mawaziri kabla hata repirt haijaenda Bungeni ni Rais mwenye kikatiba na tuache ngonjera zingine za kisiasa ambazo hazitasaidia kuubadilisha ukweli huu wa kikatiba.

  Someni ibara mbili za katiba yaani 143 na 144 ambapo ukweli ninaosema umeanikwa wazi hata primary school pupil anaweza kuusoma.

  Namalizia tena, hongera mleta mada, na kama magazeti yatapitia thread hii, hii ni habari mpya ya kubadilisha upepa wa suala zima ambalo sasa eti linachukua sura ya kisiasa wakati ni suala la kikatiba.
   
 19. hirorobert

  hirorobert Member

  #19
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nadhani ulikuwa unahitaji jibu hili-ofisi yake huwa inakaguliwa na PWC.
   
 20. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,445
  Likes Received: 4,729
  Trophy Points: 280
  Ni kweli imeniumbua maana imfichua uchafu wa mbunge wangu niliye muamini na kumpa kura yangu
   
Loading...