Hivi ni mwanasiasa gani kwa sasa mwenye mvuto na ushawishi zaidi kwa jamii ambaye anastahili kuwa alama ya siasa za Tanzania?

1- JK Nyerere

2- JK Kikwete ( Mzalendo, anapendwa naturally tu na wapinzsni, watanzania hata ndani ya CCM kama ilivyo kwa Lowassa )

3- Warioba Sinde ( Mzalendo wa nchi )

4- Dk Slaa ( huyu katumikishwa na Mbowe, kiasi kwamba hivi karibu alikuwa kana kachanganyikiwa baada ya kusalitiwa )

5- Freeman Mbowe ( Huyu biashara ya siasa anaijua vizuri )

6- Edward Lowassa ( anapendwa ndani ya CCM na watanzania, alikuwa akichukiwa na wapinzani kabla ya 2015 )

7- Zitto Kabwe ( huyu ni mgumu sana kumfanya msukule, anachoona mwenyewe ni sahihi kufanya, anatekeleza bila kujali wengine wataonaje )

Mkuu unaelewa ulichojibu?
 
Mpaka sasa siasa za Tanzania ziko chini ya kivuli cha Mwalimu Nyerere. Nchini kwetu unaruhusiwa kumkashifu na kumkejeli Mungu, lakini huruhusiwi kabisa kumkashifu wala kumsema vibaya Mwalimu Nyerere. Kila kiongozi/mwanasiasa wa Tanzania anayeibukia jamii humpima kwa kumvalisha viatu vya Nyerere na kama havitamtosha basi ataonekana ana walakini fulani hata kama ni mtu mzuri.

Tanzania ina miaka 60, mpaka sasa kumekuwa na vizazi vitatu. Sehemu kubwa ya maisha ya vizazi hivi yamejengwa kwenye msingi wa Falsafa za mwaka 1967 (Ujamaa na Kujitegemea): Aidha kwa mazuri yake au mabaya yake. Hivyo nadhani unavyozungumzia sura ya siasa za Tanzania tokea mwaka 1967 hadi miaka mingine ijayo, zimwi la Nyerere halina mpinzani.

Nyerere's Ghost will haunt this state for many generations to come......
Either for better or worse....
 
Kama mada inavyojieleza hapo juu, kila nchi kwa nyakati tofauti hujaaliwa kuwa na mwanasiasa au wanasiasa wenye kujaaliwa vipaji vikubwa vya uongozi kiasi cha kugeuka kua kichocheo na hamasa kubwa kwa wanasiasa wanaoibukia na hata wasio wanasiasa. Ndipo nikajiuliza tunao wanasiasa wa namna hiyo kama nchi kwa sasa?
Tunapojadili na kufikiri hili, tuzingatie vigezo vipi?.

1. MOSI, kwa maoni yangu, kwenye kutazama na kupiga kura kwenye hili, tuiondoe CCM kabisa maana huko hakuna wanasiasa.
Tuwatazame wanasiasa walio ktk vyama vya siasa vingine vilivyo nje ya serikali...

2. PILI, vigezo vikubwa tunavyoweza kuvitumia ktk kupiga kura na kupick mwanasiasa/wanasiasa hawa vinaweza kuwa;
å Consistence ktk misimamo yao
å Wasioshawishika kirahisi kubadili misimamo yao na kufanya kile kilichoitwa "kuunga juhudi"
å Ushawishi (influence) yao ktk jamii

KWANGU MIMI; Hawa wawili tu mpaka sasa ndiyo wanasiasa hawajawahi kuyumba ktk misimamo pamoja na kupitia misuko suko ya kila aina ikiwemo kufungwa jela, kuingia ktk majaribio ya kuuwawa na Mungu kuwasaidia na kuwaponya, kufilisiwa rasrimali zao na taabu zingine zote za watawala, lakini kamwe hawajawahi kuogopa na kubadili misimamo yao...

å TUNDU A. M LISSU
å FREEMAN A. MBOWE

Hawa wawili wako kwenye kundi la viongozi wanaoitwa "Influential leaders" and it's very true wanawa - influence vijana wengi hata kuona na kuelewa maana ya SIASA..

3. TATU yupo mtu anaitwa ZITO Z. R. KABWE anatajwa tajwa sana kuwa awe kwenye orodha. Ni sawa kabisa kuwa, huyu ndugu ni mwanasiasa mmoja mzuri sana...

Lakini anakosa sifa moja muhimu sana ambayo mwanasiasa yeyote makini anapaswa kuwa nayo. Sifa hii ni UVUMILIVU...

Huyu ndugu ni rahisi sana kumteka na kumfanya akane misimamo wake, awakane wenzake maarufu kama "Sell out" kwa kutumia vishawishi kama pesa, madaraka nk nk...

Huyu ndugu hawezi kusubiri kwa maana kwamba hawezi kuvumilia...!

Mimi nasema ni makosa kumweka ktk orodha hii...
 
Mpaka sasa siasa za Tanzania ziko chini ya kivuli cha Mwalimu Nyerere. Nchini kwetu unaruhusiwa kumkashifu na kumkejeli Mungu, lakini huruhusiwi kabisa kumkashifu wala kumsema vibaya Mwalimu Nyerere. Kila kiongozi/mwanasiasa wa Tanzania anayeibukia jamii humpima kwa kumvalisha viatu vya Nyerere na kama havitamtosha basi ataonekana ana walakini fulani hata kama ni mtu mzuri.

Tanzania ina miaka 60, mpaka sasa kumekuwa na vizazi vitatu. Sehemu kubwa ya maisha ya vizazi hivi yamejengwa kwenye msingi wa Falsafa za mwaka 1967 (Ujamaa na Kujitegemea): Aidha kwa mazuri yake au mabaya yake. Hivyo nadhani unavyozungumzia sura ya siasa za Tanzania tokea mwaka 1967 hadi miaka mingine ijayo, zimwi la Nyerere halina mpinzani.

Nyerere's Ghost will haunt this state for many generations to come......
Either for better or worse....
Tatizo la Nyerere ni moja, hata kama humpendi kwa kiasi gani yaani kuna kitu tu utakubaliana naye.

Ndio maana nchi hii karibia kila kundi kuna mambo wanakubaliana na Nyerere ikiwemo Wapinzani.

Binafsi naona Failure kubwa ya Nyerere ilikuwa kwenye UCHUMI, lakini aliidhoofisha baada ya kung'atuka ili mtu mwingine arekebishe.

Na strength kubwa ya Nyerere ipo kwenye MAADILI (Kutokujilimbikizia mali, tena wakati ambao angefanya tu anavyotaka ). Na vile vile kuachia madaraka kwa hiari kitu ambacho mpaka sasa ni bidhaa adimu sana Africa.

Hata ukiwasikiliza wakosoaji wakubwa wa Nyerere hoja zao hazina nguvu.
 
Alishaharibu kitambo kwa kujikomba kwa mabeberu!
Itakuwa ngumu sana kwako kujadili hoja hii iwapo utaongozwa na hisia zako za ndani tu pasipo kuzingatia "FACTS" muhimu kumhusu mtu huyo unayemjadili...

Hoja ya "mababeru" umeibeba tu na kuiweka ktk akili yako kwa kuwa "umesikia watu wanasema"..

Lakini ukitakiwa ku - prove ukweli wa hoja hii, mimi najua kabisa kuwa utaishia kujiuma uma tu na labda unaweza kujijitetea kwa kusema " mimi nimesikia tu pale kwenye kijiwe cha kahawa cha mzee Mudi wanasema hivyo na mimi nikaamini"

Hata ukiulizwa ueleze maana ya "beberu" au "mabeberu" na mfano wake, pengine ukashindwa kueleza lolote...

Poor you...
 
Kama mada inavyojieleza hapo juu, kila nchi kwa nyakati tofauti hujaaliwa kuwa na mwanasiasa au wanasiasa wenye kujaaliwa vipaji vikubwa vya uongozi kiasi cha kugeuka kua kichocheo na hamasa kubwa kwa wanasiasa wanaoibukia na hata wasio wanasiasa. Ndipo nikajiuliza tunao wanasiasa wa namna hiyo kama nchi kwa sasa?
BAVICHA_&_CHASO_on_Instagram:_“Enzi_hizo_Lijuakali_hapajui_mjini._%0A%0ALeo_anamtukana_Mwe...jpg
Tutamtoa_Mkoloni_Mweusi_Soon_on_Instagram:_“Mwenyekiti_wa_Chadema_Taifa_akisalimiana_na_Waziri...jpg

FB_IMG_1589397986327.jpg

No_Hate_No_Fear_on_Instagram:_“Uongozi_ni_kusikiliza.”%22_.jpg
 
Kama mada inavyojieleza hapo juu, kila nchi kwa nyakati tofauti hujaaliwa kuwa na mwanasiasa au wanasiasa wenye kujaaliwa vipaji vikubwa vya uongozi kiasi cha kugeuka kua kichocheo na hamasa kubwa kwa wanasiasa wanaoibukia na hata wasio wanasiasa. Ndipo nikajiuliza tunao wanasiasa wa namna hiyo kama nchi kwa sasa?
HAKUNA MWANASIASA BORA DUNIANI KUMZIDI MAGUFULI
 
Back
Top Bottom