Hivi ni mwanasiasa gani kwa sasa mwenye mvuto na ushawishi zaidi kwa jamii ambaye anastahili kuwa alama ya siasa za Tanzania?

Aliepigwa risasi 16 akimpinga dikteta ndio the best alimwaga damu kutetea nchi.
 
Ahahahahaha mama njoo uchungulie huku,ndo utajua wabwabwaji wa kwenye mitandao ndo hawa wa upinzania.

Ukisoma mawazo yao na kuyazingatia wanamwingiza mtu chaka.
 
Mpaka sasa siasa za Tanzania ziko chini ya kivuli cha Mwalimu Nyerere. Nchini kwetu unaruhusiwa kumkashifu na kumkejeli Mungu, lakini huruhusiwi kabisa kumkashifu wala kumsema vibaya Mwalimu Nyerere. Kila kiongozi/mwanasiasa wa Tanzania anayeibukia jamii humpima kwa kumvalisha viatu vya Nyerere na kama havitamtosha basi ataonekana ana walakini fulani hata kama ni mtu mzuri.

Tanzania ina miaka 60, mpaka sasa kumekuwa na vizazi vitatu. Sehemu kubwa ya maisha ya vizazi hivi yamejengwa kwenye msingi wa Falsafa za mwaka 1967 (Ujamaa na Kujitegemea): Aidha kwa mazuri yake au mabaya yake. Hivyo nadhani unavyozungumzia sura ya siasa za Tanzania tokea mwaka 1967 hadi miaka mingine ijayo, zimwi la Nyerere halina mpinzani.

Nyerere's Ghost will haunt this state for many generations to come......
Either for better or worse....
Hili taifa lenu lina mapepo makubwa sana
 
Itakuwa ngumu sana kwako kujadili hoja hii iwapo utaongozwa na hisia zako za ndani tu pasipo kuzingatia "FACTS" muhimu kumhusu mtu huyo unayemjadili...

Hoja ya "mababeru" umeibeba tu na kuiweka ktk akili yako kwa kuwa "umesikia watu wanasema"..

Lakini ukitakiwa ku - prove ukweli wa hoja hii, mimi najua kabisa kuwa utaishia kujiuma uma tu na labda unaweza kujijitetea kwa kusema " mimi nimesikia tu pale kwenye kijiwe cha kahawa cha mzee Mudi wanasema hivyo na mimi nikaamini"

Hata ukiulizwa ueleze maana ya "beberu" au "mabeberu" na mfano wake, pengine ukashindwa kueleza lolote...

Poor you...
Ndio watz walivyo, wapo kama li bendera
 
Kama mada inavyojieleza hapo juu, kila nchi kwa nyakati tofauti hujaaliwa kuwa na mwanasiasa au wanasiasa wenye kujaaliwa vipaji vikubwa vya uongozi kiasi cha kugeuka kua kichocheo na hamasa kubwa kwa wanasiasa wanaoibukia na hata wasio wanasiasa. Ndipo nikajiuliza tunao wanasiasa wa namna hiyo kama nchi kwa sasa?
Samia Suluhu Hassan
 
Back
Top Bottom