Hivi ni makampuni gani ambayo yalifanya shughuli zake kihalali kabisa nchini, na yalifunga shughuli baada ya utawala wa Magufuli kuingia madarakani?

Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
6,516
2,000
Hii ilinishangaza sana... WALIPOSEMA HAWAKUSAJILI,
1. Michango ya NSSF/PPF ya wafanyakazi ilikuwa inafikaje huko kwa jina gani!?

2. Mishahara ya wafanyakazi, ilikuwa inalipwa kupitia BENKI, hizo electronic transfer zilikuwa zinafanyikaje na huku hawakusahiliwa!?
3. OSHA certificates zilipatikanaje!?
4. ILE HT line ya kutoka Shinyanga hadi KMCL TANESCO walikuwa wanapeleka Bill's za umeme kwa jina gani!?

5. Serikali, PAYE za wafanyakazi walizipokea wakiwa wanafanya kazi wapi!?
6. HELB nao walikuwa wanakata mikopo ya waliosoma elimu ya juu, walikuwa wanakata vipi!?
7. Twiga cement nao yale maloli yao yalikuwa anapeleka cement kwa nani!?

8. KMCL walikuwa na ndege DASH 8, ilikuwa inatumiaje uwanja wa ndege wa Dar? Na ile airstrip ya pale kakola, waliruhusiwaje kuijenga!?

BY THE WAY, MKAPA NDO ALIUFUNGUA MGODI NA ALIPEWA ZAWADI YA SEPETU YA DHAHABU... hii nayo ilikaaje!?
Marehemu magufuli alikuwa mwongo sana
 

jiwemton

JF-Expert Member
Feb 27, 2017
274
500
Uhuni wao n nn hebu leo nijuze maana ninachojua zilikua n fitina kukwepa competition
 

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
8,540
2,000
Makampuni ya Manji, Mbowe, Mo..Chupuchupu baada ya kuvishwa kanga, Dangote naye almanusura afunge kiwanda n.k
Naelewa manji ndio kakimbia ila makampuni yake yako ila mipango yake ya kifisadi kama kumiliki ufukwe wa koko beach imekomeshwa.
 

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,527
2,000
Kumekuwepo na tuhuma nyingi sana mitandaoni, na sehemu mbalimbali toka kwa baadhi ya watanzania wenzetu , yakwamba enzi ya utawala wa Magufuli wafanyabiashara wengi na makampuni yaliacha kufanya biashara halali na kuondoka nchini,kisa walionewa?

Naomba kupitia uzi huu tutaje baadhi ya wafanyabiashara na makampuni hayo ambayo biashara zao zilisajiliwa brela na yalifanya biashara kihalali nchini na yalikuwa yakilipa kodi stahiki kwa taifa letu.
Wimbo huu umeshamiri sana ,kukata mzizi wa fitina twendeni na facts.

Isije kuwa kampuni na wafanyabiashara wakwepa kodi ndio waliokimbia na sasa wanaamini mwendazake hayupo tena hivyo ni fursa tena kwao .?
Inawezekana kufanya utafiti na kuanika majina ya kampuni ulizosema. Lakini kuna njia nyingine.

Kwanza kabisa kauli hiyo imetolewa na Rais Samia, na kuwataka TRA wajirekebishe.

Hoja yako ndio ilikuwa majibu standard miezi ya mwanzo ya Sera mbovu za uchumi za Magufuli. Kwamba biashara zinazofungwa ni za wapiga dili.
Kikao cha wafanyabishara na Rais Magufuli kilifichua mengi. Na hoja hii ilishakufa.

Kwamba bado unaishadidia, inaonesha kiwango chako cha kupagawa na Umagufuli. Kila la heri
 

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
770
1,000
Ka
Shopprite, Choppies, Nakumat, Quality Group, Rhino Cement, Schrumberger, Fast Jet, Kampuni ya Waturuki iliyokuwa na Maduka Makubwa Mbezi Beach Dar es Salaam, Kampuni zilizokuwa zinamunia na kunangua korosho Mtwara, Mkono Advocates, Mbinga Bank, Twiga Bank, Bank M, Bank ya Wanawake, Bilicanas club, Mashamba ya Mbowe ya Hai, SIMON Group na mengineo mengi saana
Kampuni ya tumbaku Morogoro?
 

Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
2,336
2,000
Hauna unachokijua baina ya bgml na acacia/abg ndo nikakuuliza vile. Keep in mind bgml still existing mpaka dakika hii.
Hehehe basi weka taarifa zako tuzisome kwamba Bulyanhulu Gold Mine Limited ndo iliyopo sasa.
labda unachanganya kati ya Barrick Gold Mine na Bulyanhulu Gold Mine.Barrick Gold Mine ndo babu yao na hivyi ni vitawi tu kama hiyo BGML iliyobadilishwa kitambo na kuwa ABG.
 

Times9

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
3,167
2,000
Bgml yaani bulyanhulu gold mine ule mgodi haupo brela?
Daah! Umenikumbusha mbali sana, Meko aliwazingua hawa jamaa BGML mpaka nikakosa sponsor yao ya kunisomesha uinjinia Marekani yaani kila kitu kilikua kimeenda vizuri ila walivyoanzwa kuzinguliwa na yule shetani mambo yakaharibika...
 

Bukali

JF-Expert Member
May 7, 2018
1,208
2,000
Shopprite, Choppies, Nakumat, Quality Group, Rhino Cement, Schrumberger, Fast Jet, Kampuni ya Waturuki iliyokuwa na Maduka Makubwa Mbezi Beach Dar es Salaam, Kampuni zilizokuwa zinamunia na kunangua korosho Mtwara, Mkono Advocates, Mbinga Bank, Twiga Bank, Bank M, Bank ya Wanawake, Bilicanas club, Mashamba ya Mbowe ya Hai, SIMON Group na mengineo mengi saana
Shoprite walikwisha yumba siku nyingi, hata hivyo walijuwa wanauza kwa Nakumati.
 

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,547
2,000
1. Kampuni ya Panasonic ilifunga kiwanda Dar na kurudi Japan

2. Nakumati hawa wawekezaji toka Kenya walikuwa na maduka makubwa Malls Dar, Arusha na Moshi kote wamefunga baada ya 2015

3. Fast Jet kampuni ya usafirishaji wa anga kwa bei chee.

4. Magazeti ya Mtanzania (kampuni siijui)
Wote hao wanajulikana je wasiojulikana ni wangapi?
 

Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
6,516
2,000
Hehehe basi weka taarifa zako tuzisome kwamba Bulyanhulu Gold Mine Limited ndo iliyopo sasa.
labda unachanganya kati ya Barrick Gold Mine na Bulyanhulu Gold Mine.Barrick Gold Mine ndo babu yao na hivyi ni vitawi tu kama hiyo BGML iliyobadilishwa kitambo na kuwa ABG.
Bulyanhulu haijawahi kubadilishwa kuwa abg bali abg ilianzishwa ili kusimamia kampuni za buly, buzwagi na north mara. Abg/barrick ni kampuni mama inayosimamia makampuni ya bulyanhulu mine, buzwagi mine na north Mara mine so bgml ipo na itakuwepo.
 

Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
6,516
2,000
Daah! Umenikumbusha mbali sana, Meko aliwazingua hawa jamaa BGML mpaka nikakosa sponsor yao ya kunisomesha uinjinia Marekani yaani kila kitu kilikua kimeenda vizuri ila walivyoanzwa kuzinguliwa na yule shetani mambo yakaharibika...
Marehemu dikiteta magufuli aligharimu ajira za watanzania elf2 pale bulyanhulu.
 

Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
6,516
2,000
Lakini Bulyanhulu, tofauti wamezimaliza wamerudi.
Nakubali lkn marehemu dikiteta magufuli alicost ajira za watanzania elf2 pale bulyanhulu, pamoja na kurudi mpaka sasa buly haijachangamka imeajiri wafanyakazi ambao hawafiki mia3
 

nature boy

Senior Member
Dec 22, 2012
104
250
Kiufupi wanaolalamika wengi ni wale ambao walikuwa na ujanja ujanja kwenye kulipa kodi ila wale ambao walikuwa wanalipa kihalali wanadunda mpaka saivi. Siasa mda mwingine ni ujinga flani ivi wa kudanganya watu kama hawana akili
Mama Samia ktk hotuba yake aliwaambia TRA warejeshe pesa za wafanyabiashara na kufungua account zao. We ukiliona hilo?. Au hujaelewa hapo.
 

Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
2,336
2,000
Bulyanhulu haijawahi kubadilishwa kuwa abg bali abg ilianzishwa ili kusimamia kampuni za buly, buzwagi na north mara. Abg/barrick ni kampuni mama inayosimamia makampuni ya bulyanhulu mine, buzwagi mine na north Mara mine so bgml ipo na itakuwepo.
We ndo unachanganya Barrick ndo msimamizi wa migodi yote tangu zamani yaani mgodi wa Bulyanhuru,North Mara nk, BUlyanhulu Gold Mine aweje msimamizi.
walichokifanya wazungu ni kutenganisha tu share zilizokuwa kwenye migodi yao ya Africa na migodi mingine duniani ndo hao Barrick wakabadilisha jina kwa migodi iliyopo Africa kuwa Africa Barrick Gold mine.
ile ilikuwa ikiitwa BGML ikawa Africa Barrick Gold mine Bulyanhulu,na Buzwagi Gold Mine ikiitwa Africa Barrick Gold Mine Buzwagi nk.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom