Hivi ni mafunzo rasmi, mazoea au kitu gani?

wapalepale

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
259
56
Jamani karibu 'makonda' wote wa daladala wanapotoa msaada kwenye tuta kwa abilia wa huwasisitiza watangulize mguu wa kushoto. Huwa nashindwa kuelewa ni kwa nini nimeona niwaulize wenzangu kwanza huenda inahusiana na physics, geog or the like.

Nawasilisha
 
Okey! Iko hivi, milango ya daladala ipo upande wa kushoto, unaposhuka wakati gari bado inatembea unatakiwa uangalie mbele kwenye uelekeo wa gari ili usije ruka ueleko kinzani na ule wa gari. Na wazoefu wanaporuka, huongezea na kamwendo ka kukimbia kwa hatua chache, katika hali hiyo ukitanguliza mguu wa kulia utashindwa kufanya hicho hapo juu na kuna uwezekano mkubwa wa kujivunja enka... Kama milango ingekuwa upande wa kulia wa gari vivyo hivyo tungetanguliza guu la kulia kwenye msaada!
 
nimekusoma mkuu thanx a lot
 
Binadamu wote huanza hatua kwa guu la kulia the opposite ina- cancel force,umeelewa
 
Wapalepale, Mphamvu kakujibu kwa uzuri. Lakini nakuongezea jibu kwa mujibu wa swali lako.

Hiyo ni pure physics. Inahusu principles/laws of motion, gravitational force and balancing, centripetal forces, etc
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom