Hivi ni lazima Mawaziri wanapoongea kumtaja taja Rais kila baada ya sentensi mbili?

The unpaid Seller

JF-Expert Member
Oct 27, 2019
1,876
5,428
Salaam,

Hapa nilikua nasikiliza hotuba ya waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa alipokua anazungumza na maafisa Mawasiliano wa mikoa, aise jamaa kamtaja rais zaidi ya mara 20.

Ndio kuna mahala katika hotuba kuna uhitaji wa kumtaja rais labda kuna maagizo au nukuu au kufanya rejea ya matukio nk ila jamaa anataja hata ambapo hamna logic katika mtiririko wa hoja wala umuhimu wa kumtaja.

Yani anaweza kua anaongelea jambo fulani afu ghafla tu "nampongeza rais mama yetu mpendwa mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama yetu mpendwa sana Samia Suluhu Hassan " . Yani mpaka hotuba inaisha kaitaja hiyo paragraph ya kumpongeza rais zaidi ya mara 20.

Na sio yeye tu ukichunguza mawaziri wakuu wa mikoa na wilaya wote wana huu utaratibu. Hili limekaaje ? au ndio woga, au kumjaza kichwa mama yetu, au ni kutojiamini, au vyote ?! Au ni nini?

Screenshot_20220711-080641_Gallery.jpg
 
Sio lazima kwani ni uoga na kupenda sifa zisizo na ulazima yaani kudeka ndiko kunawasumbua hawa watu.
Pia ni kutokujiamini kwao katika majukumu waliyopewa kuyafanya
Itakuwa hujui kitu. Hao wamejifunza somo kutoka kwenye kung'atuka kwa Job Ndugai.
 
Back
Top Bottom