Hivi ni lazima chaguzi zetu zisimamiwe na wasimamizi kutoka nje? Afrika tutakuwa watumwa mpaka lini?

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,592
11,831
Nimemsikiliza mh Bernard Membe leo ameongea jambo ambalo kwa kweli linaamsha fikira nyingi sana. Anahoji tutakwenda vipi kwenye Uchaguzi bila kuwepo kwa wasimamizi wa uchaguzi wa kimataifa? Kwasababu kutokana na Janga la corona itasababisha wasimamizi hao kuto kuja mwezi Oktoba, ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa wengine walishauri kuwa uchaguzi huo usogezwe mbele ili kutoa nafasi ya wasimamizi wa kimataifa waweze kushiriki.

Hivi ina maana sisi waafrica hatuwezi kujisimamia wenyewe kwenye chaguzi zetu?

Yani tuahirishe uchaguzi kisa tu mzungu hajaja kutusimamia?

Uko wapi uwezo wetu wa kujitawala na kujiamulia mambo yetu?

Fikira za kikoloni zitaondoka lini vichwani mwa hawa viongozi wetu?

Sasa sisi watanzania awamu hii tutafanya uchaguzi kwa kujisimamia wenyewe hatutaki hao wazungu tuone kama tutashindwa kupata viongozi makini.
 
Kama mnawategemea hao wazungu wawapatie fedha kutatulia mikwamo yenu, hadi dawa mnawaomba hao hao wazungu lazima na uchaguzi wawasimamie maana hamuaminiki
 
Hatuwezi kujisimamia; tunawategemea "mabeberu" kwa misaada yao, zaidi hatuaminiani, wenzetu wanatumia mpaka polisi kuiba kura za wananchi wapeleke upande wao.
Ila hao wazungu ndio wakuaminiwa.
 
Hivi wale jamaa huwa wanasimamia au wanaangalia tu mchakato unavyoenda?

BTW, kwa hiyo membe anataka tuvunje katiba kwa kusogeza mbele uchaguzi kisa corona?
 
Hizo hela zenyewe wanazoomba wakipewa wanatia mifukoni
Kama mnawategemea hao wazungu wawapatie fedha kutatulia mikwamo yenu, hadi dawa mnawaomba hao hao wazungu lazima na uchaguzi wawasimamie maana hamuaminiki
 
Interrnational standard.

Kila general election International observers lazima wawepo kwa nchi yoyote ile.

Africa toka UN,SADC,EAST AFRICA COMMUNITY,ECOWAS, COMESA.

Inaonekana UNPITWA uelewa na Mwanfunzi wa O-LEVEL.

Shuleni kwenu hukosoma elimu ya Uraia???

Inaonekana ndo mara ya kwanza unasikia term INTENTIONAL OBSERVERS??

Pole sana.....🤩🤩🤩🤩 SHAME ON YOU!
 
Hivi wewe unadhani kwa Tume hii hii inayoamua nani awe Mbunge eneo gani, ndiyo kweli tuna Tume huru kweli?

Naunga mkono kauli ya Membe kuwa hatupaswi kuingia kwenye uchaguzi mkuu, bila kuwa na Tume huru ya uchaguzi
 
Mpa
Kama mnawategemea hao wazungu wawapatie fedha kutatulia mikwamo yenu, hadi dawa mnawaomba hao hao wazungu lazima na uchaguzi wawasimamie maana hamuaminiki
Mpaka ARVS wanatusaidia wao.....🤩🤩🤩 Niambe mzee Baba MMAWIA
 
Yaani kifupi jiwe hachomoki kachero mbobezi kaweka goti shingoni mwa jiwe yaani hakuna kupumua
 
Back
Top Bottom