Hivi ni kweli watanzania sio waelewa kiasi hiki?

beal

Senior Member
Dec 30, 2012
114
60
Kuna vitu viwili vinalazimishwa kwenda sawa hapa.
1. Ukame
2. Njaa.

Ukame wa sasa hauwezi kua na immediate effect kwenye stoo zetu. Ikiwa hakuna mvua sasahivi, au mvua zipo nyingi sasahivi, hakuna uwezekano wa leo au kesho kuwa na njaa au neema ya chakula. Impact tuione kwenye kipindi cha mavuno.

Njaa.
Hii njaa imetoka wapi? (Naomba majibu) hali ya hewa msimu uliopita ilikuaje? Je tulikua na mavuno au hatukuanayo? Yalikua yakutosheleza au hafifu? Kama yalikua hafifu ni sawa kua na hali ya njaa kwakua balance haikua yakutosha. Kama tulikua na mavuno ya kutosha, chakula kikowapi? Kwa mujibu wa Mh. JUMA kuna wabunge waliomba kutolewe kibali cha kuuza chakula nje ya nchi, hii maana yake tulioata mavuno ya kutosha. Na chakula kiliuzwa kingi kiasi cha kutoweka akiba ya kutosha.

Naomba wataalam wa kufatilia mambo waniambie miaka mitatu ikiyopita, muda kama huu Dec, Jan na Feb hali ya mahindi hua ikoje?

Tusijikute tunaongelea tusilolijua kwakua tumeshikiwa vichwa na wale vijana wana TANZAGIZA
 
Ipo hivi wakulima wengi ni wa jembe la mkono na serikali yetu haitoi ruzuku kwa wakulima hivyo mkulima huwa anategemea mvua ili alime vibarua kwanza ndio akalime kwake.walio na mahindi kwa sasa ni wafanyabiashara mkulima amebakiwa na mbegu tu JPM bila kujielewa anaongea asivyovijua
 
Kuna vitu viwili vinalazimishwa kwenda sawa hapa.
1. Ukame
2. Njaa.

Ukame wa sasa hauwezi kua na immediate effect kwenye stoo zetu. Ikiwa hakuna mvua sasahivi, au mvua zipo nyingi sasahivi, hakuna uwezekano wa leo au kesho kuwa na njaa au neema ya chakula. Impact tuione kwenye kipindi cha mavuno.

Njaa.
Hii njaa imetoka wapi? (Naomba majibu) hali ya hewa msimu uliopita ilikuaje? Je tulikua na mavuno au hatukuanayo? Yalikua yakutosheleza au hafifu? Kama yalikua hafifu ni sawa kua na hali ya njaa kwakua balance haikua yakutosha. Kama tulikua na mavuno ya kutosha, chakula kikowapi? Kwa mujibu wa Mh. JUMA kuna wabunge waliomba kutolewe kibali cha kuuza chakula nje ya nchi, hii maana yake tulioata mavuno ya kutosha. Na chakula kiliuzwa kingi kiasi cha kutoweka akiba ya kutosha.

Naomba wataalam wa kufatilia mambo waniambie miaka mitatu ikiyopita, muda kama huu Dec, Jan na Feb hali ya mahindi hua ikoje?

Tusijikute tunaongelea tusilolijua kwakua tumeshikiwa vichwa na wale vijana wana TANZAGIZA
9563ae0119ed30fb6c166dec734436b1.jpg
 
Hapa ndipo ninapoamin kuwa vijana wengi wa kitanzania wana akili za kushikiwa, MTU badala ya kujibu hoja anakimbilia ktk kusadikika
 
Ukame wa mwaka huu unatengeneza njaa ndani ya miezi 6 ijayo kama hatua stahiki hazichukuliwi. Hivyo kuhusisha njaa na ukame uliopo ni sahihi kabisa.

Sasa projection ya chakula kuanzia sasa tunapokuwa na ukame ikoje? Tukiangalia akiba tuna tani 90,000 tu tofauti na miaka iliyopita, sio hilo tu bei ya mahindi imepanda tofauti na miaka ya nyuma ikihashiria upungufu wa bidhaa hii. Hii nayo inaonyesha tuna njaa sasa na tutakuwa na njaa zaidi baada ya miezi sita kama ukame utaendelea.

Kwa uchumi wa Tanzania usiotegemea kilimo cha umwagiliaji na umasikini wa kushindwa kuhifadhi chakula na kuingiza kutoka nje kwetu sisi UKAME = NJAA. Mengine yote utakayoongea ni siasa au kujaribu kutetea kundi fulani la watu.

Tunaweza kujadiri kiasi cha njaa kitakachotokea na uwapo wa mvua chache maeneo kadhaa lakini hatuwezi kusema ukame tulio nao hautaleta njaa.
 
Ukame uwe wa mwaka jana , juzi au mwaka huu, wewe toa jibu lako njaa ipo au haipo? Tuanzie hapo kwanza.
Hawajamlaumu yeye mkuu kuwa ameleta njaa, ila kunasehe baadhi ya mikoa wameshaanza kuomba msaada wa chakula. Wewe unaekaa Dar ndani ya kiyoyozi, huwezi jua wenzako mvua zikiwa zinanyesha huwaga wanapata neema ya vitu vingi, mbali na kulima na kupanda mazao, kuna upatikanaji wa maji ya kunywa kwa watu + mifugo, kuna mboga za majani. Wewe kama huvijui vyote hivyo, endelea kukusanya remote kwenye meza + usisahau kuseti kiyoyozi baridi liwe 18.
 
Back
Top Bottom