Hivi ni kweli Watanzania hatuwezi kufanikiwa bila kuiba au kugushi?

Magehema

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
428
27
Kuna dhana imeanza kujengeka miongoni mwa watanzania kwamba haiwezekani kufanikiwa katika maisha bila kufanya usanii (kuiba, kughushi, kula 10% illegally etc), matokeo yake kumekuwa na matukio kemkem ya matumizi mabaya ya madaraka katika nyanja mbali mbali. Je dhana hii ina ukweli wowote?
 
Nakuunga mkono kamanda, Kampuni ninayo fanyia kazi watu wanaiba mno, watu wamekula mpaka 500 millioni, dream ya vijana sasa hivi ni nitoke vipi na hizo 10%. kila mtu kwenye nafasi yake anafanya ufisadi. Mtu akipewa pesa na kampuni akanunue kitu fulani ananunua used badala ya Brand new, yaani kazi kweli kweli. magari watu wananunua, wanajenga house za millioni 200 mbezi huko, lkn mshahara wake ukiambiwa utashangaa, ndio hivyo Bongo mambo yanavyokwenda ni WIZI MTUPU.
 
Na baada ya hapo ndio maana hatuna uchumi endelevu; fedhaumezipata kwa wizi hata zikiwa bilioni ni mara chache sana zikafaidisha jamii yako; iliyo mara nyingi unaishai kumiliki assets tu kama hivyo!
 
Na baada ya hapo ndio maana hatuna uchumi endelevu; fedhaumezipata kwa wizi hata zikiwa bilioni ni mara chache sana zikafaidisha jamii yako; iliyo mara nyingi unaishai kumiliki assets tu kama hivyo!

True man!!
we dont do a thing with them money!
tunajenga na kununua gari, kwisney! sana sana labda kujenga gesti hausi, kwasababau tunawaza ngono zaidi!
 
Braza, kwa Tanzania kufanikiwa bila...

...Kukwepa kodi..
...Kutumia muda wa ofisi yako kwa kazi zako...
...Kutumia rasilmali za ofisi kwa kazi zako....
...Kutoa udhuru kazini ili usimamie miradi yako...

Ni ngumu sana.
Afrika is just how it is.
Let it be.
 
yes inawezekana kufanikiwa bila kufanya usanii ukimwamini mungu maana ndiye atupaye nguvu za kupata utajiri.

wengi kweli utajiri wao ni wakisanii mtupu ebu jaribu siku kumuliza tajiri wa kitanzania naomba uniambie umepataje utajiri wako na mm nijifunze sikiliza majibu atakayo kupa
 
dah nimeanza kuonja machungu ya kupigwa usanii,jamaa yangu ambaye tulikua tunashirikiana biashara nikiwa hapo bongo yaani sasa hivi ananifanyia usanii mpaka nakoma maana kila biashara nikimtumia auze akishauza analeta hadithi nyiiingi mpaka nije kupata hiyo hela yaani utafikiri naomba msaada tena,namimi naona noma kumuwekea kibesi,halafu usanii wake unapomsikiliza unagundua tu huyu ananidanganya,lakini poa sasa hivi naachana naye kabisa nishachoka.
 
Inawezekana ukafanikiwa bila kuiba wala kughushi,tatizo itabidi uwe mvumilivu sana na ufanye kazi sana na kwa kufuata taratibu na sheria zetu.

Asilimia kubwa ya vijana sasa hivi si waaminifu kihivyo. Raha ni pale unapofanikiwa kihalali kwa sababu unakuwa jasiri kuelezea mafanikio yako bila hofu kwa wanao na jamaa zako,huna dhambi(kwa waumini),mafanikio yako ni endelevu pia kwa asilimia kubwa.

ni maoni yangu.
 
Back
Top Bottom