Hivi ni kweli Watanzania hatuoni faida ya kuwa na Upinzani imara?

kwenyula

Member
Aug 28, 2016
36
150
Hakuna kitu roho inaniuma kama kuona Upinzani nchi hii wakiwa wanazongwa kila kona. Wanaonekana hawaitakii mema nchi hii; wananyanyasika, hata wakipata matatizo wanachekwa, wamerundikiwa kesi lukuki kila kukicha mahakamani mara polisi yaani hata zile haki zao za kikatiba wananyimwa na Watanzania wanaona sawa tu.

Hivi tumesahau hata Rais huyu wa sasa CCM walilazimika kumpa nafasi ya kugombea 2015 kutokana na kuwepo Upinzani imara (UKAWA)?

Hivi tunadhani hii shauku na moyo wa kujituma alionao Rais na CCM kwa Watanzania siku upinzani ukifa moyo huo utakuepo?

Hivi tunadhani kwamba hawa wanasiasa wa Upinzani ambao wamekuwa wakijitoa kila kukicha kuishauri serikali, kuikosoa na kuipa changamoto za fikra za kimaendeleo wakisema wote wahamie CCM watakosa ulaji?

Hivi kweli Tundu Lissu akiamua kuwa kama Dr. Slaa atapoteza nini? Hivi Zitto akiamua kuwa kama Prof Kitila atapoteza nini? Hivi Mbowe akiamua kuwa kama Mrema atapoteza nini!?

Saivi kila msanii anaimba wimbo wa kuwazodoa upinzani kama vile wanamlani shetani.

CCM hii bila upinzani imara itabweteka, itatunyanyasa Watanzania, watatuibia sana hawa. Hivi vinavyofanyika saivi vilitakiwa vifanyike kipindi cha CCM ya Nyerere.

Watanzania kuna siku tutakuja kujuta. Wapinzani walipaswa wapewe moyo kwani wana mchango mkubwa sana katika hili Taifa.
 

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
4,337
2,000
Kila kitu ni fursa, hakuna mtu anayekufanyia mema usione wanalialia... kama haileti hela kwako hai-make sense tu.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
3,907
2,000
Unataka CCM dhoofu na mahututi kama hii ya awamu ya tano ndiyo iwe na Upinzani imara! Wenyenye tu ndani ya chama wanamsema Mwenyekiti wao kwa kificho!

Kiufupi tu mzee hana hulka ya kupenda upinzani au kukosolewa kwa namna yoyote ile. Na hajawahi kujificha katika hilo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom