Hivi Ni Kweli Watanganyika Hawajui Siasa za Zanzibar!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Ni Kweli Watanganyika Hawajui Siasa za Zanzibar!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by X-PASTER, Aug 10, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Aug 10, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Katika pita pita zangu mitandaoni nilikutana na article moja ambayo ilivuta macho yangu, baada ya kuisoma na kutafakali niligundua udhaifu mwingi wa hoja zilizotolewa humo, japokuwa mwandishi aliungwa mkono na wachache. Nami nikaona niiweke hapa ili wasomaji wengine wapate kuisoma na ikiwezekana waelewe nini kinaendelea kwenye vichwa vya watu wachache dhidi ya Watanganyika.

   
 2. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mbona hakuna mahali alipotueleza hiyo siasa iliyo pekee kwa Zanzibar ikoje?

  Amandla..........
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Aug 10, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  X-PASTOR,
  Achana nao hao kama kweli wao wanazijua siasa Za zanzibar mbona hizo kura za maoni pekee zimeonyesha kugawanyika? Na laukama wanasema haikutolewa ELIMU ya kutosha, sii ndio sawa na kusema hata wao wenyewe hawajui siasa zao wenmyewe!
  Wee subiri tu utasikia matokeo ya Kura na CUF wamebakia na kitu gani ndipo wataijua chuki iliyopo ndani visiwani kwenyewe.. CCM na CUF Zanzibar ni maadui kuliko CCM na CUF Bara..
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..jamani wa-Tanganyika tuko milioni 40 wakati wa-Zenj idadi yenu ni milioni 1 na ushee.

  ..Tanganyika ni kubwa mno na ina mambo mengi ya msingi ya kuyajua zaidi ya siasa na migogoro ya wa-Zenj.

  ..zaidi, wa-Tanganyika tuna matatizo[barabara mbovu, elimu,afya,mazingira,rasilimali kuibiwa,viongozi mafisadi...] lukuki ya kuyashughulikia sasa mwandishi bila staha wala huruma anataka kututwisha mzigo mwingine wa mgogoro wa siasa za wa-Zenj.

  ..mwandishi anapaswa kutofautisha kati ya viongozi wa kisiasa wa CCM-bara na wananchi wa kawaida wa Tanganyika. angeliweza kufanya hivyo nina hakika angeandika makala tofauti kabisa isiyo na shutuma za jumla-jumla dhidi ya wa-Tanganyika wote.
   
 5. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Wanachofanya hawa jamaa ni kukacha kujadili matatizo yao kwa kutafuta mchawi atakayewaunganisha. Badala ya kukaa na kuangalia Pemba na Unguja zinawezaje kuwa pamoja wanashupalia Muungano! Au wanataka kutuambia kuwa Muungano ndiyo chanzo cha siasa za chuki baina ya wapemba na waunguja? Wanasahau kuwa wakati wanachinjana kimbilio lao lilikuwa Bara. Hata Sultani wao alikimbilia Bara baada ya Kenya kukataa kumpa hifadhi! Wakina Babu na wengine isingekuwa bara yangewapata yaliyowapata wakina Hanga na Mdungi. Leo hii wanakuja na kiburi na kutuambia ati hatujui siasa zao!

  Amandla......
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..mimi naona ni vizuri tu wanavyodai wameungana sasa hivi.

  ..sasa waje Dodom ndani ya Bunge la Jamhuri na wajenge hoja kwamba wanaonewa.

  ..masuala ya Muungano yanapaswa kuzungumziwa ktk Bunge la Jamhuri Dodoma.

  ..tatizo la hawa "ndugu zetu" ni kwamba suala likizungumziwa Dodma wanakaa kimya, halafu baadaye unasikia makelele toka maskani na baraza la wawakilishi Zenj.
   
 7. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ni kwasababu wakija bunge la muungano wanakutana na kizingiti cha Halmashauri kuu ya CCM Bara ambapo ukiingiza swala Muungano unashughuliwa vilivyo na Halmashauri kuu ya Chama (umesahau yaliyomkuta Aboud Jumbe?) Sasa ni bora wapige kelele kule kwani huku mpaka labda wakiwa wabunge wengi Chadema ndio utaiona hoja ya muungano inaibuliwa venginevyo hakuna mtu atakayesema Dodoma
   
 8. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kudadadeki! Kama mnaona aibu kuitwa wa tanganyika wezenu wanaona fakhari kuitwa wazanzibar, nyie kaeni tu! Sisi wa tanzania, waZenj wameshtuka muungano ni nchii mbili Tanganyika na Zanzibar, Zanzibar ipo ile Tanganyika iko wapi? Aaaaaaah kumbe Zanzibar inatawaliwa na Tanganyika iliyojivisha koti la Tanzania, sasa Wazenj wanataka kulivua hilo koti,waiweke Tanganyika pale na Tanzania pale na Zanzibar pale.
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Mdondoaji,

  ..tatizo ni kwamba ukiwa Zenj unaweza kutamka jukwaani kwamba Tanganyika inainyonya Zenj, na kwamba wa-Zenj wanawalisha wa-Tanganyika na wananchi wakakuamini. kuna wachangiaji wengi hapa JF wameleta kauli kama hizo walizozipata kwenye mikutano ya Maalim Seif na CUF.

  ..bungeni Dodoma huwezi kuleta kauli zisizo na utafiti kama hizo. wabunge watakuhoji na kudai ushahidi, pia wengine wataleta ushahidi unaopingana na hoja zinazowadhalilisha wa-Tanganyika.

  ..pia Muungano unawafaidisha sana kiuchumi wanasiasa wa-Zenj kwa hiyo hawawezi kutoa maneno ya shutuma dhidi yake kama wanayoyatoa wakiwa Zenj. Aboud Jumbe aliyekuwa akipinga Muungano amejisitiri huku Kigamboni Mjimwema sijui kwanini haendi kuishi Zenj. Kiongozi wenu Hamad Rashidi amekuwa akiganga njaa Tanganyika kama mjasirimali wa biashara ya vyuma chakavu. Mzee Mwinyi amejimbikiza mapande makubwa-makubwa ya ardhi mikoani Tanganyika. the list goes on.

  NB:

  ..kama Muungano ni mbaya sana, basi Maalimu Seif na CUF wahamasishe wa-Zenj waliojazana huku Tanganyika kufunga vijiduka vyao na kurudi kwenye Zenj kwenye neema na utajiri.
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Aug 10, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mdondoaji,
  Mkuu sii kweli kusingizia Halmashauri kwa sababu ni hao hao viongozi wa Zanzibar wanapokuja kuzungumzia Muungano wanazungumzia nafasi zao wao kiutawala. Believe me, hawazungumzii kabisa kero za wananchi isipokuwa Zanzibar kama Nchi au Taifa -Who give the f... kama ni nchi au Taifa?

  Nakuomba waulize vizuri hao viongozi utajiri wao wameuapata vipi?..Fedha na mapato ya Zanzibar ni yanatumika vipi utawasikia wakikuita wewe mwenyewe Mhuni kwa sababu hakuna sababu Zanzibar na Bara kutegemea Misaada hadi leo - hakuna hata kama Zanzibar itajitegemea kiuchumi. Seif mwenyewe alipokuwa waziri wa Elimu aliingiza Upemba akasahau mamlaka aliyokabidhiwa ni kwa Zanzibar nzima, leo anakuja na story kibao.

  Swala moja kubwa tunalosahau wananchi ni kwamba hawa viongozi wetu ni sawa kabisa na Mkoloni, akili zao ni kututawala hivyo maslahi yote wanayatazama kwa picha ya kutawala. Ni watumwa waliokuwa huru wanataka nao kuwa sawa na mabwana (masters) waliowaachia madaraka. zanzibar sio nchi ya kuwa matatizo waliyokuwa nayo leo kiuchumi hata kama.

  Na kwa bahati mbaya wamefanikiwa kuwajaza Ujinga wa kufikiria tu nafasi ya Zanzibar kuwa nchi au Taifa hali yapo maswala makubwa zaidi ya Muungano wa mipaka. Na amini maneno yangu tukiunda serikali tatu bado tutakuja na maswali ya viongozi ktk serikali ya Muungano watoke upande gani na jinsi gani watagawana madaraka wao hali huu sii Muungano wa viongozi au mipaka bali ni muungano wa WATU. Muungano ni kuwezesha MAZINGIRA safi ya kuishi WATU wake....

  Na hakika hizi habari za Udini nchini ndio haswa Chimbuko la swala la Muungano na hakika litatupeleka kusiko tusipoangalia kwa makini. Unamzungumzia Aboud Jumbe ambaye kitabu chake chote kimejaa mahubiri ya Udini mtupu kama vile bara hakuna Waislaam au kuna Waislaam waliotawaliwa. Mbona hakuzungumziwa alivyochopekwa yeye from nowhere wala haku deserve nafasi hiyo in the first palce?

  Hizi hofu mnazojaribu kuzipandikiza zitakuja zua mabaya zaidi ya kuimarisha Muungano kwani mkuu wangu kaburini utazikwa wewe peke yako na hakika Munkar wa Nakil anakusubiri wewe na sio serikali ya Muungano wala zanzibar.. yeye hayajui hayo..

  Kero kubwa ya MUUNGANO iwe ni WATU wenyewe. kama zipo sheria zinazomtenga Mzanzibar au Mbara au kuna mapungufu ktk mgao wa Pato la taifa hizi ndizo ziwe hoja zetu na sio mipaka yetu. Na hakika tukianzisha sababu kama hizi ndio tunarudisha ile hofu ya Karume mwenyewe kufikia Muungano huu.
   
 11. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Du! hofu kwa ajili ya nini sasa? Mbona hukuna ufaanuzi.

  I am just trying to imagine how hard it is kujitambulisha na mtu wa fikra kama hizi kwamba ni mtanzania mwenzio.
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  Aug 11, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Swali kwa Wazanzibar,
  Tanganyika inawanyonya wazenj. Tuangalie data rahisi za mitaani zenye ukweli. Bajeti ya Zanzibar kwa mwaka ni sh Billion 500. Wastani wa sh
  16.5 Billion kwa mwezi sawa na makusanyo ya soko la kariakoo/mwezi. Sasa hapa unyonjaji uko wapi!
  Je Znz inachangia kiasi gani kuendesha muungano? endapo mishahara inatoka hazina Tanganyika.
  Wazenji waeleze Tanganyika ina hofu gani na itapoteza nini muungano ukitoweka.?
   
 13. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  lazima ushangae wewe Tanzania unayoijua ni hapa Dar es salaam...umewahi kuishi Zanzibar? Umefika Mtwara? au ndio nyinyi mnakwenda mbio kutafuta hela ya bia (pombe) baadae biashara imekwisha... Kwanini Tanzania masikini?
   
Loading...