tweenty4seven
JF-Expert Member
- Sep 21, 2013
- 15,672
- 19,186
"Mimi ni Dereva wa boda boda, sijaelewa ni kwanini kila mteja ninayempakia kwenye piki piki tukianza kuongelea habari kuhusu rais wetu hua wanachukia sana na kuanza kuponda tuu,kwani amekosea amekosea wapi? sijakutana na mteja hata mmoja anayesifia utawala wake"
Yakikua ni mazungumzo kati yangu na bwana mmoja aliyekua amenipakia kwenye bobaboda kama mteja wake.
Alinishangaa sana mimi kuona ninamsifia sana sana rais wangu kwa kazi anazofanya, aliniona mimi ni mtu wa tofauti tofauti na wengine ingawa yeye pia alikua na mawazo tofauti na yangu.