Hivi ni kweli wamikili wa Vyombo vya Habari na Wahariri wamepigwa mkwara na Magufuli?

Mkuu Dombwela, please acha kutudanganya humu jf, hakuna mhariri yoyote aliyekuambia kuwa kapigiwa simu.

Yaani mhariri apigiwe simu na rais kuipangiwa namna ya kufanya kazi yake na isiwe big headline gazetini kwake, halafu ndio aje akuambie wewe Mkuu Dombwela?!.
Huu utakuwa ni uongo tuu, hakuna kitu kama hiki.

Na kama ni kweli hili limetokea na huyu mhariri hakuripoti, then huyu mhariri amevamia tuu fani ya Habari, atafute shughuli nyingine ya kufanya.

P
Mkuu ya darasani ni ya darasani. Kufanyia kazi uliyojifunza darasani ni kitu kingine. Kwa maana nyingine nadharia na vitendo ni vitu viwili tofauti.
 
Mwanzoni nilizipata hizi taarifa kwa mhariri mmoja akiniambia kuwa amepigwa mkwara na Magu kwa kupigiwa simu na Magu moja kwa moja akaambiwa amuache afanyeje kazi.

Majuzi tena nimeambiwa hivyo hivyo na mhariri mwingine kuwa naye kapigwa mkwara kuwa amuache afanye kazi!.

Nimejiuli hivi nikweli Magu amefanya hayo kwa kuwaambia waandike na kutoa taarifa zenye lengo la kusupport yale anayofanya tu na si kuchallenge anayofanya?.

Lakini pia nimejiuliza kama ni kweli, hii jeuri ya kuwapangia wamiliki na wahariri wa vyombo binafsi anaitoa wapi?, na kwanini pia hao wamiliki na wahariri wamekubaliana naye?.

Nimejiuliza sana, hivi Magu anaogopa nini? au ni uzalendo tu kwa Taifa lake?.

Haya niliyoambiwa na hawa wahariri yanaweza kuwa ni kweli au wanamsingizia Magu?.

Jamani aliyewahi kulisikia hili atushirikishe labda yawezekana hawa walioniambia nao walikuwa visa vyao kwa Magu!.

Sent using Jamii Forums mobile app

Na ndiyo maana unaona wenye ' Akili ' kubwa Siku hizi Gazeti letu, Runinga Yetu na Redio yetu ni huu Mtandao Wetu ' pendwa ' na ' uliobarikiwa ' kabisa wa JamiiForums kwani hapa unapata kila Kitu hadi yale ambaye usingeweza au kuthubutu kuyaona katika Magazeti au Kuyasikia katika Redio kama siyo Kuyatizama pia katika Runinga ( Television )

Hata hivyo sina uhakika kwamba ni kweli Rais kama Rais amewapigia Simu hao ' Gate Keepers / Editors ' na ' Kuwatishia ' hivyo kwani ' Hadhi ' ya Urais kama Taasisi ni kubwa mno nchini. Ungeniambia kuwa labda Watendaji wake wa chini ndiyo kwa ' Viherehere ' vyao wamefanya hivyo ningekuamini kwa 100% lakini kwa hili la ' Kumsingizia ' Mheshimiwa Rais moja kwa moja nitakuwa wa mwisho Kukuamini.

Kwa kukusaidia tu kwa mfumo mzima wa Vyombo vya Habari Tanzania ambavyo muda mrefu vimekuwa ni ' tegemezi ' hasa kwa upande wa kupata ' Matangazo ' kutoka kwa Wadhamini wakubwa ambao ni Serikali hawana jinsi zaidi ya kuwa Watu wa Kujipendekeza kama siyo Kujikomba Kwao vinginevyo Uhai wao kama Vyombo vya Habari unakufa Kifo Kitakatifu.

Ni mpaka pale Vyombo vyote vya Habari vya Tanzania vikiwa na ' Financial Muscle ' kama ambavyo walivyo Mwananchi Commmunication Limited chini ya Kampuni Kubwa na Tajiri tu ya Nation Media Group ndiyo wanaweza wasiwe ' wanatishwa ' mara kwa mara na Mamlaka au wakawa wanawanyenyekea.

Mwisho kabisa ukiachia mbali kuwa sijui ' wanatishwa ' hivyo ila usisahau pia ya kwamba Tanzania hatuna ' Hardcore Journalists ' kama waliopo nchini Kenya, Uganda, South Africa, Ghana na Egypt ila hapa tuna ' PR Journalists ' na ' Brown Enveloped Journalists ' na ndiyo maana unaona 95% wengi Wao wamekuwa ni Watu wa Kusifu tu huku muda wote wakihimiza kupewa ' Bakshishi / Takrima ' pale wanapoenda kufanya ' Coverages ' zao.

Huko Kunyanyasika na Kupelekeshwa na Dola / Mamlaka wamekutaka wenyewe na wasipojitoa muhanga watayaona makubwa.
 
Mkuu Dombwela, please acha kutudanganya humu jf, hakuna mhariri yoyote aliyekuambia kuwa kapigiwa simu.

Yaani mhariri apigiwe simu na rais kuipangiwa namna ya kufanya kazi yake na isiwe big headline gazetini kwake, halafu ndio aje akuambie wewe Mkuu Dombwela?!.
Huu utakuwa ni uongo tuu, hakuna kitu kama hiki.

Na kama ni kweli hili limetokea na huyu mhariri hakuripoti, then huyu mhariri amevamia tuu fani ya Habari, atafute shughuli nyingine ya kufanya.

P
Mimi niliambiwa na mkuu wa chombo fulani ni kweli anafanya hivyo ni muoga sana kwa sababu ni mwizi na mvunja katiba
 
Mwanzoni nilizipata hizi taarifa kwa mhariri mmoja akiniambia kuwa amepigwa mkwara na Magu kwa kupigiwa simu na Magu moja kwa moja akaambiwa amuache afanyeje kazi.

Majuzi tena nimeambiwa hivyo hivyo na mhariri mwingine kuwa naye kapigwa mkwara kuwa amuache afanye kazi!.

Nimejiuli hivi nikweli Magu amefanya hayo kwa kuwaambia waandike na kutoa taarifa zenye lengo la kusupport yale anayofanya tu na si kuchallenge anayofanya?.

Lakini pia nimejiuliza kama ni kweli, hii jeuri ya kuwapangia wamiliki na wahariri wa vyombo binafsi anaitoa wapi?, na kwanini pia hao wamiliki na wahariri wamekubaliana naye?.

Nimejiuliza sana, hivi Magu anaogopa nini? au ni uzalendo tu kwa Taifa lake?.

Haya niliyoambiwa na hawa wahariri yanaweza kuwa ni kweli au wanamsingizia Magu?.

Jamani aliyewahi kulisikia hili atushirikishe labda yawezekana hawa walioniambia nao walikuwa visa vyao kwa Magu!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Waambie mods warekebishe heading,wamikili-wamiliki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kina Kikwete na Mkapa hawakufanya kazi? Yeye magazeti yamzuia nini kufanya kazi wakati hajawahi hata kukutana na waandishi wa habari wakamuhoji maswali? Anajua akiinama atajamba sasa analazimisha watu wasiweke vitu chini wamuwekee mezani achukue akiwa kakaa...Hajiamini.
 
Mkuu Dombwela, please acha kutudanganya humu jf, hakuna mhariri yoyote aliyekuambia kuwa kapigiwa simu.

Yaani mhariri apigiwe simu na rais kuipangiwa namna ya kufanya kazi yake na isiwe big headline gazetini kwake, halafu ndio aje akuambie wewe Mkuu Dombwela?!.
Huu utakuwa ni uongo tuu, hakuna kitu kama hiki.

Na kama ni kweli hili limetokea na huyu mhariri hakuripoti, then huyu mhariri amevamia tuu fani ya Habari, atafute shughuli nyingine ya kufanya.

P
P. Hoja yako ungeitendea haki, Kama ungeeleza wazi mahojiano yako na Mjengoni, Kama alivyo omba yule Mkaguzi.
Ukituhumu mhariri jituhumu na wewe, mana naamini wewe ni mwandishi tena wa kujitegemea, siipati picha jinsi headline yako ingesomekaje!.
 
Tangu day one niliomba ku reserve my comments.
P
 
Yaani mhariri apigiwe simu na rais kuipangiwa namna ya kufanya kazi yake na isiwe big headline gazetini kwake, halafu ndio aje akuambie wewe Mkuu Dombwela?!.

Mkuu kuiweka headline si ndio itafanya aokotwe coco beach, Tujipe muda kama ni hadithi za umbea zitapita kimya kimya
 
Back
Top Bottom