Hivi ni Kweli waathirika wa ukimwi wanaweza kujifungua Mtoto asie na maambukizi na Mtoto huyo akakua vizuri

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,104
27,085
Kuna Mtoto alizaliwa mwaka 2009 wazazi wake walikuwa waathirika na walifariki miaka minne baadae. Mtoto inasemekana hakupata maambukizi wakati wa kujifungua . Mtoto Sasa hivi yupo darasa la saba na anaonekana ana afya njema Tu.

Je ni Kweli kabisa waathirika wanaweza kujifungua Mtoto asie na maambukizi na akaweza kusurvive ?

How?
 
100% na pia Survival sio issue, hata mtoto akizaliwa na virusi bado atasurvive Tu kama akipewa matunzo vizuri. Kama lishe ndio duni na analelewa mazingira yaliyojaa stress hapo chances ndio zinakuwa ndogo za kutoboa sabsbu ya kinga yake ya mwili kuwa rahisi kushambuliwa na magonjwa nyemelezi
 
Yes nikweli.
Ikiwa mama amepata maambukizi ya HiV na akatumia ArV kwa usahihi, basi mama huyo amaweza asimuambukize mtoto virusi na hata mume wake pia.
Mengini nitakueleza kwa kirefu nikipata nafasi
Viral load wanakua chini sana hata kwenye damu hawezi kuwa detected wanajificha kwenye viungo, Ila kukiwa na matumizi ya ARVs kwa 100 kwa waathiraka wote ukimwi utatokomezwa
 
How? Hiyo mechanism imekaaje mkuu?
Kuna program inaitwa PMTCT( prevention to mother and child transmission).

Mama akipima afya akiwa na maambukuzi ya HIV ataanzishiwa dawa, au atakuwa ameshaanza kutumia dawa kupitia CTC.

Kumbuka maambukuzi ya mtoto hutokea akiwa tumboni( kabla mtoto kuzaliwa wakati wa mimba), pia hutokea wakati wa kujifungua na kunyonyesha.

Dawa za ARV zikitumiwa kwa usahihi na wakati muafaka husaidia kufubaza virusi, kupunguza viral load na kuongeza kinga ya mwili.

Pia wakati kichanga kinazaliwa kinapewa dawa za ARV na dawa za kuzuia magonjwa nyemelezi.

Jitihada zote hizo zikifanyika mtoto atazaliwa bila na maambukizi.
 
Kuna Mtoto alizaliwa mwaka 2009 wazazi wake walikuwa waathirika na walifariki miaka minne baadae. Mtoto inasemekana hakupata maambukizi wakati wa kujifungua . Mtoto Sasa hivi yupo darasa la saba na anaonekana ana afya njema Tu.

Je ni Kweli kabisa waathirika wanaweza kujifungua Mtoto asie na maambukizi na akaweza kusurvive ?

How?
Ukiona mama hanyonyeshi mtoto wake jua huyo ni muathirika na anamkinga mtoto wake asipate maambukizi
 
Kuna program inaitwa PMTCT( prevention to mother and child transmission).

Mama akipima afya akiwa na maambukuzi ya HIV ataanzishiwa dawa, au atakuwa ameshaanza kutumia dawa kupitia CTC.

Kumbuka maambukuzi ya mtoto hutokea akiwa tumboni( kabla mtoto kuzaliwa wakati wa mimba), pia hutokea wakati wa kujifungua na kunyonyesha.

Dawa za ARV zikitumiwa kwa usahihi na wakati muafaka husaidia kufubaza virusi, kupunguza viral load na kuongeza kinga ya mwili.

Pia wakati kichanga kinazaliwa kinapewa dawa za ARV na dawa za kuzuia magonjwa nyemelezi.

Jitihada zote hizo zikifanyika mtoto atazaliwa bila na maambukizi.
PMTCT=Prevention of mother-to-child transmission
 
So ni kwamba anazaliwa akiwa Hana maambukizi kabisa? Au hiyo program inasaidia kufubaza virusi WA Mtoto husika?
 
Kuna program inaitwa PMTCT( prevention to mother and child transmission).

Mama akipima afya akiwa na maambukuzi ya HIV ataanzishiwa dawa, au atakuwa ameshaanza kutumia dawa kupitia CTC.

Kumbuka maambukuzi ya mtoto hutokea akiwa tumboni( kabla mtoto kuzaliwa wakati wa mimba), pia hutokea wakati wa kujifungua na kunyonyesha.

Dawa za ARV zikitumiwa kwa usahihi na wakati muafaka husaidia kufubaza virusi, kupunguza viral load na kuongeza kinga ya mwili.

Pia wakati kichanga kinazaliwa kinapewa dawa za ARV na dawa za kuzuia magonjwa nyemelezi.

Jitihada zote hizo zikifanyika mtoto atazaliwa bila na maambukizi.
Asante kwa kunisaidia chief.
Bilashaka LIKUD amepata majibu mujarab kabisa
 
Si kweli.
Mama mwenye maambukiz ya VVU ananyonyesha vizuri tu, bila shida yoyote na mtoto hapati maambukizi.
Ila ni miezi sita , na sio zaidi ya hapo.kwani baada ya hapo haishauliwi kwani akianza kuota meno, anaweza akang'ata chuchu za mama na kuweza kupata maambukizi, kupitia damu.
 
Back
Top Bottom