Hivi ni kweli vilikuwa vita vya Dunia kama tunavyoaminishwa?

DALA

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
2,212
4,517
Wakuu salaam!

Naomba kuelimishwa. Kwanini tunaviita vita vilivyopiganwa huko nyuma vya dunia wakati moja kwa moja vilikuwa kati ya mataifa makubwa? Afrika au mataifa ya kiafrika iligombana na mataifa gani zaidi ya wanaume kuandikishwa kwenda kupigana upande wa Ujerumani au Uingereza na mataifa mengine ya huko Ulaya?

Kwanini viitwe vita vya dunia? Yaani wazungu ndo dunia peke au?

Naomba kuelimishwa.

Uzi tayari.
 
Ni kama wanavyosema Tanzania ilitawaliwa na wakoloni ili hali kule kwetu kilimajaro hakukuwa na ukoloni wowote, watu walikuwa huru kufanya shughuli zao, hakuna kufanyishwa kazi za shurti au kukamatwa na kupelekwa kuuzwa.

Sasa inamaana historia inapindishwa?
 
ntaongezea tu kuwa
hizo ni symbol za mzungu ili imjengee mweusi kifikra kuwa mzungu ni wa hatari kuliko mweusi.

kuna muda huwa najiuliza watoto wanasomaga namba za kiarabu na za kirumi shule za msingi ila kwa upofu wetu mpk leo hatuhoji kwanini? hii ni dhahiri bado tunatawaliwa.
 
Kuna mambo mengi ya kijinga tumeaminishwa ikiwa ni pamoja na mijitu eti inakuja Tanzania kutokea Ulaya alafu anaivumbua mlima Kilimanjaro!
 
Wakuu salaam!

Naomba kuelimishwa. Kwanini tunaviita vita vilivyopiganwa huko nyuma vya dunia wakati moja kwa moja vilikuwa kati ya mataifa makubwa? Afrika au mataifa ya kiafrika iligombana na mataifa gani zaidi ya wanaume kuandikishwa kwenda kupigana upande wa Ujerumani au Uingereza na mataifa mengine ya huko Ulaya?

Kwanini viitwe vita vya dunia? Yaani wazungu ndo dunia peke au?

Naomba kuelimishwa.

Uzi tayari.
Mataifa yetu bado yako mapiganoni. Njaa, ujinga, magonjwa, ukibaraka bado vinatusumbua.

Tanzania 🇹🇿 na wingi wa misitu yake bado madawati ni shida chini ya utawala dhalimu na batili wa CCM
 
Wazungu wanatambua kule kwao ndio Duniani.

Ndio maana hata sisi watawala wetu hawajisikii amani kukaa hapa mpaka waende huko Duniani.
 
Wakuu salaam!

Naomba kuelimishwa. Kwanini tunaviita vita vilivyopiganwa huko nyuma vya dunia wakati moja kwa moja vilikuwa kati ya mataifa makubwa? Afrika au mataifa ya kiafrika iligombana na mataifa gani zaidi ya wanaume kuandikishwa kwenda kupigana upande wa Ujerumani au Uingereza na mataifa mengine ya huko Ulaya?

Kwanini viitwe vita vya dunia? Yaani wazungu ndo dunia peke au?

Naomba kuelimishwa.

Uzi tayari.
Kwasababu nchi nyingi zilishiriki kwakuwa zilikuwa makoloni ya hao mabeberu, mfano askari wengi tu kutoka Tanganyika nao walienda pigana vita
 
Weww Jamaa jishughulishe kusoma historia angalau kidogo...Hapa Tanganyika pia vita ilikuwepo
 
Kwasababu nchi nyingi zilishiriki kwakuwa zilikuwa makoloni ya hao mabeberu, mfano askari wengi tu kutoka Tanganyika nao walienda pigana vita

Lakini havifanyi vita hivyo kuwa vya dunia. Hatukushiriki kwa hiari na wala hatukua na mgogoro wa moja kwa moja na hayo mataifa yaliyokuwa yanapigana
 
Waliopigana Vita ndiyo walimiliki dunia nzima kwa kila kitu kwa kipindi hicho, 'majority' Kama sisi waafrika tulibakiwa na pumzi tu kutoka kwa Muumba,vilivyobaki vyote vilimilikiwa na hao waliopigana vita,kwahiyo Basi kwa kuwa wao walimiliki dunia nzima Basi jina zuri la Vita tena lenye utamu ni VITA YA DUNIA kwasababu waliopigana ndiyo walikua wakimiliki dunia..mf.unafanya kazi serikalini au kwenye kampuni,unaweza kusema kweli kuwa hii ni kampuni yao na siyo kampuni yetu?,ijapokuwa ww binafsi huna umiliki hata wa asilimia 0.1 wa kampuni...
 
Lakini havifanyi vita hivyo kuwa vya dunia. Hatukushiriki kwa hiari na wala hatukua na mgogoro wa moja kwa moja na hayo mataifa yaliyokuwa yanapigana
Hata vita ya Ukraine kuna watu ambao hawataki hivyo vita wanashiriki tu kwa lazima, sasa kipindi hicho nchi zetu zilikuwa makoloni yao mtawala akasema twende vitani ndo tukashiriki hivyo.
Mkuu kwani uwa bungeni wakiwa wanapitisha sheria wewe unashirikishwa?
 
Vita vilipaganwa pia Africa na inakadiriwa wanajeshi wa kiafrika milioni 1 walishiriki katika vita hivyo.
Ethiopia ilishiriki vita hivyo ikiwa haiko chini ya occupation ya Italy.South Africa iliingia upande wa allies mwaka 1939.Nchi za Asia zilishiriki pia mshiriki mkubwa akiwa India.
Kama Nchi hizo ziliingia kwa kulazimishwa au kama makoloni haikuwa swali lako.Na assume ni swali sio ligi?
Ila kama unataka kuleta mada nyingine uko huru kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom