Hivi ni kweli umasikini umepungua Tanzania?

Ruyama

JF-Expert Member
Sep 6, 2019
367
561
Nikirejea maana ya POVERTY-lack of afford the basic needs such as clothes, food and shelter.
Leo hii mishahara haijaongezwa,jee itawezekana mtumishi kununua nguo mpya yeye na watoto na mke?jee mili mitatu inaliwa kikamilifu,jee ataweza kulipa kodi kwa wakati?
Sio vizuri kusema umasikini umepungua ili hali maisha ni magumu vitu bei juu
 
Yeah umepunguwa kwa wapiga deal waliokuwa wamekabwa koo kwa miaka 5 ya jiwe!😅

Sahizi wanaandaa warsha na semina nyingi tu na kujiandikia safari!

C25BA32B-D8B5-43ED-87A5-80A710F362AC.jpeg
 
Umasikini wa fikra umepungua. Leo hii mwanasiasa hawezi kudanganya zaidi ya 25% ya watanzania.

Ila umasikini wa uchumi umeongezeka. Hali ni mbaya. Watanzania wachache sana wameuaga umasikini wa kiuchumi ni kama 5%, tuliobaki tunabangaiza tu.
 
Ufukara mtaani uko juu sana. Achana na hao watumishi angalau wanaweza pata hayo mahitaji ya msingi, watu wa kawaida mtaani wana hali mbaya sana.
Kuna kundi kubwa sana la walalahoi aisee.
 
Kama wafanyakazi ndo middle class ambao tulitarajia wawe na maisha standard, ndo hao wako hoi hadi mshahara hauwezi kukutana na mwingine na wengi wana zero saving kwenye akaunti zao zaidi ya kukatwa mikopo na vikoba. Je, wale kajamba nani huko maeneo ya vijijini na mijini hali zao zikoje............usiwasikilize sana wanasihasa uchwara wa bongolala, wanaongea vitu visivyo na uhalisia...
 
siyo kweli, hapa kila mtu ananunua sukari robo mafuta ya kula mtu kajitahidi amenunua ya buku., sembe wengi ni nusu kilo.
 
Nikirejea maana ya POVERTY-lack of afford the basic needs such as clothes, food and shelter.
Leo hii mishahara haijaongezwa,jee itawezekana mtumishi kununua nguo mpya yeye na watoto na mke?jee mili mitatu inaliwa kikamilifu,jee ataweza kulipa kodi kwa wakati?
Sio vizuri kusema umasikini umepungua ili hali maisha ni magumu vitu bei juu
Yeah, umepungua kwa kuongezeka! Unaijua hii falsafa?
 
kwenye makaratasi umasikini umepungua sana maana tuko uchumi wa kati sasa hivi kila sehemu kuna viwanda vinavyolipa Kodi na tozo Tanzania mpaka kisababisha mabadiliko ya tabia ya nchi maji yamepungua kusababisa umeme wa mgao
 
Nikirejea maana ya POVERTY-lack of afford the basic needs such as clothes, food and shelter.
Leo hii mishahara haijaongezwa,jee itawezekana mtumishi kununua nguo mpya yeye na watoto na mke?jee mili mitatu inaliwa kikamilifu,jee ataweza kulipa kodi kwa wakati?
Sio vizuri kusema umasikini umepungua ili hali maisha ni magumu vitu bei juu
🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔😝😝😝😝😝Utaambiwa weye kazi yako ni kupinga kila kitu.Be aware of hypocrites!
 
Ninachofahamu mimi umasikini umepungua kwa ndugu na jamaa wa mama samia...mfano ni mkwe wake bwana Mohammed mchengerwa na wengineo waliokula shavu...
 
Back
Top Bottom