Hivi ni kweli TRA kwa gari kama hii wanabeba milioni 30 zao??

Agera 1

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
4,080
4,217
Habari ya humu ...msaada kidogo kuna site nilikuwa napitia nikakuta suzuki kei afu CIF had Dar ni milion tatu na laki mbili ....

Na kuna mtu alituma link ya calculator ya TRA humu nikafungua nikajaza ikaja kodi ya milion tatu na laki tano hivi jumla ni milion saba na kitu ambapo pale wameendika hadi registration fee ....naomba kuuliza je ni kweli ndo hvyo au kuna additional cost sababu kila gari nikiangalia inakuja bei nafuu zaidi kuliko kununua hapa hapa bongo zikiwa imported from japan as niliangalia rav 4 2004 ikaja mil 9 had bandarini na mil 9 kodi jumla ni 18 na kitu

Jingne kuna prado generation ya nne nazipenda sana haswa upate diesel 2.8L 1GD FTV ...hizi zimeanza 2009 siti ni saba zile mbili za nyuma kuna button ukibonyeza zinazama ndani ya floor kwa kweli ni nzuri sana ku compare na hizi generation ya tatu ...maana zenyewe naziona bei yake huwa ni 52m unapata namba D kabisa lakini generation ya nne ya mwaka 2013 used niliona ni 120m ...ila kwa calculator ya TRA kodi ilikuja milion 30 plus CIF had dar ni milioni 59 jumla ikaja 89milion

Hivi ni kweli TRA kwa gari kama hiyo wanabeba milion 30 zao??
 
Gari anasa kaka, sishangai, pole, ila tafuta gari la uwezo wako na sio kama wanunua nyumba mkuu, whats important is moving from point A to B. Kubeba mizigo kodisha, jithamini kama waweza kuligharamia
 
Kodi ya tractor marsey fargason ni bei gani?


Sasa mleta hoja hapa kama unasema ulishaangalia hiyo calculator ya TRA na imekupa majibu ya bei ,sasa unataka nini tena?wewe jipange kulingana na uwezo wako na nawapongeza TRA kwa kuweka uwazi ili mtu ujipange kulingana na uwezo.
 
afu ww sijui ndo invisible .....acheni ushamba mbna site za wenzenu hawafanyi hvyo mambo ya kipuuzi mna edit thread ili nini
 
Kwakweli ile calculator na gharama halisi za kodi wanazokuja kuzitaja bandarini gari ikifika havina uhusiano. We jipange vizuri tu mkuu. Usije ukajikuta kwenye listi ya Mama Kevela wa YONO
 
Nimeshangaa kwanini ushuru haujawa 120m kama bei ya kununulia. maana bei ulonunulia gari ndo ushuru wake. sijui hii system imekaaje :D
 
Back
Top Bottom