Hivi ni kweli tipa ilikufa yenyewe haikuhujumiwa?

gforum

Member
Feb 26, 2012
61
6
Jana nilikuwa na angalia kipindi cha KIPIMA JOTO kinachorushwa na ITV kila Ijumaa, nilishangaa kusikia kutoka kwa mwakilishi Wa tasisi moja ya Serikali inayoshughulika na maswala ya mafuta akisema bila haibu ETI TIPA YA KIGAMBONI iliyokuwa inasafisha mafuta ya PETROLI ilikufa yenyewe kutokana na hesabu zake kuonyesha kiwanda kilikuwa kinaendeshwa kwa hasara na kwamba kilishidwa kushindana na Mafuta yaliyokuwa yanaingwizwa kutoka nje ya nchi yakiwa yamesafishwa.
Na sababu ni kwamba TANZANIA HAINA MATUMIZI YA MAFUTA KIASI CHA KUTOSHELEZA KUWA NA KIWANDA CHA KUSAFISHIA.
Binafsi nashangaa kwa kauli hii kwa sababu Tanzania ina watu wengi sana (KARIBU 40,000,000) na matumizi ya mafuta ni mengi pia,
USHAHIDI WA HILI NI KWAMBA JIRANI ZETU ZAMBIA WANA watu 12,000,000 na wana kiwanda cha kusafishia mafuta NDOLA AMBACHO PIA MAFUTA GAFI YAKE YANAPITA TANZANIA KWA BOMBA LA TAZAMA.
NA HATA HIVYO KIWANDA HICHO HAKIJATOSHELEZA ZAMBIA BADO WANAAGIZA MAFUTA YALIYOSAFISHWA NJE. KULIKONI WATANZANIA TUSEME TIPA ILIKUWA INAJIENDESHA KWA HASARA? JE KINGEKUWA KINAFANYA KAZI HATA ZAMBIA WANGENUNUA MAFUTA KWETU KWANI BADO WANA AGIZA NJE? VIPI CONGO, BURUNDI, RWANDA NA MALAWI ambao wote wanapitisha mafuta yao Tanzania? LABDA MIMI SI ELEWI NAOMBA WADAU MNISAIDIE TUITETEE TIPA NA SEKTA YA MAFUTA, JOMBAA MAFUTA NI MUHIMU NA BEI INAPANDA KILA KUKICHA, AU?
 
Boss hiyo iachage tu!mie hata huwa nashindwa jua hawa wakulu-kina "mjuzi wa ukoo " huwa wanapataje usingizi baada ya kutenda dhambi kama hii.

TIPER ilihujumiwa! Ndo hata mambo tunasema ukiwa Maskini uwe na power of negotiation - wazungu na ORYX,na mawaziri waroho ndo waliiuwa TIPER,Motel Agip, na mtambo wa lami (hizi zote zilikuwa zinamilikiwa na Govt of Tanzania na Agip then ORYX) kazi ya waitaliano hao..!
 
Mkuu, kama unajua hata Zambia licha ya kuwa na refinery bado wanaaaagiza white product basi ujue kuna mambo mengi ya kuangalia kuwa na refinery za kizamani kuna hasara gani. Nitakutafutia barua ya IMF kuhusu kufunga Tiper.
 
Back
Top Bottom