Hivi ni kweli Tanzania (Tanganyika wakati ule) ilipata uhuru mwaka 1961?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,396
6,538
Historia inasema kuwa Tanzania (Tanganyika enzi hizo) ilipata uhuru tarehe 9 Desemba 1961, na waziri mkuu alikuwa hayati Mwalimu Nyerere. Halafu tarehe 9 Desemba 1962 Tanzania (Tanganyika enzi hizo) ikawa Republic na Rais kuwa hayati Mwalimu Nyerere.

Sasa tuangalie maana ya maneno 'uhuru', 'republic', 'waziri mkuu', na 'Rais'. Republic means a country without a king or queen, usually governed by elected representatives of the people and a president. Independence means freedom from being governed or ruled by another country. President means the person who has the highest political position in a country that is a republic, and who in some of these countries is the leader of the government. Prime minister is the leader of the government in some countries (source: Cambridge advanced learner's dictionary 4th ed).

Swali: kwa kipindi cha mwaka mmoja (miezi kumi na mbili) yaani kutoka 9/12/1961 mpaka 9/12/1962 hayati Nyerere akiwa waziri mkuu nani alikuwa mkuu wa nchi ukizingatia Tanzania (Tanganyika wakati ule) haikuwa Republic? Na wakati huo alikuwa anajibu kwa nani aliyekuwa juu yake kabla ya kuwa Republic?

Watanzania wenzangu tuzungumze hapa juu ya jambo hili.
 
Back
Top Bottom