Hivi ni kweli Slaa alipata kura hizi Karatu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kweli Slaa alipata kura hizi Karatu?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kiresua, Nov 7, 2010.

 1. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2010
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  nimekuwa nikifuatilia hesabu za kura katika jimbo la Karatu, Kwenye website ya Tume ya Uchaguzi hakuna jimbo la Karatu lakini Kwenye Mwananchi Dr. Slaa alipata kura 147 (0.2%) Jk alipata kura 24,382 (98.1%). Matokeo ya Ubunge Dr. Lorry ccm alipata kura 26,281, na Israeli Chadema alipata kura 41,132. Ukiangalia matokeo ya Ubunge na Uraisi utaona kuwa tofauti kubwa ya wapigakura,
  Je haya ni makosa yangu kuangalia, makosa ya gezeti kuachapisha, au ni makosa ya TUME, au ni matokeo halisi

  wanajamii nisaidieni kama kuna mwenye data za uhakika
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Malaria Sugu
   
 3. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2010
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Kuna Mtu ameandika Malaria Sugu hapa, I dont knw what does this mean? please give me breack! Niliona habari juu ya kupuuza Malaria Sugu no Idea what does this mean and who ar you talking about.
   
 4. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  haya nayo makubwa
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  i think bila hata kutumia logic ni vigumu Dr Slaa kupata less than 50% Karatu... ni sawa na JK kupata 40 ukwereni
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Nov 7, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Is not clarified yet? what happened? wanachadema vipi? this was honesty question!
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  jk 24,36435.08%slaa 43,13762.10%
  source nec
   
 8. G

  Galilee Galileo Member

  #8
  Nov 7, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wanalazimisha watanzania kutwaa nchi kwa nguvu ila ole wao siku zinakuja ule mtindo wa kuchezea wazanzibar kuwanyang'anya kura CUF na kulazimisha CCM kushinda hata kama imeshindwa hautafanya kazi Tanzania Bara
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  hapo tena watasema wewe mchonganishi
   
 10. G

  Galilee Galileo Member

  #10
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ng'wanangwa siku zinakuja hapa si uchonganishi ni ukweli kwanza CCM walikuja na hila zao kuwa CHADEMA ni chama cha kikabila lakini kimewaprove wrong kwa kutwaa ubunge kila kona ya nchi isingekuwa uchakachuaji kingepata majimbo si chini ya 80 yakiwamo majimbo ya Kigoma mjini, Sumbawanga, Shinyanga mjini, Kishapu, Buchosa, Karagwe, Ulanga Magharibi, Segerea, Kigamboni, Mbeya vijijini, Mpanda, Tarime, Geita, Busanda, njombe, chunya na kwingineko kwingi

  Halafu pia CCM wajiulize kuwa iwapo wasukuma ni kabila kubwa ambao huwa ni wapole na hawana makuu lakini safari hii Sukumaland imekabidhiwa upinzani katika majimbo ya Nyamagana, Ilelema, Maswa Magharibi, Maswa Mashariki, Meatu, Bariadi magharibi (UDP) Biharamulo Magharibi na Bukombe ambayo ni ya wasumbwa jamii iliyomegeka toka kwa Wasukuma wao na Wadakama ni kama kusema muingereza (Englishman) na muayalendi (Irishman) na bado CCM wakachakachua majimbo mengine manne ya Sukumaland ambayo yalikuwa yamenyakuliwa na upinzani majimbo haya ni pamoja na Shinyanga Mjini, Geita, Kishapu na Busanda basi wajue sasa nchi imeamka kama kabila lenye idadi nyingi ya watu ambalo halina makuu limeona CCM haifai hakuna atakayesimamisha hili wimbi la mageuzi CCM watake wasitake siku zao zinahesabika

  Naomba nieleweke hapa siongelei ukabila ila najadili kwa kina hali halisi ya nchi ya Tanzania
   
Loading...