Musundi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 1,583
- 2,600
Mwenzenu niko njia panda kabisa hata sijui lipi ni lipi sasa. Toka utotoni nilizoea kusikia msemo huu na niliamini huo ndo ukweli maana siamini Mungu anaweza kumpenda Msema-uongo
Na hata sasa msemo huu bado umetamalaki.
LAKINI mbona kivitendo tunafanya kinyume chake kabisa?!! Au zama hizi kuna wanaoruhusiwa kusema ukweli na wengine kusema ukweli ni haramu?
Nimeshangaa kukuta taarifa huko TWITTER ati jalada limefunguliwa kwa ajili kuwashtaki wanaosambaza picha mitandaoni za vitabu vilivyochapishwa vikiwa na makosa.
Labda nasumbuliwa na ujinga wa kutojua sheria. Lakini najiuliza tu: Hizi picha ni za kweli au wanaozisambaza wamezusha tu uongo kwa nia ovu? Kama ni za kweli mchapishaji alikosea, anayejaribu kulionesha kosa hilo ana hatia gani? Sio MSEMA-KWELI huyu?
Naomba kuelimishwa na wajuzi wa sheria.