Hivi ni kweli migomo vyuo vikuu suluhisho lake ni mabomu ya machozi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kweli migomo vyuo vikuu suluhisho lake ni mabomu ya machozi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nhunda, Feb 4, 2011.

 1. N

  Nhunda Member

  #1
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wa na jamii imefikia kipindi tujiulize njia stahiki za kutatua matatizo ya migomo katika vyuo vikuu vyetu, kuwapiga mabomu ya machozi wanafunzi wanapo taka suluhu ya matatizo yao sinauhakika kama ni njia harisi na halali kwa kutatua matatizo yao. Kwanza kabisa tunapo wapiga mabomu lazima tujiulize nini gharama ya machozi yao, pia ni lazima tujue ni kwakiasi gani wanaongezewa maumivu, kwasababu tayari wanamaumivu ya matatizo halafu wanatwikwa mzigo mwingine wa mabomu ya machozi. Je hivi nikweli wana JF suluhisho la migomo vyuo vikuu ni mabomu ya machozi?
   
 2. mawazoyangu

  mawazoyangu JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 327
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Ndio njia pekee ya kuwaambia wanachuo na wananchi kuwa hatutaki kuwasikiliza. kwanza watoto wa wakubwa wengi hawapo hapa vyuo vya tanzania. Wale waliopo hawashiriki migomo kwa kuwa wanapewa fedha na hao mafisadi.
  Nakumbbuka vizuri maandamo ya 2004 yaliyofanywa na UDSM kupinga kuanzishwa kwa bodi ya mikopo lengo likiwa ni kuondoa ubaguzi ambao wanauita "madaraja ya mikopo" Walipiga sana mabomu, polisi wakaiba sana simu za mikononi za wanafunzi lakini polisi hao hao leo hawawezi kusomesha watoto wao vyuo vikuu, wamekuwa kama maroboti wanafanya kila wanaloambiwa hata kama linapingana na katiba ya nchi "maandamano"
  Naomba itokee siku ya Tunisia na Misri yatokee tanzania, mm nitakuwa mstari wa mbele. Fedha za kulipa dowans zipo lakini za kukopesha wanafunzi ambazo ni MKOPO na zitrudishwa hazipo!!! uchizi huo
   
 3. t

  the mkerewe JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndio manake wanaleta siasa za CDM (fujofujo) kwani shida vyuoni zimeanza leo mbona huko nyuma haikuwa hivi migomo kwa wingi kama sio kudanganywa na SLAA?

  PIGA HAO WAENDE WAKASHAKI KWA SLAA
   
 4. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  the mkerewe, nadhani hujui unachochangia 1.unatakiwa kujua kuandamana ni haki ya msingi/kikatiba ya mwananchi yeyote kama njia mojawapo ya kuadai haki yake au kupinga hali eg.kulipa dowans,mambo ya IPL,EPA n.k 2.serikali au polisi kupiga mabomu au kubugudhi raia/watu waliokusanyika pamoja bila kufanya fujo ni kuingilia uhuru wa kikatiba(ref:right to assemble) 3.tz ni nchi ya vyama vingi ambavyo jukumu la msingi(primary objective) la kila chama cha siasa ni kuchukua uongozi wa nchi-na hili ni kupitia kwa kunadi sera za chama husika kwa wananchi na hapo tegemea sera tofauti kutoka kwa kila chama,kwa maantiki hiyo basi CDM kama chama cha siasa hakileti fujo kama unavyofikiri ila wanajitahidi kunadi sera tofauti na CCM,CUF,UDP,TLPn.k ili wachaguliwe lakn sababu watu wenye mtazamo kama wa kwako wa kudhan kila kitu wanaweza wao na ukipingana nao inakua nongwa wana supress ile haki ya vyama vya siasa. 4.hapo nyuma migomo haikuwepo ingawa matatizo yalikuwepo sbb wanafunzi walijua hali ya kifedha ya serikali labda si mzuri unlike now hela ya kulipwa dowans ipo tena ilipwe haraka iwekanavyo lakn hela ya kusomesha wanafunzi less than ya dowans haipo 5.slaa sio muongo kama unavvyofikiria hayo unayofikiri hayawezekan ni kwamba yanawezekana kama kuna proper means ya ku-allocate resources za nchi na good scale of preference.
   
 5. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwani wamepigwa mabomu leo??
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  usitumie makalio kuwaza. tumia ubongo.
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo unataka kusema kabla ya Chadema kuanzishwa hapakuwa ni migomo vyuoni?
  Jamani sio lazima kila mada uchangie, kama huna point kuwa msomaji tuu.
   
 8. K

  KOPLO MAJAKA New Member

  #8
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unacharazwa nini, au na wewe ni polisi. Asilimia kubwa ni std 7 na form 4 zero div. Na watoto wenu hamuwezi hata
  kuwasomesha univarsity. Bata jike we.
   
 9. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Sina hakika kama we ni mtanzania.!!!!!!!!!!!!!
   
 10. M

  Mmongolilomo Senior Member

  #10
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kimsingi ndani ya Vyuo vyote vikuu kuna matatizo makubwa na ya Msingi ambayo pengine hayataki ama hawataki kuyaweka wazi. Kuna ukosefu mkubwa wa sehemu za malazi kwa wanafunzi, kutozingatia vigezo vya utoaji mikopo, Uhaba wa Wahadhiri na nafasi za kufundishia, pesa ndogo ya kujikimu. Ssa ukichanganya na ubovu wa uongozi wetu basi tunachochea vurugu ambazo watawala hawazitaki kwani zinakuwa kero badala ya mwongozo katika utatuzi wa tatizo husika...... :A S crown-1:
   
 11. R

  Ralph Nicholz Member

  #11
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Heeeeeeeeeeeeeeee, katoka wapi huyu!??
   
Loading...