Hivi ni kweli mheshimiwa rais ana nia ya kuwachukulia hatua mawaziri wezi wa mali za umma? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kweli mheshimiwa rais ana nia ya kuwachukulia hatua mawaziri wezi wa mali za umma?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtumishi Wetu, May 2, 2012.

 1. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Ni muda sasa umepita tangu bunge letu tukufu limalizike kwa kumtaka waziri mkuu ajiudhuru au mawaziri waliotajwa kwenye riporti ya CAG wajiudhuru!!!!
  Kwanza jambo la kusikitisha Mheshimiwa Raisi hali akijua kuwa kuna sakata linalomtaka PM ajiudhuru, yeye huyo akaenda majuu Latin America kukagua mashamba ya nyanya!!!!!
  Baada ya kurudi moto ukiwa bado unawaka yeye huyo kwenye mazishi ya Merehemu Raisi wa Malawi, kama vile anakwepa kitu fulani vile!!!
  Si mnajua tena kama kuna shida nyumbani au watu wanakusubiri kwa jambo fulani na wewe bado hujawa tayari, utapita kwa jirani au mahali ili upitishe muda watu hao waondoke ndio urudi nyumbani kupata taarifa zao kwa mama!!!
  Hiyo ni delaying tactic watasubiri mwisho watachoka, hapo ni kwamba nia thabiti ya kufanya jambo muhimu hakuna!!!!!!!!!
  Kama ni kweli unataka kumchukulia mtu hatua tena umeambiwa ni mwizi, lazima kwanza umtoe ofisini tena kwa ghafla, hapo utakuwa na uhuru wa kupekua kitu kimoja kimoja mpaka upate ushahidi wa kitu unachotafuta!!!!
  Sasa unapompa mkuu kwenye ofisi muda huku kukiwa na vitisho vya kufukuzwa kazi, wewe ukamuacha pale unategemea nini????
  Eti kwenye hotuba mkuu anasema ripoti ya CAG iwe wazi hivyo ana maana gani kwani hiyo ripoti CAG ataleta kwenye tume za bunge ripoti isiyokuwa wazi??????
  Kama ripoti zimefikishwa bungeni na wabunge wamejihakikishia kuwa ni sawa huo wizi umefanyika bila kujali ilichukua muda gani kufanyika inatakiwa hatua ya haraka kuchukuliwa ili kuokoa maeneo mengine mapya yasifanyiwe wizi!!!
  Ni lazima wahusika wa wizi wasimamishwe kazi ili uchunguzi huru ufanyike, uchunguzi utafanyika vipi wakubwa wakiwa bado maofisini????
  Nia thabiti ya kuokoa fedha za Watanzania zisiendelee kuibiwa haipo mimi hilo naliona sijui wenzangu mnasemaje kuhusu hili?????
   
 2. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Hao mawaziri na wakubwa walioachwa maofisini huku wakiwa na tuhuma za wizi unategemea hivi sasa wanafanya nini, hili ni janga la kitaifa na hasara kubwa sijui matokeo yake ni nini ??????

   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Aanze kwanza va wezi wa EPA ndo tutamuelewa otherwise,
  hizo zinazoibiwa sasa sina mikono ya hao hao wezi wa EPA
  NA ccm IMEFAIDIKA NAZO PIA ktk uchaguzi wa 2010 na 2010.
   
 4. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Kikwete ni msanii, jana mlimsikia anasupport wabunge, tena kama mkuu wa nchi aliyepelekewa taarifa na mwenye wajibu wa kuwawajibisha wezi hao alifanya nini? Anasupport wabunge? Si mtaona! Nia yake ni kuonekana mwema kwa kila mtu... Hana nia ya kuwashughulikia
   
 5. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kwani we hadi sasa hujazizowea tu ngonjera za mheshimiwa? 'Mosi' ilikuwa lini ili leo iwe 'pili'? Hapo ni nguvu ya umma tu ndo italeta mabadiliko. Tujipange tu, 2015 sio mbali.
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  yeye mwenyewe ni Mwizi atawezaje kuwawajibisha wezi wenzie?
   
 7. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Hiyo ni kweli Mkuu huyu Bwana anapaka chama chake rangi mbele za watu, lakini achunge Mtanzania wa leo sio mjinga wa kupewa ahadi hewa kama zamani!!! Hizo hila na propoganda za chama yatamtokea puani!!!!!!!!!!

   
 8. T

  Tata JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Huu ni upepo mbaya tu anasubiri upite ili afanye maamuzi upepo ukiwa mzuri kiasi.
   
 9. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo anawapa muda wezi waendelee kusafisha ofisi zao na kufilisi, je tutakuta kitu kweli???? Kweli hapo Mheshimiwa Raisi anayo mapenzi ya dhati kwa nchi yetu ya Tanzania na watu waliomuweka madarakani?????

   
 10. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mkuu tutangoja hadi 2015 lakini nchi inazidi kufilisiwa na hawa wezi, ni bora basi kuwe na stop gap ili tulinde kile tulicho nacho!!!! Njia sahihi ni kuchukua hatua ya umma wote wa Tanzania tukatae dhuluma kwa fedha na mali zetu!!!!!!

   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  May 2, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hayo matokeo yake nadhani jk ndo alikuwa akiyataka!
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  May 2, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli mkuu kwani njiwa wa jamii moja huruka pamoja
   
 13. j

  jjjj Senior Member

  #13
  May 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  jk ni msanii
   
 14. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #14
  May 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mkuu usanii nao si una mwisho wake, watu sasa wamechoka usanii wanapiga mahesabu wafanye nini!!!!!!

   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  "Sikukasirishwa na wala kufedheheka na mjadala ule, nilifurahia ripoti kujadiliwa kwa uwazi. Tatizo watu wanasahau mapema. Mimi ndiye niliyeamua ripoti hii ya CAG ijadiliwe kwa uwazi bungeni tangu mwaka 2007. Nilifikia uamuzi huo baada ya kuona wapo baadhi ya watu ambao ni mchwa wanaokula fedha za umma."

  Kikwete
   
 16. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #16
  May 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Kama kweli Mkuu alifurahia ripoti ya CAG kuweka wazi wezi wa mali za umma, basi awachukulie hatua aache dally dally na usanii!!!! Watu wanateseka mitaani hawataki tena siasa za maji taka!!!!!

   
 17. S

  SokoroDar Member

  #17
  May 2, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Angemalizia hivi " na tangu 2007 mimi ndiyo niliyoamua wezi wote waachwe na wasishitakiwe maana pesa wanazochukua ni vijisenti tuh !"
   
 18. v

  vutakamba Senior Member

  #18
  May 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 199
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  unafiki wa watawala ndio uliotufikisha hapa tulipo leo. Mawaziri na watendaji wengine hawawezi kuwa mafisadi ukamuacha mkuu pembeni. Anajaribu kujikosha bure. Watanzania tunatakiwa kutomwonea huruma mtu anayeteua na kusimamia mfumo wa wezi ktk nchi. na kutunyima maendeleo. Tunapaswa kuendelea kukataa, maneno matamu yamepitwa na wakati. Sharti wawajibishwe.
   
 19. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #19
  May 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Huo Mkuu ndio ukweli Watanzania lazima tutafute njia mbadala ya kuondoa wezi hawa MADARAKANI!!! Muda wowote wanaokaa maofisini wana plan kuendelea kuiba hawana mpango wowote kuleta maendeleo kwa nchi hii!!!!
  Lazima tutafute solutions za ukombozi wa nchi yetu, maana serikali hii ya CCM imeshindwa kabisa haina jipya ni wizi tuu!!!!

   
Loading...