Hivi ni kweli mh. Freeman mbowe na dr. Slaa ni madikteta?

milimo

Member
Nov 29, 2012
61
32
Kama ni kweli Mh. Mbowe na Dr. Slaa ni madikteta nawapa kongole. Maana udikteta wao unafaida sana. Udiktea wao usingekua na faida nadhani chadema isingefika ilipofika sasa na kuwa chama tishio kwa chama tawala ccm. Udikteta wao umekiimarisha chama na kuwa chama mbadala kinachosubiri kuingia ikulu.

Umekifanya chama ambacho kinapendwa na wanyonge (hivi chama kinachongozwa na dikteata mbaya kitapendwa na wanyonge?). Mh. Mbowe na Dr. Slaa mkiwakilisha uongozi wa juu wa chadema, ili tuwamini na kuwapa nchi 2015, msiogope kuwa madikteta wa kusimamia maamuzi ya chama na baadaye ya nchi.

Tuseme kweli, hivi kuna nchi yeyote duniani imendelea bila ya kiongozi wake kuwa na vitabia vya kidikteta; haiwezekani asilani. Hivi utavuna mazao ya shamba kwa kucheka na ngedere wanaokula mavuno. Mfano; unapanga kuendeleza vikundi vidogo vidogo vya wajasiliamali wadogo kwa kutenga mfuko unaoitwa mapesa ya mheshimiwa, halafu wajanja wachache wanakula hizo pesa bila kuwafikia walengwa na wewe unacheka nao, maendeleo yatakuwepo?

Unanapanga mipango ya maendeleo ya kijani (kilimo) unatoa ruzuku kwenye zana za kilimo (kama mboleo) halafu wajanja wachache wanajinuifaisha bila hizo zana kuwafikia walengwa (wakulima) halafu wewe unacheka cheka nao, maendeleo yatakuja? Unanzisha mjadala wa kuwavua gamba mnaowaita mafisadi halafu baadaye mnasema chama kitayumba mkiwavua gamba, kweli kwa staili hiyo nchi itasonga mbele? Ili kupata maendeleo ni lazima kiongozi awe na vitabia vya kidikteta, ambaye ni muumuni mzuri wa mungu (dini yeyote). Mwenye huruma na watu wake, mwenye upendo kwa anaowaongoza, msikivu lakini anayetoa maamuzi na kusimimia maamuzi yake, asiyeogopa kulaumiwa kwa maamuzi yake kwa manufaa ya nchi n.k. Hivi vyote vinahitaji tabia ya kaudikteta hivi.

Ili chama kibaki na heshima yake, chadema fanyeni maamuzi magumu kwenye huu upepo unaopita. Safisheni chama muda huu, na chadema hakiwezi kufa kwa mtu mmoja kufukuzwa kwa kuyumbisha harakati za kuipumzisha ccm,hivi hawa vijana mbona walikua na ‘future' nzuri sana. Wametuonyesha kwamba sio wavumilivu hawa ndio madikteta hatari wa siku za mbele. Maana dikteta mbaya ni yule asiyekuwa na subira, anayetaka kuongoza kwa njia yeyote hata kama ni haramu. Tunajua akina dr. Slaa kuna siku nao watapumzika muda muafaka ukifika (kwa sasa bado tunawahitaji), kwa nini hao vijana wasingendelea kujijenga taratibu na kuvuta subira? Wanakimbilia wapi? Hivi kwenye uenyekiti na ikulu kuna biashara gani wanayokimbilia? Bahati mbaya wametumiwa na watu na wao wakakubali kutumika. Kama ni maarufu kwa juhudi zao basi ni wakati mzuri wa wao kutuonyesha nje ya chadema kama umaarufu wao utazidi kuimarika (sio kwa maeneneo wanayotoka tu ila kwa pande zote za nchi). Kwa tabia zao hawa vijana hawawezi wakakubali kuwa wanachama wa kawaida, hivyo kutofanya maamuzi sahihihi chama kitaendelea kuyumba.

Ulisikia wapi adui wako anamtetea kamanda wako. Acha wale wafinyu wa fikra waendelee na ngonjera zao za kusema chadema ni chama cha udini, ukabila na ukanda lakini wanaoelewa wanajua chadema ni chama cha kitaifa.

Hatuwezi kusema ccm ni chama cha kidini kwa sababu mwenyekiti na katibu mkuu ni wa dini moja au ni cha kikanda kwa sababu ukanda wa pwani kina wafuasi wengi (huo pia utakua ni upuuzi).

Watu hawaichukii ccm kwa kuwa chama cha kidini, kifamilia, kikabila, kikanda nk, bali kuwasahau walio wengi na kulinda
wachache ambapo sasa kimewekwa kwenye kona mbaya na hao wachache hakiwezi kufuruku kujinasua (kama ni wanaume
wavue magamba tuone). Hakuna chama chochote tanzania ambacho kitatumia udini, ukabila na ukanda kitaweza kupata
wafuasi tanzania kama chadema ilivyo na wafuasi nchi nzima.

Mwenyezi Mungu tunakuomba uibariki Tanzania, uwalinde wenye mapenzi mema na nchi hii, maana binadamu hawezi
kufanya chochote kukiwepo na ulinzi wako Bwana. Wape ujasiri watanzania ili wasiogope mabadiliko. Tupe amani ya
kweli wakati huu wa uanaharakati wa mabadiliko, tupe moyo wa kuvumiliana, tunakuachia wewe kupigana na wale wanaopanga njama ovu za kuwadhuru wengine ili waendelee kukaa madarakani kwa hira na ubinafsi, Amen​.
 
Siku nyingine yakikubana wahi msalani, sio vyema kuja kuyaachia hapa....

Udicteta wa Mbowe na Dr Slaa kwa watovu wa nidhamu kama wewe na Zitto kwani ukicheka na nyani utavuna mabua wasaliti wote wanao pokea vihela toka magambani ni wakupigwa chini bila mjadala.
 
Siku nyingine yakikubana wahi msalani, sio vyema kuja kuyaachia hapa....

Pamoja na kuishi kwa wazungu akili zako bado ni kama mchungaji ng'ombe, nimekubali
kwamba unafanya kazi ya Uyaya, hebu mtawaze mtoto haraka kajisaidia usije kufukuzwa
kazi. Sasa nakubaliana na wanaosema ulitafuna rambiranbi ya mjane, kama b7 inakutoa
Akili hivyo.
i
 
Kama ni kweli Mh. Mbowe na Dr. Slaa ni madikteta nawapa kongole. Maana udikteta wao unafaida sana. Udiktea wao usingekua na faida nadhani chadema isingefika ilipofika sasa na kuwa chama tishio kwa chama tawala ccm. Udikteta wao umekiimarisha chama na kuwa chama mbadala kinachosubiri kuingia ikulu.

Umekifanya chama ambacho kinapendwa na wanyonge (hivi chama kinachongozwa na dikteata mbaya kitapendwa na wanyonge?). Mh. Mbowe na Dr. Slaa mkiwakilisha uongozi wa juu wa chadema, ili tuwamini na kuwapa nchi 2015, msiogope kuwa madikteta wa kusimamia maamuzi ya chama na baadaye ya nchi.

Tuseme kweli, hivi kuna nchi yeyote duniani imendelea bila ya kiongozi wake kuwa na vitabia vya kidikteta; haiwezekani asilani. Hivi utavuna mazao ya shamba kwa kucheka na ngedere wanaokula mavuno. Mfano; unapanga kuendeleza vikundi vidogo vidogo vya wajasiliamali wadogo kwa kutenga mfuko unaoitwa mapesa ya mheshimiwa, halafu wajanja wachache wanakula hizo pesa bila kuwafikia walengwa na wewe unacheka nao, maendeleo yatakuwepo?

Unanapanga mipango ya maendeleo ya kijani (kilimo) unatoa ruzuku kwenye zana za kilimo (kama mboleo) halafu wajanja wachache wanajinuifaisha bila hizo zana kuwafikia walengwa (wakulima) halafu wewe unacheka cheka nao, maendeleo yatakuja? Unanzisha mjadala wa kuwavua gamba mnaowaita mafisadi halafu baadaye mnasema chama kitayumba mkiwavua gamba, kweli kwa staili hiyo nchi itasonga mbele? Ili kupata maendeleo ni lazima kiongozi awe na vitabia vya kidikteta, ambaye ni muumuni mzuri wa mungu (dini yeyote).

Mwenye huruma na watu wake, mwenye upendo kwa anaowaongoza, msikivu lakini anayetoa maamuzi na kusimimia maamuzi yake, asiyeogopa kulaumiwa kwa maamuzi yake kwa manufaa ya nchi n.k. Hivi vyote vinahitaji tabia ya kaudikteta hivi.

Ili chama kibaki na heshima yake, chadema fanyeni maamuzi magumu kwenye huu upepo unaopita. Safisheni chama muda huu, na chadema hakiwezi kufa kwa mtu mmoja kufukuzwa kwa kuyumbisha harakati za kuipumzisha ccm,hivi hawa vijana mbona walikua na ‘future' nzuri sana.

Wametuonyesha kwamba sio wavumilivu hawa ndio madikteta hatari wa siku za mbele. Maana dikteta mbaya ni yule asiyekuwa na subira, anayetaka kuongoza kwa njia yeyote hata kama ni haramu. Tunajua akina dr. Slaa kuna siku nao watapumzika muda muafaka ukifika (kwa sasa bado tunawahitaji), kwa nini hao vijana wasingendelea kujijenga taratibu na kuvuta subira?

Wanakimbilia wapi? Hivi kwenye uenyekiti na ikulu kuna biashara gani wanayokimbilia? Bahati mbaya wametumiwa na watu na wao wakakubali kutumika. Kama ni maarufu kwa juhudi zao basi ni wakati mzuri wa wao kutuonyesha nje ya chadema kama umaarufu wao utazidi kuimarika (sio kwa maeneneo wanayotoka tu ila kwa pande zote za nchi). Kwa tabia zao hawa vijana hawawezi wakakubali kuwa wanachama wa kawaida, hivyo kutofanya maamuzi sahihihi chama kitaendelea kuyumba.

Ulisikia wapi adui wako anamtetea kamanda wako.acha wale wafinya wa fikra waendelee na ngonjera zao za kusema chadema ni chama cha udini, ukabila na ukanda lakini wanaoelewa wanajua chadema ni chama cha kitaifa.

Hatuwezi kusema ccm ni chama cha kidini kwa sababu mwenyekiti na katibu mkuu ni wa dini moja au ni cha kikanda kwa sababu ukanda wa pwani kina wafuasi wengi (huo pia utakua ni upuuzi).

Watu hawaichukii ccm kwa kuwa chama cha kidini, kifamilia, kikabila, kikanda nk, bali kuwasahau walio wengi na kulinda
wachache ambapo sasa kimewekwa kwenye kona mbaya na hao wachache hakiwezi kufuku kujinasua (kama ni wanaume
wavue magamba tuone). Hakuna chama chochote tanzania ambacho kitatumia udini, ukabila na ukanda kitaweza kupata
wafuasi tanzania kama chadema ilivyo na wafuasi nchi nzima.

Mwenyezi Mungu tunakuomba uibariki Tanzania, uwalinde wenye mapenzi mema na nchi hii, maana binadamu hawezi
kufanya chochote kukiwepo na ulinzi wako bwana. Wape ujasiri watanzania ili wasiogope mabadiliko. Tupe amani ya
kweli wakati huu wa uanaharakati wa mabadiliko, tupe moyo wa kuvumiliana, tunakuachia wewe kupigana na wale wanaopenga njama ovu za kuwadhuru wengine ili waendelee kukaa madarakani kwa hira na ubinafsi, Amen​.

1378137_487023108060382_1249243279_n.jpg

WANAKUNYA JUICE PEKE YAO ; MM-MBOWE KAMTENGA ZITTO IKULU
 
Pamoja na kuishi kwa wazungu akili zako bado ni kama mchungaji ng'ombe, nimekubali
kwamba unafanya kazi ya Uyaya, hebu mtawaze mtoto haraka kajisaidia usije kufukuzwa
kazi. Sasa nakubaliana na wanaosema ulitafuna rambiranbi ya mjane, kama b7 inakutoa
Akili hivyo.
i
Njoo na wewe nikutawaze
 
Kete ya CCM ilikuwa kwa Zito sasa kwisha habari yake! Akijitetea vyema atabakia kuwa mwanachama kama Shibuda.
 
kama unadhani slaa na mbowe wanafaa kupewa nchi basi kawape nchi ya m am a yako sio Tanzania.
 
Back
Top Bottom