Hivi ni kweli Mbeya inanyimwa maendeleo sababu ya CHADEMA au kuna jambo limejificha?

Kuna mjadala unaendelea kwamba Mbeya inanyimwa maendeleo sababu ya Chadema, kwahiyo akipewa Dkt. Tulia, Mbeya itasonga mbele.

Kuna wemgine wanapinga wanasema kama suala ni Chadema mbona Arusha, Moshi, Kawe, Ubungo nk kuna miradi mikubwa tu imejengwa na serikali wakati wabunge wa hapo ni Chadema? Mbeya inakwama wapi?

Awamu hii ukitoa Dar es Salaam, maendeleo yote yameelekezwa Mwanza kwa kiasi kikubwa, Arusha na Dodoma

Aliyekudanganya kuwa Jimbo la Kawe limeendelea na Kupiga Maendeleo makubwa katika Awamu za Mbunge Halima Mdee ni nani Ndugu yangu?
 
Mkoa wa Mbeya na Mikoa mingine ya kusini hasa Lindi na Mtwara imesahaulika na serikali na ndiyo maana maendeo yake yako chini sana. Kwa ufupi Mkoa wa mbeya na wilaya zake ni maskini, serikali inapaswa kuuangalia kwa jicho la huruma maana hata wao ni Watanzania. Hakuna mradi wowote wa maana kule ukilinganisha na sehemu zingine, mji wa Mbeya ni aibu hata kuita jiji na kunasehemu Wilaya ya Rungwe wananchi walikuwa wanavuka mto mkubwa kwa kamba na miti mpaka mbunge wao alipojitolea kujenga daraja la kubabaisha kwakutumia pesa yake binafsi , kuna maeneo nchi hii hali kama ile ikionekana basi hatua huchukuliwa haraka sana. Wakati mikoa mingine ikipiga hatua kwenda mbele mbeya inapiga hatua kurudi nyuma.
Mkuu unaweza ukawa hujaijua mbeya vizuri.
Ni kweli mbeya hakuna miradi mikubwa ilopelekwa na serikali ,ila mbeya sio masikini.

Mbeya unaendelezwa na wananchi wenyewe na miradi midogo midogo ya ndani,ukiangalia Wilaya kama Rungwe na kyela hakuna wilaya yoyote ya jiji la Arusha inazipita kwa ukuaji wa mji na mazingira...nmeongelea Arusha kwakua ndio nina experience nao.

Ila jiji kama jiji dah ni Aibu kubwa,jiji limeminywa mpaka basi,hamna cha maana hadi stand tu gavoo haijaweka
 
Mbeya the Green City. hatutegemei hisani wala hatujipendekezi Magogoni wala Chamwino kufanya maisha yetu. Tunae Mungu anaenyesha mvua zisizokoma mwaka mzima.
 
Sidhani kama ndio sababu. Mbona wilaya ya kyela inaongozwa na mbunge Wa ccm lakn haina maendeleo?
Mwakyembe anaiongoza Kyela ila anawachukia wanaKyela na ndio maana anawakomesha makusudi .....Mwakyembe gombea majimbo ya Dar waachie wakazi wa Kyela wachaguane
 
Mkoa wa Mbeya na Mikoa mingine ya kusini hasa Lindi na Mtwara imesahaulika na serikali na ndiyo maana maendeo yake yako chini sana. Kwa ufupi Mkoa wa mbeya na wilaya zake ni maskini, serikali inapaswa kuuangalia kwa jicho la huruma maana hata wao ni Watanzania. Hakuna mradi wowote wa maana kule ukilinganisha na sehemu zingine, mji wa Mbeya ni aibu hata kuita jiji na kunasehemu Wilaya ya Rungwe wananchi walikuwa wanavuka mto mkubwa kwa kamba na miti mpaka mbunge wao alipojitolea kujenga daraja la kubabaisha kwakutumia pesa yake binafsi , kuna maeneo nchi hii hali kama ile ikionekana basi hatua huchukuliwa haraka sana. Wakati mikoa mingine ikipiga hatua kwenda mbele mbeya inapiga hatua kurudi nyuma.
Mkuu hv Mbeya inaifahamu ?? Asikudanganye mtu bhana..mbeya huwezi kuifananisha na geita shinyanga Dodoma wala morogoro...baada ya dar na mwanza ndo inafuata mbeya kimaendeleo...mbeya ya sugu sio ile ya mpesya aliyekuwa mbunge wa mbeya mjini...
 
Mtu anaesema Mbeya ipo nyuma kimaendeleo hajatembea, au hajafafanua maendeleo ya namna gani, Mbeya ni moja ya mikoa mizuri na yenye maendeleo katika nyanja nyingi sana,
 
Kuna mjadala unaendelea kwamba Mbeya inanyimwa maendeleo sababu ya Chadema, kwahiyo akipewa Dkt. Tulia, Mbeya itasonga mbele.

Kuna wemgine wanapinga wanasema kama suala ni Chadema mbona Arusha, Moshi, Kawe, Ubungo nk kuna miradi mikubwa tu imejengwa na serikali wakati wabunge wa hapo ni Chadema? Mbeya inakwama wapi?

Awamu hii ukitoa Dar es Salaam, maendeleo yote yameelekezwa Mwanza kwa kiasi kikubwa, Arusha na Dodoma
Hiki kitu nilikua najiuliza...lakin mbeya jiji kubwa....Ila vumbi ad katkat ya mji hata kairinga kanakuja juu et.....kamji kasafi wametoa vumbi katkat ya mji...n mirad Kama wind power....

Mbeya ikiendelezwa itatisha sana
 
upo sahihi mkuu
 
Back
Top Bottom