Hivi ni kweli mauaji ya albino yameanza hivi karibuni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kweli mauaji ya albino yameanza hivi karibuni?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hofstede, Jan 12, 2009.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ninakumbuka zamani kulikuwa na uvumi kuwa, albino hawafi, yaani wanaishi ukifikia muda wao hutoweshwa na kwenda kusikojulikana. Ilifikia mpaka watu wakawa wanabishana kuwa ni nani aliwahi kuhudhuria mazishi ya albino?. Kwa kweli hakuna mtu aliyekuwa na jibu na wote niliowafahamu walisema hawajawahi. Kutokana na kuzuka kwa mauji ya albino kwa kasi hivi sasa mtu anaweza kufikiria kuwa huenda mauaji haya hayakuanza leo ni mambo yaliyokuwepo tangu zama kwa imani hizo hizo za kishirikina na wahenga wakaamua kuleta dhana hiyo ili kuficha yaliyokuwa yanajili gizani kuhusu hawa ndugu zetu.

  My take: Kutokana na kuongezeka kwa watu na hali ya uchumi huenda kuna waliojaribu kuona kuwa demand imekuwa kubwa na hivyo kuanza vitendo vya ukatili vya hawa ndugu zetu albino kwa uwazi. Na kama uvumi huo ungekuwa ni kweli kuwa Albino hutoweka basi leo hii nafikiri tusingeshuhudia mauji ya kinyama ya hawa ndugu zetu, nafikri hili suala tuliangalie kwa upana zaidi, kuwa kwa nini zamani watu waliaminishwa kuwa albino hawafi? hutoweka?
   
Loading...