Hivi ni kweli maji baridi (Maji ya mito)na maji ya bahari hayachanganyiki?

Wakulonga

JF-Expert Member
Oct 29, 2012
659
1,000
Habari wana JF! Katika soma soma yangu nimepata kuona katika vitabu vya dini kuwa maji matamu na maji ya bahari hayachanganyiki. Pia Kila mara nikielekea Zanzibar kwa boti nifikapo Msasani lazima kuwe na wimbi hata kama bahari iko shwari nikauliza nikaambiwa hapa kuna mkondo wa maji matamu ( baridi) sasa hii kisayansi imekaaje wajuzi tujuzeni jamani.
 
natoka hapa

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
8,503
2,000

Ni kweli hayachanganyiki, hii ni kutokana na tungamo (density) za maji hayo kuwa tofauti.

Maana yake maji yenye chumvi yanakuwa mazito ukilinganisha na maji yasiyokuwa na chumvi.
 
Mwanamaji

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
1,665
2,000
Habari wana JF! Katika soma soma yangu nimepata kuona katika vitabu vya dini kuwa maji matamu na maji ya bahari hayachanganyiki. Pia Kila mara nikielekea Zanzibar kwa boti nifikapo Msasani lazima kuwe na wimbi hata kama bahari iko shwari nikauliza nikaambiwa hapa kuna mkondo wa maji matamu ( baridi) sasa hii kisayansi imekaaje wajuzi tujuzeni jamani.
Ngoja namimi nishee tumaarifa kidogo hapa:

Kinachotofautisha maji ya bahari na maji baridi (usiseme maji matamu tafadhali) ni kiwango cha chumvi kilichomo ndani yake (Salinity). Majibahari yana chumvi nyingi huku maji baridi yakiwa na kiwango mno cha chumvi.

Ukichukua lita moja ya maji bahari na moja ya maji baridi ukavipima uzito, yale ya bahari yatakua mazito zaidi kuliko maji baridi kwa sababu ya ile chumvi iliyomo ndani yake.

Kwahiyo hadi sasa tunaweza kukubaliana kwamba ''sea water is denser than fresh water'' kama alivyoeleza mdau mmoja hapo juu.

Kwa kanuni za kifizikia juu ya vimiminika vyenye ''density' tofauti vinapokutana, kile kizito zaidi (more denser) kinakaa chini na chepesi kinakaa juu.
Mfano ukichukua mafuta na maji, maji yanakua chini na mafuta (mfano ya taa) yanakua juu kwa sababu maji ni mazito (denser) zaidi ya mafuta.

Linapokuja suala la maji ya bahari yanapochanganyikana na maji baridi, mfano mto unapoingia baharini, maji baridi huwa juu ya maji bahari (kwa sababu ya wepesi wake). Huu utengano kitaalamu tunaita ''stratification''.

Lakini baadae haya maji yanakuja kuchanganyikana kutokana na nguvu za upepo na mkondo wa bahari (Ocean currents) ili kupata ''fairly even water salinity'' ya maji ya ''ukanda'' fulani wa bahari.

Hivyo basi, dhana ya kwamba maji ya bahari na maji baridi hayachangayikani inakua sahihi kwa kipindi kifupi tu, baada ya muda yanakuja kuchanganyikana kwa utaratibu nilioueleza hapo juu.

Suala la mkondo wa Msasani sitaligusia kulijibu kwa sababu naona limekaa katika muktadha wa ''marine navigation'' zaidi (linawafaa mabaharia zaidi) na mada hapa inahusu ''mixing behavior'' kati ya maji chumvi na maji baridi.

Pia kama ukipenda kujua kuhusu ''water masses'' humo baharini basi utanambia maana kuna makundi mengi ya maji chumvi yenye tabia mbalimbali na tofauti tofauti na yanaweza yasiwe yanachanganyika pia.

Nadhani angalau utakua umepata kitu.
 
Ntalukwilasa

JF-Expert Member
Jun 24, 2017
776

Asante sana
 
Wakulonga

JF-Expert Member
Oct 29, 2012
659
1,000
Hapo

Hapo nimeelewa vema ila kama utatuelimisha juu ya water masses nayo itakuwa vema
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom