Hivi ni kweli maisha ya mtanzania 2011 ni bora kuliko ilivyokuwa miaka 50 iliyopita? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kweli maisha ya mtanzania 2011 ni bora kuliko ilivyokuwa miaka 50 iliyopita?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mo-TOWN, Jul 17, 2011.

 1. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  JF naomba tujadiliana hii mada. Binafsi napata shida kidogo kukubalina na kauli hiyo.

  Naomba tuwe objective tuangalie swala hili qualitatively siyo kujadili siasa za jumla ya kilomita za barabara, idadi ya shule etc.

  Mimi niliyesoma shule ya msingi na sekondari miaka ya 80 ukweli ni kwamba mazingira ya shule (quality ya walimu, vitabu) then yalikuwa general bora kuliko leo kwa shule zile zile nilizosoma. Nakumbuka kulikuwa na barabara za lami mitaa ya magomeni mapipa/Kondoa, ilala gerezani na sehemu nyingi za nchi ambayo leo hii hazipo. Na tujadili sasa.
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Jiulize miundombinu aliyojenga mjerumani leo ipo wapi?walau wazee walipata kazi ya umanamba ktk mashamba makubwa ya chai katani.hii miaka -ve 50 kabla sio baada ya uhuru
   
 3. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa miaka 50 ya uhuru Tanzania TUNASONGA MBELE KWA SWALA LA IDADI [QUANTITY] NATUNA RUDI NYUMA KWENYE UBORA [QUALITY ] za mambo na vitu vyetu vingi kwenye jamii yetu.Tuna ongezeko la Shule za Msingi,Sekondari na hata Vyuo vikuu [Universities] vingi lakin vyenye uwezo mdogo wa kuzalisha wasomi na kada zenye uwezo mdogo kukidhi mahitaji ya soko kulingana na zama tulizo nazo sasa hivi.

  Matokeo hayo yameendelea hivyo hivyo mpaka kwenye UTAWALA,SIASA,AFYA,VIWANDA NA MENGINEYO.Kazi hipo japo wanaotuongoza kwa kuwa wao katika maisha yao ya kila siku matumizi yao yamezungukwa na vitu vyenye UBORA [QUALITY].Kwa mantiki hiyo HAWANA CHA KUPIMIA MBELE YA UMMA WENYE WINGI WA SHULE ZA KATA [KAYUMBA], VITUO VYA AFYA VISIVO NA DAWA,VYUO VYENYE UTITILI WA WANAFUZI VISIVYOWEZA KUWAHUDUMIA.
   
Loading...