Hivi ni kweli kwamba tumeshindwa kabisa kusimamia matumizi halali ya kodi zetu?

Mwamsosi

New Member
May 23, 2011
2
0
Nawapongeza wote ambao mmekuwa mstari wa mbele kuweka wazi yaliyofichika na uchafu wa wale walioteuliewa kuongoza na badala yake kutawala!

Pongezi za pekee kwa mwanzilishi/waanzilishi wa hili jukwaa!

Swali lipo wazi, je kabla ya kulaumu kuna hata mmoja wetu amewahi chukua hatua yoyote kutaka kujua matumizi ya kile achangiacho kama kodi?

Siwaungi mkono watawala wa sasa maana si viongozi bali sisi tunachukua hatua gani madhubutu kuwawajibisha watawala hawa? Nimechoka na malumbano yasiyo na msingi tuingie kwenye utekelezaji.

Salam kwao wanaouhujumu uchumi wa taifa hili, watanzania tumechoka uvumilivu umefika kikoma! Mtujibu kwa vitendo na si kuhubiri kumaliza ufisadi
Je mwajua mwastarehe kwa kodi zinazowatesa watanzania masikini. Kodi rejea imekuwa ndoto kwa mtanzania tangu serikali ya awamu iliyopita!
 
Ni kweli kuna haja kubwa kwa watanzania kuanza kuchukua hatua za wazi kupinga matumizi mabaya ya fedha za umma. Hatua hizo zinaweza kuanzia katika kususia ziara za viongozi zinazoambatana na misafara mirefu. Hivi majuzi Dr.Slaa akiwa jimboni kwa Pinda, alisema msafara wa waziri huyo mkuu unajumuisha magari yapatayo 30 ambayo thamani yake ni shs.600 bilioni. Matumizi kama hayo ni ya ubadhirifu na qwananchi wana kila sababu za kususia misafara kama hiyo ambayo ina kila dalili za kuwakoga badala ya kuwaletea faraja kutoka na hadha za maisha zinazowakabili.
 
Back
Top Bottom