Hivi ni kweli kwamba kiswahili kinaupungufu mkubwa wa msamiati wa maneno ya kisayansi

Mpigamsuli

JF-Expert Member
May 24, 2012
3,885
575
wana jf ninaomba mnipe sababu za msingi kwamba kiswahili kinaupungufu mkubwa msamiati ukilinganisha na kiingereza evdenc
 
Hilo liko wazi mfano maneno kama PRINTER,CPU,USB,MODEM,MOUSE nk sidhani kama kuna tafsiri ya moja kwa moja kutoka kiingereza kuja kiswahili, Kwa kweli lugha yetu ya kiswahili ina upungufu mkubwa sana wa misamiati ukilinganisha na lugha nyingine za kimataifa kama kiingereza.Pamoja na kutohoa maneno kadha wa kadha kutoka lugha hizo za kigeni ila bado lugha yetu haijitoshelezi kimsamiati,me naona sababu kubwa ni ukosekanaji wa wataalamu wa kutosha,pamoja na kuidharau lugha yetu wenyewe(Kasumba) n.k
 
Kichapishio, UKI(uti wa mgongo wa kinakilishi), waya malaya, kinasa mawimbi mtandao, na kielekezo komandi. Una lingine?
 
waliosoma degree za kiswahili ndio wanafosi mambo na kutuletea maana za kulazimisha ambazo hata hazina ladha mdomoni, ni bora kutumia maana ya neno kama lilivyo kwa kiingereza. sababu pia kiswahili ni lugha iliyoundwa na mchanganyiko wa lugha nyingi kiarabu+kingereza+kireno n.k , hivyo bora tukaendelea kutumia neno kama lilivyo na sio kulazimisha maana.
 
Kwanza kabisa kila lugha inajitosheleza kimsamiati kwa watumiaji wa lugha husika pasipo kuchanganya na mapokeo kutoka nje ya jamii husika. MF. Hakuna mahali ambapo kiswahili kitakosa neno kwa ajili ya kitu au jambo lolote ambalo asili yake ni ndani ya jamii ya waswahili.Lakini ni dhahiri kuwa kiswahili kitakosa neno la moja kwa moja kwa kitu ambacho kilianzia nje ya jamii ya waswahili then kikaletwa katika jamii ya waswahili hadi pale watumiaji wa lugha hiyo watakapoipatia neno mbadala la kiswahili.
 
Hawa wataalamu wetu wa lugha mambo ya kulazimisha kutafsiri maneno ya lugha za kigeni mwisho watatuletea matusi,mf:dadavuzi mpakato (laptop),mara waya malaya ni bora tutumie tu maneno kama yalivyo.
 
Kiswahhili kina misamiati ya kutosha,sema tu ni uzembe wenu wa kutokuwa karibu na kamusi,vitabu vya isimu na fasihi, na wataalam wa kiswahili.
Ukitaka kuthibitisha huu uzembe fuatilia tofauti kati ya watangazaj wa tz na wale wa Idhaa za kiswahili za BBC,DW,VOA,RFI.
 
Back
Top Bottom