Hivi ni kweli kuwa wasichana hawapendi mwanaume bila kupewa kitu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kweli kuwa wasichana hawapendi mwanaume bila kupewa kitu?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Akili Unazo!, Aug 7, 2009.

 1. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,812
  Likes Received: 2,520
  Trophy Points: 280
  Kumekuwa na hija nyingi sana kwenye thread zinazohusiana na mahusiano na michango mingi kuwa wasichana walio wengi kuwa hawawezi kumpenda au kujenga uhusiano na mwanaume kama hakuna kitu atakachopewa iwe gari/pesa/kulipiwa kodi ya nyumba/ada ya shule/kununuliwa au kupewa hela kwa ajili ya vipodozi/kujaziwa gari mafuta?

  Kwa nini hawa viumbe wanashutumia tuhuma kubwa kama hiyo.

  Hivi ni kweli bila kitu hakuna upendo??????
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Chaku, thread zako nyingi zinashabihiana.
  Unafanya utafiti nini juu ya viumbe hawa adhimu?

  Hawa wanawake bana, hasa wa dunia ya leo, ni wabaya sana!

  Wanatumia kauli kama ya Invisible kwamba ` mkono mtupu haurambwi`!

  Kwa msichana ambae yuko katika standard ya kawaida tu, lazima uonyeshe msisitizo wa hela ya makemiko, maenjo-face, malipstick, machok-stick na kadhalika, ili at least akuelewe unachomaanisha!

  Sasa hujaenda kwa hao wa kutaka nyumba na ma-Harrier`

  Fedha zimechukua nafasi ya juu sana katika penzi, hata hawa wadada wa humu JF wanajua hilo, japo watalielezea kwa kulipamba kwa maneno ya kulifunikafunika kiaina!

  Zamani, pesa hazikutumika kwa kumvutia mwanamke! Kilichozingatiwa ni uchapa kazi na upendo!...jaribu sasa hivi, hata kama umepewa tuzo zote za ufanyakazi bora, bila ya kuhonga ndugu...mke unamkosa!

  Nawahurumia sana akina Sipo ambao wana Vision2015 za kuoa, maana kipindi hicho sijui itakuwaje! Kwi kwi kwiiii...
   
 3. GP

  GP JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  shemeji,
  bila kutoa kitu mapenzi siku hizi hayapo!, ndo maana waswahili wanasema kono mtupu haulambwi!. ila sio kwa wanawake wote, wengine hawana nongwa na kitu kutoka kwa mwanaume.
  ingawa mapenzi ya kweli ni moyo wa mtu kumridhia mwenzi wake katika hali yoyote ile, hivyo mwanaume nae iabidi ajitahidi kadri ya uwezo wake kumpatia mwanamke chochote kile, na kwakua uwezo wa mtu unatofautiana na mtu mwingine, basi mwenye uwezo kubwa atatoa gari, mwenzangu na mie hata bajaj sina nitatoa kadri ya uwezo wangu.
  unapompa kitu mwenzi wako iwe pesa au mali inaonyesha ni jinsi gani unamjali na kumpenda. hali hii itakua tofauti pale tu mwanaume akiwa hana uwezo mkubwa na mwanamke akitamani awe na kitu ambacho labda kaona mwanamke mwenzake kapewa, hapo huyo mwanamke ataona hakuna mapenzi.

  shemeji, hebu tujikumbushe kwenye mada moja ulisema hivi
  na huyu mbeijing mwingine nae alisema hivi:
  hapo ukimpa mwanamke gari, pesa, nyumba etc, atakuona unampenda sana.
  ni sawa na demu wa mkuu Fidel80 alipokua anakomaa apewe elfu 70 akare-touch nywele akidhani ndio anapendwa!, so mkuu asingekua anampa hizo elfu 70 basi huyo mwanamke angesema hapendwi, lakini kwa kua mkuu Fidel80 ni PDG, haikusumbua kivileeeee!
   
  Last edited: Aug 7, 2009
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Demu wa Bongo!! Penzi = Pesa!

  Kama huna pesa penzi linafulia haraka sana Bongo!
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Je ingekuwaje kama wangekuwa hawapewi kitu kabisa? Wengi hawana kazi na hutegemea waume zao. Yaani kuna mtu anafikiria kuwa utamtongoza demu ukajiangushe nae then aondoke hivi hivi bila hata voucher. Hiyo itakuwa mbingu sijui ya wapi. Vitu vingine ni demand driven , vinakuja tu hata kama hajakuomba.
   
 6. The Native Son

  The Native Son Member

  #6
  Aug 7, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Ebwana wanawake wanapenda sana utegemezi japo degree zimetofautiana kutoka mmoja kwenda mwingine na hili ndilo linalowafanya eti ili aone kuwa anapendwa basi lazima yule ampendaye akidhi matakwa yake ya utegemezi ndio maana utaona mwanamke kuna mambo ambayo ni madogo madogo, kwa nionavyo mimi, anaweza kujimudu mwenyewe lakini atataka atekelezewe na mwanaume. Hiyo ni kwa upande ule

  Ila kwa upande huu sasa, utaona kidume kinatafuta sifa kuingia gharama ambazo hata huyo mwanamke mwenyewe haitaji ilimradi kuonesha misuli yake kukidhi ambacho hajatakiwa kukifanya. Nadhani huwa ni MISIFA YA KIJINGA. Hii nayo ni upande huu

  kwa pande zote sasa nadhani ni mambo ya sidhani kama nikiyaita ya kuumbwa hivyo, mara nyingi wanaume wanadhani kupenda ni kuonesha misuli kiuwezo wa material na wanawake kwao kupendwa ni kupatiwa materials wanazohitaji. Ni hayo
   
 7. k

  kissgarage Member

  #7
  Aug 7, 2009
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 30
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  saa nyingine na ninyi mnapenda sana kuhonga.
   
 8. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  hatutaki mwanaume suruali , tunataka pesa...........joke. ndo mambo ya leo.

  Nanyi wanaume mmezidi kujipendekeza hata kama mwanamke hataki basi unampa tu ili uonekane kibosile.
   
 9. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #9
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,395
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  dah mkuu iyo mada ya leo saluti yani

  kama vile ulikuwepo mioyoni mwa masela wangu wote ambao huwa tunajadili mambo kama hayo!

  theone
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ndiyo wanawake wa namna hiyo wapo ila siyo wote. The same way kuna wanaume wanamtaka mwanamke kwa ajili ya uroda tu ila si wote. It's a two way thing. Cha muhimu ni uangalie ni wanaume/wanawake wa aina gani unao waattract. Kama wewe kila ukitongoza unatumia gia ya pesa uta attract wanawake wachunaji kila siku na wanawake wa maana kamwe hawata kupa time.
   
 11. N

  Nkashilingi Member

  #11
  Aug 7, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hodi hodi jamani wanajamii nipokeeni maana mie ni mgeni humu wa kuchangia ingawa ni msomaji sana hii site long time, Nadhani mmenipokea kwa mikono yote,
  TUwe wakweli mapenzi bila hela au gari au chochote kama nyumba ni BIG NO, basi kama huna kabisa hata voucher!! dunia ilishapinduka long time wajameni, Money first!!
   
 12. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2009
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Wapo wanaopenda bila chochote ila ni wachache sana, au nyie haijawahi kuwatokea? Poleni.
   
 13. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Tabia za utegemezi ziko kotekote kwa wanaume na wanawake.Kinachotofautiana ni dhana na hulka zilizomo kwenye jamii na vichwa vya watu.Nitatoa maoni yangu kuhusu kilichozungumzwa hapo juu na nikawekea rangi kama ifuatavyo.
  1.Black - Hiyo ni dhana potofu.Wapo wanawake na wanawake.Kuna wenye kupenda utegemezi kama walivyo wanaume wenye kupenda dezodezo. Inategemea hao unaowajua wewe wenye hulka hiyo.
  2.Red- Hilo ndio jibu.Kujipendekeza na kujifanya unakuja kumuokoa mtu ambaye wakati mwingine hana hata haja ya kuokolewa nawe.
  3.Purple -Mwanaume mwenye mwelekeo huo mara nyingi ana mapungufu ambayo anajaribu kuyaficha kwa kujifanya anavyo vya kutoa kama msaada wa mama Theresa.
  Kwa maisha ya sasa ni ujinga wewe mwanaume kujifanya unajua sana kuhonga.Mambo ni kupeana.Ila ukipenda mwanamke aliye dhaifu kwa kila hali kuanzia kufikiri hadi kujitafutia, basi uwe tayari kumgharamia kila kitu na usilalamike mwisho wa siku.Toa kwa moyo mmoja.

  Halafu jamani msisahau pia kuwa hakuna mwanaume anamtaka mwanamke hivihivi tu.Na ndio maana kwa miaka ya sasa inakuwa ngumu kwa wadada kujitunza hadi wafikie kufunga ndoa bila kutoa chochote! Mbona hili nalo hamlioni?
   
 14. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,497
  Trophy Points: 280
  heheheh,..Nkashilingi..does that signify your name? laribu JF!
   
 15. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #15
  Aug 11, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,497
  Trophy Points: 280
  Yaani WoS hapo umemaliza kila kitu. Mi binafsi siamini katika mapenzi ya kuegemea kwenye pesa tu! nadhani tulishajadili hii kitu hapa siku si nyingi zilizopita. Pesa, magari, nyumba na vyote vilivyomo humo ni viwezeshaji tu mapenzi ya kweli yapo moyoni mwa mtu! Mtu anayesisitiza sana mambo hayo 'ya kidunia' ni wa kuogopwa kama ukoma manake hakuna mapenzi ya ukweli hapo!

  Bahati nilishapenda zamani na hakuna kupenda mara mbili lakini sidhani kama ningebadili msimamo eti kwa vile siku hizi 'mambo yamebadilika'?

  Mkuu Mbu vipi au ndo swaumu imeshaanza?:cool:
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  huu ukweli ni ukweli kabisaa! Consciously wanasema wanapenda bila mali ila subconsciously ni kinyume. wanaume msidanganyike na kauli zao. dhahiri ni pale mwanamke anapokupita kipato. ishini nao kwa akili kama biblia inavyoagiza. mwanamke anakuforecast kwanza ndio akukubali au akuchune au akutumie kwa starehe nyingine. ONYO! si wote bali ni asilimia kubwa
   
 17. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  women can spot a sucker,from a mile away.Billionaire Bernie Eccelstone,F1 supremo na ex wife wake ex model Slavica wapi na wapi!.women only want money as a compensation for not really fancying their man.ndio maana city boys rather then have these high maintenance headaches wanakuwa patrons wa hookers na lapdancing hotspots.
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Dada Chaku mkono mtupu wanasema haulambwi.
   
 19. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Kuhonga inatumiwa kama nyenzo na wanaume wengi. Lakini pia kina dada wengi bwana bila ya kuwa na fedha hata kama anakupenda, ujue utahangaishwa sana. Ndo mambo yalivyo, bottom line utafanyaje
   
 20. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Mi naona kama siku hizi wote tunahitajiana kabla ya ndoa. Siamini ni wanaume tu ndo wanapoanza uhusiano wanahitaji kupewa dozi. Hata kina dada nao ukiwa na relationship bila kumgusagusa anaweza akakufikiria vingine.
   
Loading...