Hivi ni kweli kuwa Rais ana mamlaka ya kufanya chochote anachotaka?

Salam wakuu!

Yameishasemwa mengi...!

Nimekaa nikawaza kuhusu mwenendo wa jitihada za kupambana na corona hapa nchini nikapata maswali kadhaa ambayo sijayapatia majibu.

Ni wazi kuwa hakuna anayeridhishwa na ushiriki wa rais katika vita hii.

Ukiachilia mbali kwa inavyosemekana kuwa rais hayupo ikulu kwa sasa kutokana na sababu zisizojulikana, bado ameendelea kutoa kauli ambazo hazina tija kwa taifa kulingana na hali ulivyo kwa sasa, ameonekana kuwa mkaidi dhidi ya hatua zinazodhaniwa kusaidia katika mapambano.

Maswali ninayo jiuliza ni-
1. Rais ana mamlaka ya kufanya chochote anachojiskia?
2. Je, mihimiri mingine ya serikali kama bunge na mahakama haina uwezo wa kumshurutisha kuchukua hatua flani?
3. Hakuna mamlaka zinazoweza kumuamuru arudi ofisini kwake mara moja?
4. Hakuna mamlaka zinazoweza kupinga waziwazi maamuzi yake?

Nihitimishe kwa kusema kuwa vita hii ni ngumu sana na Mtu anayetakiwa kuongoza mapambano hatumuelewi.
Ni kwa Tz tu, ndio rais ana madaraka kupindukia, mihimili mingine haina chao. Rais anadai ndie anayewalipa hivyo ndio kila kitu, sisi tunaotoa hizo hela pia tumefungwa midomo na tunatandikwa ikibidi, kwani wawakilishi wetu, wanawakilisha chama, sio jimbo na watu wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom