Hivi ni kweli kuwa bajeti ya kukimbiza mwenge ni kubwa kuliko ya wizara ya viwanda na biashara?

Seif al Islam

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
2,156
638
Nakumbuka bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara (ambayo ndio Wizara ya Kipaumbele kwa Mujibu wa Ilani ya CCM) ilikuwa shilingi bilioni 99 hivi kama sijasahau na juzi tu tumetoka kuzima Mwenge ambao inadaiwa kuwa Gharama ya kuuzungusha nchi nzima (bila kujali pesa hizo zilitoka wapi) ni shilingi zaid ya bilioni 200.

Takwimu hizi zimeniacha nikiwaza kama ni za kwel au ni ghiliba za wale vijana wanaolipwa ujira mdogo kumzuia mzee asitekeleze mipango ya maendeleo. Naomba mwenye taarifa sahihi atusaidie.

Screenshot from 2016-10-16 10-53-10.png
 
Kuna mambo ni ujinga wa hali ya juu, na kila mmoja anakubali kuwa ni ujinga lakini hakuna mwenye uthubutu wa kuchukua hatua. JPM alijaribu kuupumzisha kwa mwaka mmoja.
 
Back
Top Bottom