hivi ni kweli kupiga kura ni haki yangu?

wiser

Member
Feb 16, 2008
6
0
mara nyingi najiuliza hili swali wakati wa kampeni huwa kunakuwa na kaulimbiu inayosema"kupiga kura ni haki yako" mi inanikanganya sana hii, kama kupiga ni haki yangu ya kimsingi ya kidemokrasia kwa nini wakati wa kampeni hasa kwa vyama vya upinzani kunakuwa na askari polisi kibao na ffu ambao lazima ama wapige watu ama wawarushie mabomu ya machozi!

yote tisa, kumi siku yenyewe ya kupiga kura ndio balaa, polisi ni wengi ajabu,usipindishe mstari wa kuingia kwenye chumba cha kupigia kura, sasa haki ya kidemokrasia iko wapi? si afadhali ukae nyumbani usubiri story za walioenda huko alfajiri ili wawahi kuepuka usumbufu na msongamano lakini bila mafanikio, kwani hakika huboreka! haki gani hiyo?

kuna lingine hili kuibiana kura huko sitagusia sana kwani sina eveidence mwana wane, lakini kwa nyepesi nyepesi ndicho kilichotokea katika jimbo la ubungo jimbo la mbunge mvivu ajabu sijawahi kuona popote kwa hakika, huyu ni Charles Keenja ambaye anadaiwa kumshinda kwa mlango wa nyuma John Mnyika wa chadema.

nakutana na watu wengi ambao wanasema wao siku hizi mtindo ni kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili wapate kile kitambulisho lakini mwisho wa siku hawaendi kubanana kupiga kura! je kwa mtindo TZ itakuwa na demokrasia huru na ya haki lini jamani?????????
 
Kupiga kura ni haki kabisa ya kila mtanzania lakini ni haki ambayo watanzania wengi au kwa kutojua au kwa kudanganywa wamepoteza haki zao nyingi.

Watanzania wamepoteza haki hii kama vile mtoto ambaye pamoja kwamba vitu alivyoacha baba yake alipofariki ni vyake lakini amekaa mbali navyo na wakati mwingine ulazimika kwenda kwa majirani akiomba ruhusa ili akavune matunda ndani ya shamba la marehemu baba yake.

Nakumbuka kisa hiki ambacho nikikikumbuka hata leo ingawa ni miaka mingi imepita nacheka sana kwa ujinga wangu niliokuwa nao wakati huo.

Siku moja nyakati za likizo kijijini alikozaliwa baba yangu na nilikwenda shambani na mfanyakazi wa baba wa shambani kufanya kazi. Kipindi hicho nilikuwa darasa la sita au saba hivi kama sisahau. Nyakati hizo baba yangu alikuwa akifanya kazi nje ya mkoa alikozaliwa hivyo sikuwa mwenyeji sana huko kwao. Na kwenye viunga vya shamba palikuwa na miwa mingi sana iliyostawi saaaana. Nilipomwambia yule mfanyakazi wa shamba la baba nina hamu na miwa alikwenda kukata miwa mingi na kisha alinishauri tujifiche ili tusijeonekana na mwenye shamba hilo. Na kwa hiyo tulianza kula ile miwa tukiwa tumejificha katika vichaka bila kujali hatari ya kung'atwa na nyoka. Kila kelele yoyote hata ya mdudu, ndege au panya iliposikika roho yangu ilikuwa juu juu kwamba tumekamatwa na mwenye shamba. Nakumbuka niliumwa sana na wadudu weusi mithili ya sisimizi. Sikuwa na starehe kabisa muda wote na sikufurahia kabisa utamu wa miwa ile mizuri.

Baada ya siku si nyingi nilikwenda tena shambani kule kule ila safari hii nilikwenda na marehemu bibi yangu. Baada ya kazi alikwenda kukata miwa kwa ajili yangu. Ajabu aliikata pale pale. Nami nilimtahadhalisha kwamba 'bibi mbona unakata miwa ya watu bila kibali chao?' Aliniangalia kwa sura ya tabasamu na kuniambia kibali unachohitaji ni cha nani wakati miwa ni yangu na nimeipanda mimi? nilimuuliza maswali mengi na mwisho nikajitolea kumsimulia yalitokea nilipokuwa na yule mfanyakazi. Alishangaa sana na akanipa kibali kuwa tangu siku ile nikitaka muwa niende nivune wala nisiogope maana ni haki yangu.

Ndivyo ilivyo kwa watanzania wengi kutojua haki yao wamepoteza nafasi nzuri ya kujikwamua katika lindi la ghiriba ya hawa mabepari na wezi weusi wanaowatisha usiku na mchana. Watu bado wanajiandikisha kupiga kura lakini hawaendi kupiga kura. Watu wengine wanauza shahada kwa sababu hawajui haki yao kikatiba kwamba hiyo kura inampa haki ya kumiliki shamba la miwa kama ilivyokuwa kwangu. Wengi wamejaa woga, ujinga na wanadanganywa kwa vitu vidogo vidogo kama watoto wanavyodanganywa kwa kupewa wanasesere.

Watu waelekezwe wafunguke na kujua haki zao.

KUPIGA KURA NI HAKI YA KILA MTANZANIA.

TUSIDANGANYIKE
 
Kupiga kura ni haki ya msingi na haki ya kikatiba ya kila mwananchi aliyefikia umri wa miaka 18.

Ingawa haki hii imekuwa kiini macho huko Tanzania. Lakini usiache kupiga kura.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom