Hivi ni kweli kuna watu wana nguvu (Pawa) za asili au ni mazingaombwe tu?

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
1,896
2,711
Wakuu habarini za leo tena, nina mda sijaandika chochote humu hii ni kutokana na kuwa bize kwa mda kidogo ila leo katika pitapita zangu huko fesibuku nimekutana na video ya ajabu sana, maana mambo ambayo tulikuwa tunasoma kwenye magazeti na kwenye vitabu vya hadhiti cha ajabu leo nimeshuhudia yakifanyika na kijana wa kitanzania hapahapa nyumbani.

ETI Jamaa ana uwezo wa kunyanyua bodaboda ikiwa imepakia abiria kwa mdomo, pia ana uwezo wa kuzuia magari mawili kwa mwili wake na yasitembee, anao uwezo wa kubeba njemba mbili tena kwa mkono mmoja na kutembea nazo kama kwamba hajabeba chochote, Hapa swali langu ni je?

Kama mambo haya ni kwel? kwanini watu hawa wasipewe nafasi wakawa hazina ya taifa, au kwanini wasijiunge na michezo ya masumbwi na mieleka watuwakilishe, au wajiunge na jeshi la polisi ili kuwadhibiti hawa panyaroad kuliko kutumia nguvu zao kwenye maonesho ya kuchangiwa 300, 200, ambazo hazina msaada kwao?

NB kwa wale matomaso wanaotaka video sijapata accessories ya kuiapload hapa. ila source ni video ipo kwenye page ya AFRIMAX. Wazoefu tuambieni hawa jamaa wanatumia nguvu gani?"
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom