Hivi ni kweli kuna wanawake wenye viungo vya uzazi vya kiume?

Askarimtu

JF-Expert Member
Sep 7, 2019
277
185
Katika mihangaiko ya hapa na pale nimeona kitu hiko hapo juu, ambacho kweli sijawahi kupata ushuhuda/ habari za maana ili kukiamini.

Lakini nikakumbuka kuwa mwaka fulani niliambiwa kuwa katika shule moja ya wasichana ya bweni, kuna msichana alikuwa ni mwanamke kwa nje lakini kwa ndani ni mwanaume ila baadhi ya wenzie walimfichia hii siri kwa sababu zao wenyewe, na wala walimu hawakujua hii kitu. Nikamuuliza yule aliyekuwa ananiambia, ''wewe, ni hapa hapa Tanzania au?''' Mara nikaona stori imepeperuka na upepo, lakini hiki kitu nilikiweka kichwani japo sikukiamini mpaka leo siamini.

Juzi tu hapo, nimeona pia habari kuna msichana kafanyiwa upasuaji ili kukamilisha sehemu yake ya kiume iliyoota juu ya sehemu ya kike; Uganda.

Ukiacha hizo hapo juu, kuna jamaa katika mtandao mmoja amesema kuwa; kuna msichana wa kazi alidai kuwa amepewa mimba na boss wake wa kike, watu wakamwambia wewe umechanganyiwa, hakuna kitu kama hicho; msichana akajibu ni kwasababu hamjui kama boss wangu ni mwanaume kwenye viungo lakini ni mwanamke kwa mwonekano (nywele ndefu, matiti, nyonga, sauti, mwendo)

Sasa: Madaktari kama hi hali ipo kweli, hii hali inasababishwa na nini? Na, kama watu hawa wapo kweli katika jamii wanatambulikaje au ndio wanafichwa tu?

Assume sasa, kijana ndio kakutana na huyu bidada wa aina hii na kampenda kwelikweli; na vijana wa sasa hivi tulivyo ving'ang'anizi, daah!

Nasikia pia katika Uislamu kuna kitu kinaitwa KHUNTHA ndicho kinachowatambulisha watu wa aina hii (sina uhakika).

Ambao mmeshakutana au kusikia habari hizi tusaidieni kutoa stori zenu labda tutapata picha kamili kwa mawazo ya wengi!

NB: Nataka elimu tu na taarifa, sipo katika kukejeli kundi fulani la watu.
 
  • Thanks
Reactions: THT
Shemale ni hali ya kawaida tu ili mradi ujue kipi kinafanya kazi 💯%

Waache kinachofanya kazi tena ukiwa mdogo. Nimeishi na jamaa ana uke lakini haina kazi wazazi walimficha.
 
Hebu nenda kagoogle Hermaphrodite utapata majibu yako. Lakini sasa hivi watu wenye jinsia mbili hawatambuliki tena kama Hermaphrodite bali INTERSEX, na tayari wapo kwenye LGBTQI Community, ni watu wanaobaguliwa tangu wanapozaliwa, huonekana wa ajabu ndiyo maana hata wazazi huwaficha.

Nina rafiki ni Intersex, ukimuona ni mwanamke wa haja lakini ana wachakaza madada duu hatari, lol, wesiomjua hudhani ni lesbian kumbe ni jibaba.

NOTE: Hermaphrodite/ Intersex siyo Shemale, hao ni watu wawili tofauti.
 
culture gal,
Naona na wewe ni member. Lakini vipi hawa watu hamna historia yeyote kutoka kwa wazazi wao ambayo inaweza ikawa chanzo cha wao kuwa hivo?

Labda mama alikuwa tasa muda mrefu au mama alizaa katika umri mkubwa sana au mtoto alizaliwa nje ya mfumo wa mwili wa mama yaani labda kwenye test-tube au hata labda mtoto alikaa tumboni miezi 11.

Hujawahi kusikia chochote?
 
Wapo kibao sema wengi wanakimbilia kucheza video za ngono huko ulaya. Kuna mdada mmoja miaka ya 2010 alikuwa anaendesha bodaboda anajinsia ya kiume na anawachakaza warembo.
 
Tafuta Sana mtandaoni utaona ipo video,
Intersex hawi na jinsia mbili kamili,niliyemuona mtandaoni anamuonekano wa kiume na ana uke lakini juu ya uke Kuna penis ndogo Sana na Hana korodani,
Huyu yupo africa
 
Niliwahi kusikiaga kwenye hekaheka huko shinyanga mtoto wa kike ana jinsia mbili ya kiume ndiyo inanguvu Sana..wazazi na nduguze wengine walikua wanalazimisha awe ki-kike.. mwenyewe anataka awe wa kiume...
 
Niliwahi kusikiaga kwenye hekaheka huko shinyanga mtoto wa kike ana jinsia mbili ya kiume ndiyo inanguvu Sana..wazazi na nduguze wengine walikua wanalazimisha awe ki-kike.. mwenyewe anataka awe wa kiume...
Unajua kinachotambulisha jinsi yake ni kile kilichopo ndani yake, sawa muonekano wake ni wa kike lakini jinsi yake iliyo na nguvu ni ya kiume, kumlazimisha awe kulingana na muonekano wake ni kumkosea heshima na kumdhulumu nafsi yake.
 
Unajua kinachotambulisha jinsi yake ni kile kilichopo ndani yake, sawa muonekano wake ni wa kike lakini jinsi yake iliyo na nguvu ni ya kiume, kumlazimisha awe kulingana na muonekano wake ni kumkosea heshima na kumdhulumu nafsi yake.
Kabisa haujakosea.

Dogo alitoroka kwao akaja dar kuomba achangiwe pesa abadilishwe awe wa kiume.
 
Wapo kibao sema wengi wanakimbilia kucheza video za ngono huko ulaya. Kuna mdada mmoja miaka ya 2010 alikuwa anaendesha bodaboda anajinsia ya kiume na anawachakaza warembo.
Huyo mdada hakua na jinsia mbili wala nini, alikua ni lesbian mwenye dildo yake ndio akawa anawapanga hao warembo.... Intersex mara nyingi wapo shy na vile walivyo na mara nyingi huishia kua asexual.
 
Back
Top Bottom