Hivi ni kweli kama kuna jambo kubwa la maana unataka kulifanya, ni bora msikutane kimwili na mwenza wako?

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,198
6,416
Habari wadau wa nguvu wa JF.

Nimesikia watu wakisema mapenzi yana gundu. Yaani kama kuna jambo zuri lenye manufaa unataka kulifanya, eti ni bora msifanye mapenzi na mapenzi/mchumba/ mume au mkeo hadi utakapoanza kufanikisha jambo hill.

Mara nyingi mambo kama hayo ni Maombi/sala, interview ya kazi, kufungua biashara Mara ya kwanza, safari, na nyinginezo.

NB: Masuala hata ni yale ya muda mfupi wa siku moja wiki au wiki mbili. Sio mtengane mwezi au mwaka utaibiwa.

Mdau moja kaenda mbali na kusema hata katika Bible, Waisraeli wakipitia jambo gumu hutengana na wenza wao kwa muda.

Wajuvi karibuni kwa michango yenu.
 
hii inatumika kwa wenye akili timamu ni mambo ya kiroho zaidi..ukweli ndio huo
 
Halafu haya magundu yapo Afrika tu! Hivi huwa mnakosa vitu vya kusingizia au ndo kubakwa kiakili...?
Unahabari kuna watu huwa bongo zao zinafanya kazi vizuri baada ya sex..? Mtu hapo anatoka na bonge la wazo ambalo hapo kabla hakuwa nalo unalifahamu hili
 
Hata sifahamu
 
Habari wadau wa nguvu wa JF.

Nimesikia watu wakisema mapenzi yana gundu. Yaani kama kuna jambo zuri lenye manufaa unataka kulifanya, eti ni bora msifanye mapenzi na mapenzi/mchumba/ mume au mkeo hadi utakapoanza kufanikisha jambo hill.

Mara nyingi mambo kama hayo ni Maombi/sala, interview ya kazi, kufungua biashara Mara ya kwanza, safari, na nyinginezo.

NB: Masuala hata ni yale ya muda mfupi wa siku moja wiki au wiki mbili. Sio mtengane mwezi au mwaka utaibiwa.

Mdau moja kaenda mbali na kusema hata katika Bible, Waisraeli wakipitia jambo gumu hutengana na wenza wao kwa muda.

Wajuvi karibuni kwa michango yenu.
Ingekua ni kweli, basi kwa sisi tuliooa na ambao hatujui swala hilo hakuna jambo letu hata moja lingefanikiwa maana sisi tunabutua tuu kuwe na jambo la kufanya ama laa.
 
1 Wakorintho 7:5
[5]Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.

Kwa wanaofuata biblia muongozo huo hapo.......hivyo kwa mujibu Wa imani ya kikristo na wasomaji wengine Wa Biblia hilo uloandika ni sahihi....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa nukuu mkuu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom