SnowBall
JF-Expert Member
- Sep 13, 2011
- 3,054
- 2,840
Kuhusu dhana ya TABIA waswahili wana misemo mingi tu...mfano kuna msemo kama 'TABIA NI KAMA NGOZI HAIBADILIKI'....lakini hawajaishia hapo tu wakati mwingine utasikia msemo kama 'MAZOEA HUJENGA TABIA'...Hizi zote ni semi zinazobeba MAANA kubwa tu, na zote ukizifuatilia kwa Makini utaona zinaongelea kitu kile kile... Binafsi naamini kuwa TABIA inaweza kubadilika au mtu mwenye TABIA flani anaweza badilishwa na ninawashangaa wanaosema haiwezekani!!...kwa mfano ninaamini TABIA hujengwa na kama kitu kinajengwa naamini pia kinaweza KUBOMOLEWA!!!...Unaweza ukajijengea TABIA ya Ulevi na ukawa MLEVI lakini kupitia mafundisho na maonyo unaweza kuacha ulevi na ukawa mtu safi kabisa..
Kinachonisukuma kuandika hii thread ni tabia flani ambazo nimeziona kwenye MAHUSIANO...Unakuta mwenzio ana katabia flani ambako labda kanakukera na uzuri au ubaya ukute hata yeye mwenyewe anakiri kuwa hiyo ni TABIA yake...na labda ukiongea naye Utasikia anakuambia NIZOEE tu hii ni TABIA yangu..Sasa Jamani wanaJAMVI....Hivi ni KWELI KABISA KUNA TABIA HAZIWEZI BADILIKA!!!...Na kama jibu ni NDIYO..Hivi sasa utaishije na mtu ambaye ameshakiri kuwa hawezi badilika????...Hainihusu personally but nimeona nishee uzoefu wenu kupitia hili!!!..Na swali langu ni hili...''Ni kweli TABIA HAINA DAWA''??????............