Hivi ni kweli kabisa kwamba Kansa na UKIMWI havina tiba au ni biashara za makampuni makubwa duniani?

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,628
Leo nilikua nafuatilia kipindi kimoja kwa tv kuhusu ugonjwa wa saratani na walikua wanajadili ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake.

Katika huko ndo nikawaza na kuwazua ndugu yenu. Hivi ni kweli kabisa kwamba kansa na UKIMWI havina tiba au ni biashara za makampuni makubwa duniani?

Hii inawezekana vipi? Inaingia akilini kweli?

Inaingilia akilini kwamba saratani na virusi UKIMWI havina tiba?

Haingii akilini kwamba mimea yote duniani imekosa kutibu haya magonjwa.

Nini tunafichwa? Au ni makampuni makubwa ya nje yananufaika na haya magonjwa? Halafu, why HIV ipo zaidi Africa, tena Sub Sahara?

Hebu tuwaze na kuwazua leo wanajamii.
 
Utaelewa mambo mengi sana kiongozi ila hivi vitu ni biashara. . Ngoja nikwambia
Injection Moja ya anti-Cancer avastin last time I checked ilikuwa 1200,000
ARV mnazoziona sijui nini ni $300-600 per dose of 1/12.
Sasa piga $300×12x36,000,000 HIV income a yr...hujaweka sales ya Septrin na dawa nyingine.

Kwamba US wanafaidikaje na msaada ya Ukimwi jiulize ji jibu mwenyewe.

Kuna watu 9.5M duniani wanaugua Cancer.. sasa piga 4×1.2M×9.5M uje uniambie inakuwaje..

Roche, Mylan, Sanofi, Pfizer ni syndicate tu...
 
Aisee

Waafrika tunaelewa hayo..?

Ndo kwanza tupo kwenye ndumba na kuomba koneksheni zikivuja video za udambwidambwi!.. Tena unaweza kuta hata daktari mzima nae alikuwa akiomba koneksheni ya kupata ile video ya mwana chuo!.. Sasa tafiti atafanya sangapi..? Sisi wengine huku hata hatujui ndo kwanza tunaimba singeli unatoa hutoi.. we dada unatoa hutoi..😂
 
Hayo magonjwa yapo mkuu na dawa hakuna,endelea kujikinga tu,ila kama unataka kujifariji kuwa hayapo ili ufaidi,just do it at your own risk...
 
Halaf ni kweli zile connection nilimshuudia hadi dr mmoja mzito mmama anaomba connection
Waafrika tunaelewa hayo..?

Ndo kwanza tupo kwenye ndumba na kuomba koneksheni zikivuja video za udambwidambwi!.. Tena unaweza kuta hata daktari mzima nae alikuwa akiomba koneksheni ya kupata ile video ya mwana chuo!.. Sasa tafiti atafanya sangapi..? Sisi wengine huku hata hatujui ndo kwanza tunaimba singeli unatoa hutoi.. we dada unatoa hutoi..
 
Umeenda mbali mno

Mbu aenezae malaria tumeshindwa kumtokomeza mbu! Tunatumia hela nyingi sana kukabiliana na magonjwa haya ilhali ukifikiri kwa kina ilikuwa ni suala la kutafiti tu namna ya kumtokomeza mbu akatoweka kabisa asiwepo tena lakini hola

Kuku hasa wa kienyeji huwa wanashambuliwa na magonjwa lukuki tofauti tofauti kama vile kuvimba midomo na kadhalika, ukiwaona wataalamu wa kilimo na mifugo hawana majibu yaliyo sahihi ya kutatua changamoto hizi pamoja na usomi wao maprof na madokta lakini bure kabisa

Kazi kweli kweli
 
Hili jambo naibua mada kabisa.......kuna jambo nimelikumbuka
Umeenda mbali mno

Mbu aenezae malaria tumeshindwa kumtokomeza mbu!

Kuku hasa wa kienyeji huwa wanashambuliwa na magonjwa lukuki tofauti tofauti kama vile kuvimba midomo na kadhalika, ukiwaona wataalamu wa kilimo na mifugo hawana majibu yaliyo sahihi ya kutatua changamoto hizi

Kazi kweli kweli
 
Leo nilikua nafuatilia kipindi kimoja kwa tv kuhusu ugonjwa wa saratani na walikua wanajadili ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake.

Katika huko ndo nikawaza na kuwazua ndugu yenu. Hivi ni kweli kabisa kwamba kansa na UKIMWI havina tiba au ni biashara za makampuni makubwa duniani?

Hii inawezekana vipi? Inaingia akilini kweli?

Inaingilia akilini kwamba saratani na virusi UKIMWI havina tiba?

Haingii akilini kwamba mimea yote duniani imekosa kutibu haya magonjwa.

Nini tunafichwa? Au ni makampuni makubwa ya nje yananufaika na haya magonjwa? Halafu, why HIV ipo zaidi Africa, tena Sub Sahara?

Hebu tuwaze na kuwazua leo wanajamii.

Mimi hua nawaza hivi:

1. Maendeleo ya sayansi na teknolojia sio makubwa kiasi tunachoaminishwa.

Kama kuna ugonjwa ambao hauna dawa mpaka leo hii mwaka 2020 ambapo tunaambiwa dunia ipo kwenye kilele cha maendeleo ya sayansi na tekenolojia, basi inawezekana hayo maendeleo tunayoambiwa pengine ni kiini macho! Haiingii akilini kwamba wanasayansi wanaweza kurusha vyombo kutoka duniani kwenda sayari nyingine kama Mars, Jupiter, Pluto na hadi nje ya solar system mamilioni ya maili kutoka duniani, halafu eti hatuwezi kutengeneza dawa ya kansa, ukimwi, kisukari, maleria, nk. Huu utakua ni utopolo wa hali ya juu!

2. Maendeleo ya sayansi na teknolojia ni makubwa kama tunavyoaminishwa.

Kama maendeleo ya sayansi na teknolojia ni makubwa kiasi tunachoaminishwa, basi hakuna ugonjwa usio na dawa. Magonjwa yote yana dawa ambazo mtu ukipewa unapona kabisa na kurudi kuwa mzima. Tatizo ni kwamba, hati miliki za dawa hizo zinamilikiwa na makampuni binafsi ambayo hua yanatumia mamilioni ya fedha kwenye tafiti ili kutengeneza hizo dawa. Kwahiyo lazima watafute jinsi ya kurudisha pesa zao. So wanachofanya wakishapata dawa, mfano kama walivyopata ya ukimwi, badala ya kuwapa wagonjwa ili wapone kabisa, wao wanaichanganya na maji mengi ili isikuponyeshe kabisa lakini ikupunguzie tu makali ili uendelee kuishi na kuinunua miaka nenda rudi na wao waendelee kupata faida. Ndio maana magonjwa yote makubwa yana dawa za kufubaza ambazo mtu anatakiwa kutumia mpaka mwisho wa maisha yake, na sio dawa za kuponya ugonjwa. Kwahiyo huenda dawa zipo, ila ukipewa ukanywa na kupona kabisa maana yake wao wamepoteza mteja!

Hayo ndio mawazo yangu.
 
Mimi hua nawaza hivi:

1. Maendeleo ya sayansi na teknolojia sio makubwa kiasi tunachoaminishwa.

Kama kuna ugonjwa ambao hauna dawa mpaka leo hii mwaka 2020 ambapo tunaambiwa dunia ipo kwenye kilele cha maendeleo ya sayansi na tekenolojia, basi inawezekana hayo maendeleo tunayoambiwa pengine ni kiini macho! Haiingii akilini kwamba wanasayansi wanaweza kurusha vyombo kutoka duniani kwenda sayari nyingine kama Mars, Jupiter, Pluto na hadi nje ya solar system mamilioni ya maili kutoka duniani, halafu eti hatuwezi kutengeneza dawa ya kansa, ukimwi, kisukari, maleria, nk. Huu utakua ni utopolo wa hali ya juu!..
Futa hoja yako yakwanza mkuu maana kwanza hatujafika kilele cha teknolojia Wala sayansi pili kuwa na uwezo wa kupeleka vyombo nje ya dunia yetu haimaanishi kuwa ndo tuwe na dawa za hayo magonjwa.. kumbuka hizi ni sekta mbili tofauti na kila moja inafanya kazi kutokana na uwezo wake hao mainjinia waadude ya anga wameshahangaika Sana mpk kufikia hapo walipo na kumbuka kufanikiwa kwao hivyo ndo maana nzima ya utajiri wao!.. hao wataalum wa afya itakuwa wanayao tu Kama hoja yako yapili inavyoeleza.
 
Tuna shida kubwa sana katika nchi zetu hizi, wasomi wanatueleza ngazi zao za juu sana kielimu lakini wanashindwa kutatua changamoto ndogo mno zinazotukabili kama jamii

Yaani huwa namfikiria "mbu" alivyo mdogo na mwepesi kufa kisha nalinganisha na adha tunayoipata katika kupambana na malaria na gharama zake hadi nabaki naona kama kiini macho vile

Ni kweli kwamba wataalamu wetu wasomi wabobezi wameshindwa dawa ya kumtokomeza mbu!!??????? Ni aibu kwa namna fulani
 
Solution Waafrika tuingie polini kimya kimya tutafute dawa ya hayo magonjwa tunywe lakini tukiendelea kuleta udhaifu wetu wa utegemezi kwa Wazungu tutazidi Keisha tu ilihali miti tunayo
 
Back
Top Bottom